Jumanne, 17 Muharram 1446 | 2024/07/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  15 Ramadan 1444 Na: 1444 / 31
M.  Alhamisi, 06 Aprili 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Enyi Majeshi ya Pakistan! Je, Hakuna Salahuddin miongoni Mwenu wa Kuukomboa Msikiti wa Al-Aqsa?!

(Imetafsiriwa)

Enyi Waislamu wa Pakistan!

Kibla cha kwanza cha Dini yetu, sehemu iliyobarikiwa ya Isra’a na Miraji ya Mtume (saw), imenajisiwa katika mwezi mtukufu zaidi wa Ramadhan. Quran Tukufu, ambayo iliteremshwa katika mwezi huu uliobarikiwa, imechanwa na kuangushwa chini bila kujali. Mwanamke msafi wa Kiislamu ameburuzwa na kupigwa, huku damu ikiwa juu ya Hijabu yake, ambayo ilikuwa imevaliwa kwa ajili ya kumtii Mola wake (swt). Muislamu mtukufu alitupwa nje ya Al-Msikiti wa al-Aqsa, ili kutoa nafasi kwa walowezi wa Kiyahudi. Watu waoga zaidi kuliko watu wote, Mayahudi, wanazunguka-zunguka na kunguruma kama simba, huku wana wa Salahudin wakiwa wamefungiwa mithili ya wanyama wa kufugwa, ndani ya kambi zao za kijeshi.

Haitoshi kwenu kumwaga machozi. Haitoshi kwa damu yenu kuchemka. Haitoshi kwenu kuelezea huzuni na hasira yenu kwenye mitandao ya kijamii. Haitoshi kwenu kususia tende za umbile la Kiyahudi, walizozikuza kwenye ardhi za Waislamu. Ni wajibu juu yenu kuhakikisha kwamba ardhi zote za Palestina zinakombolewa kutokana na kukaliwa kimabavu, kila shubiri na kila futi mraba. Ni wajibu juu yenu kumkamata kila mmoja wa watoto wenu, kaka zenu, baba zenu na babu zenu katika jeshi la Pakistan na kuwauliza, “Je, hakuna hata Salahudin mmoja anayepatikana miongoni mwenu leo?!”

Enyi Waislamu wa Jeshi la Pakistan!

Munaona hasira kali ndani ya macho ya watu wa kawaida wanaokuzungukeni. Kwa hivyo munalazimika muweje?! Maisha yenu si ya watu wa kawaida. Watu wa kawaida hawafikirii zaidi ya kupanua biashara, kujenga nyumba na kusomesha watoto. Watu wa kawaida hudhihirisha hasira kwa ndimi zao na kauli zao, ilhali nyinyi mnatenda kwa silaha zenu. Maisha yenu lazima yawe ya shujaa wa Kiislamu, ambaye anatamani mwili wake usambaratike vitani, ili apate kuonja neema nyingi zilizotolewa na Mwenyezi Mungu (swt) kwa shahidi. Munaambiwa kwamba nyinyi ni jeshi la Khorosan linalomngoja Imam Mahdi, hivyo basi chukueni hatua sasa katika namna ya jeshi la waumini! Njia ya kweli ya jeshi la Waumini iko mbele yenu, inayo nyeshezwa kwa jasho na damu ya jeshi la Salahudin (rh). Jeshi la Salahudin kwanza lilianzisha umoja wa Umma wa Kiislamu chini ya Khalifah mmoja, akitawala kwa Uislamu. Kisha jeshi la Salahudin likajikusanya chini ya uongozi wa Khalifa, likitembea umbali mkubwa ili kupata heshima ya kuukomboa Al-Masjid Al-Aqsa. Kwa hivyo, lazima muchukue hatua sasa. Watupilieni mbali watawala hawa waovu na mutoe Nussrah yenu kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume. Hapo ndipo Khalifa Muongofu atakuongozeni katika Vita vya Pili vya Hattin, mwezi huu wa Ramadhan, ili kuwasagasaga wavamizi, kabla ya kupaza takbira za ushindi ndani ya Al-Masjid Al-Aqsa. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ]

“Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni” [Surah Al-Baqarah 2: 191].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu