Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  10 Jumada I 1441 Na: 1441 /35
M.  Jumatano, 15 Januari 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uislamu Unakataza kabisa Muungano wa Shughuli za Kijeshi na Mipango ya Mafunzo ya Kijeshi Pamoja na Dola ya Kikafiri ya Kivita, Amerika, ambayo husababisha Kuvuja kwa Siri za Kijeshi, na Kuchukua Maelezo na Kuajiri Maafisa wa Kijeshi kama Mawakala wa Amerika

Mnamo 4 Januari 2020, Naibu Katibu wa Amerika wa Mambo ya Asia Kusini na Kati, Alice Wells, alituma ujumbe kwenye mtandao wa Twittter, “Kuimarisha ushirikiano wa jeshi kwa jeshi juu ya kushirikiana katika vipaombele na kuendeleza maslahi ya usalama wa kitaifa wa Amerika, Rais wa Amerika aliagiza kuregeshwa tena kwa Elimu na Mafunzo ya Kijeshi ya Kimataifa (IMET) kwa Pakistan.” Mafunzo ya maafisa wetu wa Kijeshi katika taasisi za kijeshi huko Amerika ndio zana madhubuti za Amerika za kutafuta maelezo na kuwaajiri mawakala ndani ya uongozi wa jeshi. Kwa miongo kadhaa, uongozi wa kijeshi wa Pakistan unaoegemea mrengo wa Amerika umeandaliwa na taasisi za kijeshi za kikoloni kuamini kuwa muungano wa sumu na Amerika ni suluhisho la changamoto za kimikakati za Pakistan. Uongozi aina hii unaoegemea mrengo wa Amerika huyachoma majeshi yetu kama mafuta kwa kila mradi wa Amerika, lakini huwafunga wao minyororo katika kambi zao wakati muda umefika wa kumaliza ukandamizaji nchini Palestina, Kashmir iliyovamiwa, Myanmar, Iraq au Syria. Jenerali Pervez Musharraf, Jenerali Kayani, Jenerali Raheel na, sasa, Jenerali Bajwa wote ni bidhaa za mipango ya kijeshi ya kikoloni. Zaidi ya hayo, mipango ya mafunzo ya kijeshi ni milango ya ujasusi, kupitia milango hiyo Amerika husoma ufikiriaji, mafunzo na uwezo wa kijeshi wa vikosi vya majeshi yetu.

Uislamu unakataza mahusiano yote na dola ya kikafiri ambayo iko vitani na Waislamu. Uislamu hauruhusu hata Waislamu kuwa na mahusiano ya kidiplomasia na dola ya kikafiri iliyoko vitani nayo, achilia mbali uhusiano wa kijeshi, ushirikiano, mazungumzo ya kimikakati, mazoezi ya kushirikiana au mipango ya mafunzo. Mwenyezi Mungu (swt) asema, [الَّذِيۡنَ يَتَّخِذُوۡنَ الۡـكٰفِرِيۡنَ اَوۡلِيَآءَ مِنۡ دُوۡنِ الۡمُؤۡمِنِيۡنَ‌ؕ اَيَبۡتَغُوۡنَ عِنۡدَهُمُ الۡعِزَّةَ فَاِنَّ الۡعِزَّةَ لِلّٰهِ جَمِيۡعًاؕ] “Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je! Wanataka wapate kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu?” [An-Nisa:139]. Mtume (saw) amesema, «لا تستضيئوا بنار المشركين» “Musitafute muangaza kwa moto wa washirikina” (Ahmad, Nisai). Moto ni Kinaya cha Vita nakwa mujibu wa Uislamu unakataza mahusiano na serikali huru ya Kikafiri tulioko vitani nayo. Zaidi ya hayo, Mwenyezi Mungu (swt) amesema, [وَلَنۡ يَّجۡعَلَ اللّٰهُ لِلۡكٰفِرِيۡنَ عَلَى الۡمُؤۡمِنِيۡنَ سَبِيۡلًا] “Na Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda waumini” [An-Nisa:141]

Miongo saba ya muungano na Amerika, mazoezi ya pamoja ya kijeshi na mipango ya mafunzo ya kijeshi yametuhakikishia sisi udhalilifu wa sera ya kigeni. Sio tu kuwa Amerika ni adui wa wazi wa Waislamu, bali inafanya muungano wa kimikakati na maadui wetu wengine wa wazi, kuwaimarisha wao dhidi yetu. Kwa hivyo awezaje adui wa wazi kama huyu kutupatia sisi nguvu za kuaminika, usaidizi na mafunzo? Ni wakati wakuachana na muungano na dola za Kikafiri tunazopigana vita na kuukumbatia mradi wa Khilafah,ili kupata usalama, heshima na hadhi. Khilafah Rashidah kwa njia ya utume itaiunganisha Pakistan, Asia ya Kati na Mashariki ya Kati kama dola moja yenye nguvu, na kulazimisha kuiondoa Amerika kutoka katika dola ambazo haitajaribu tena kurudi. Mwenyezi Mungu (swt) Amesema, [اِنۡ يَّنۡصُرۡكُمُ اللّٰهُ فَلَا غَالِبَ لَـكُمۡ وَاِنۡ يَّخۡذُلۡكُمۡ فَمَنۡ ذَا الَّذِىۡ يَنۡصُرُكُمۡ مِّنۡۢ بَعۡدِهٖ وَعَلَى اللّٰهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ الۡمُؤۡمِنُوۡنَ] “Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani, basi, baada yake Yeye atakaye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu.” [Al-Imran:160]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu