Jumamosi, 26 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  20 Sha'aban 1444 Na: 1444 / 28
M.  Jumapili, 12 Machi 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mfumo wa Kidemokrasia wa Serikali Haujaipatia Pakistan Chochote ila Machafuko na Ukosefu wa Utulivu. Hakikisheni Dola Imara na Thabiti nchini Pakistan kupitia Kusimamisha Khilafah!

(Imetafsiriwa)

Machafuko na ghasia za kisiasa juu ya kufanya uchaguzi mapema au kuchelewa, ni aina ya hivi karibuni ya ukosefu wa utulivu wa Pakistan. Tatizo hili limekuwa likiendelea kwa miongo kadhaa iliyopita. Linatokana hasa na mfumo wa kidemokrasia wa serikali yenyewe. Demokrasia inahimiza ushindani kati ya watu binafsi na vyama vya kisiasa kwa ajili ya madaraka na mamlaka. Kila baada ya miaka michache, mvurugiko wa uchaguzi huongeza ushindani juu ya haki ya kuteua watu kwenye taasisi muhimu za serikali. Kuna ushindani wa uteuzi wa mkuu wa jeshi, Mkurugenzi Mkuu wa ISI, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu na majaji wa Mahakama ya Upeo. Vyama vya kisiasa vinapigana vyenyewe kwa vyenyewe ili kuamua watu wanaowapendelea katika taasisi hizi. Pande hizo pia zinachuana kuwania mawaziri wa shirikisho na mikoa, mawaziri wakuu, magavana, spika wa bunge, naibu spika, kamati ya hesabu za serikali, kamati nyengine za kudumu na mkuu wa Afisi ya Taifa ya Uwajibikaji. Demokrasia inahimiza ushindani wa udhibiti wa serikali ambao unavuruga serikali na jamii.

Mabadiliko ya serikali kila baada ya miaka mitano au zaidi hufanya dola nzima kutofanya kazi vizuri. Kukosekana kwa utulivu huanza kabla ya mwaka wa uchaguzi. Kisha, katika kipindi chote cha uongozi wa serikali, upinzani, na vikundi vyenye nguvu vilivyounganishwa nao, vinajaribu kuidhoofisha serikali. Kudhoofisha huku kunasababisha serikali kushindwa, ili wapinzani wachukue madaraka katika uchaguzi ujao. Hivi ndivyo ilivyo Marekani na nchi nyingine za kidemokrasia pia. Katikati ya ukosefu wa utulivu, serikali imeshughulika na kujilinda na kujaribu kuongeza muda wa mamlaka yake. Hii inasababisha kutokuwepo kwa mipango ya muda mrefu kuhusu nishati, ujenzi wa viwanda, usalama wa chakula, kujitosheleza, uwezo wa kimkakati wa kijiografia na utawala wa kimataifa.

Kasoro nyengine ya demokrasia ni kwamba mtu yeyote asiye na uwezo anaweza kuwa mtawala kwa misingi ya umaarufu wake. Wasio na uwezo basi wanaweza kuidhinisha na kutabanni sheria na sera zinazodhuru maslahi ya watu na serikali. Hii ni kwa sababu katika demokrasia ubwana uko kwa watu, huku katika Uislamu, ubwana ni kwa Shariah. Katika Uislamu, katiba, sheria na sera huamuliwa kwa maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw). Haziwezi kubadilishwa hata na Khalifa mwenyewe. Kwa hiyo, hakuna mtu maarufu au kundi lolote linaloweza kudhuru maslahi ya Ummah na Dini yake, Uislamu.

Katika mfumo wa Kiislamu, mamlaka ni kwa Khalifa aliyechaguliwa, baada ya kuteuliwa kupitia Bayah. Analazimika kutawala tu kwa Shariah. Anaweza kuwakilisha mamlaka fulani kwa kumteua afisa. Anaweza kuondoa mamlaka kwa kumwondoa yeyote anayemtaka. Khalifa anatawala maisha yaka yote kwa sharti kwamba Shariah inatekelezwa. Hii inahakikisha utulivu wa kisiasa, badala ya dhulma ya kisiasa. Khalifa hutabikisha sera za muda mrefu ili kuhakikisha ufuasi wa maamrisho na makatazo ya Shariah. Kila chama cha kisiasa ndani ya Khilafah kinamhisabu Khalifa kwa msingi wa kuamrisha mema na kukataza maovu. Hii inaimarisha dola na kurekebisha upotokaji. Ndani ya Khilafah, vyama vya kisiasa havishindanii mamlaka. Badala yake, vinamsaidia Khalifa katika kutabikisha Uislamu. Vinamtahadharisha Khalifa juu ya mapungufu na kufeli. Vinahakikisha kwamba Khalifa anashikamana na utabikishaji wa Shariah.

Pakistan kwa sasa imesimama kwenye njia panda. Inaweza kupata ima utawala wa kikanda na kiulimwengu kupitia kusimamisha Khilafah au inaweza kuwa dola dhaifu mithili ya Bhutan mbele ya Dola ya Kibaniani kwa kubakia chini ya Demokrasia.

Basi, Enyi Watu Wenye Nguvu! Njooni mutimize jukumu lenu. Ipeni Nusrah Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, ambayo itabadili mwenendo wa Ummah huu, inshaa Allah. Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

(وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ)  

“Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu” [Surah Ar-Rum 30: 4-5].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu