Jumamosi, 21 Muharram 1446 | 2024/07/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  12 Jumada I 1441 Na: 1441 / 36
M.  Jumanne, 07 Januari 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kwa Kutumia FATF, Amerika Inadhibiti Sera yetu ya Ndani na Nje.

Uhuru wa Kweli unaweza kupatikana pekee kwa Kukataa Nidhamu ya Kikoloni ya Kimataifa

Utawala wa Bajwa-Imran unaendelea kuachana na maslahi ya Pakistan, kwa kujisalimisha kwa matakwa ya Amerika. Mnamo 6 Januari 2019, Bunge la Kitaifa lilipitisha mswada wa makubaliano ya usaidizi wa kisheria wa mwaka wa 2019, juu ya mahitaji ya FATF. Baada ya kupitisha mswada huu, Pakistan lazima itoe ushirikiano wa kisheria na nchi zote za kigeni, hata bila ya makubaliano ya pande mbili kuwepo kabla, ikiwa raia wake wanashutumiwa kwa shughuli ambazo Wakoloni huamua kama “Ugaidi.” Kwa hivyo, kivitendo wizara ya mambo ya ndani kwa sasa iko chini ya mamlaka ya Kitengo cha Kigeni cha Amerika kupitia ubalozi wake ndani ya Islamabad. Taasisi za kikoloni, kama vile UN, Mahakama ya Haki ya Kimataifa, IMF, Benki ya Dunia, mashirika ya kukadiria viwango vya mikopo na FATF, ni sehemu ya baada ya Vita vya Dunia vya Pili, ya miundombinu ya Amerika ya kulazimisha utawala wake juu ya ulimwengu. Mataifa yenye nguvu ya kikoloni yanafanyia mzaha uhuru wa serikali nyingine, wanaposhinikiza mabunge yao ya kidemokrasia kuwa kama mihuri, kupitia tishio la kikwazo au kuweka kwenye orodha ya kijivu na nyeusi. Utawala wa Bajwa-Imran hutenda kama kibaraka wa wakoloni, wakisalimisha ubwana wa kitaifa kwa nidhamu ya kitaifa ya kikoloni, bila upinzani wowote, kwa hivyo husalimisha mambo yetu kwa wale wanaotudhuru.

Kulazimisha sheria za kimataifa hata ni kinyume na ufahamu wao Wamagharibi wa ubwana wa kitaifa, lakini Wamagharibi wanaweka sheria zao katika nchi ambazo hazina heshima na hilo ni kupitia mashirika ya kimataifa kwa sababu nguvu za wakoloni hutumia mashirika haya ya kimataifa kuhakikisha serikali nyingine zimepunguzwa katika hali ya kiwete, mikoa nusu huru. Kiasli, dola zinapaswa kutekeleza kulingana na mikataba ya nchi mbili au hiyari ya kuendana na kanuni za kimataifa, kama vile utakatifu wa balozi au makubaliano ya waarabu kabla ya Uislamu kuzuia vita katika miezi mitukufu, kwa kuogopa maoni ya umma au ushawishi wa maadili, lakini kamwe sikupitia kulazimishwa kimwili au kutishwa na mamlaka. Uislamu umekataza kutii mamlaka yoyote ya Ukafiri, bila kujali inavyozingatia, kama vile Mwenyezi Mungu (swt) aliposema,

وَلَنۡ يَّجۡعَلَ اللّٰهُ لِلۡكٰفِرِيۡنَ عَلَى الۡمُؤۡمِنِيۡنَ سَبِيۡلًا]

“Wala Mwenyenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda waumini.” [An-Nisa :141]

Ulimwengu umejaa ukandamizaji kwa sababu ya nidhamu ya kikoloni ya kimataifa. Wakati umewadia wa kuunda mahusiano kati ya nchi kulingana na Quran na Sunnah, ili kuung’arisha ulimwengu na uadilifu wa Uislamu tena. Na ni nani zaidi ya Waislamu wanaostahili heshima ya kuukomboa ulimwengu kutoka katika nidhamu hii ya ukandamizaji? Leo maafisa wachache waaminifu katika vikosi vya jeshi la Pakistan wanaweza kuitawanya nidhamu ya kikoloni ya kimataifa, kupitia kusimamisha Khilafah, kufuatia ushujaa, maono na mipango na ufahamu wa kina wa Sultan Muhammad al-Fatih, ambaye tunamkumbuka katika mwezi huu wa Jumada al-Awwal kwa kuikomboa Konstantinopoli, kwa hivyo akapata heshima ya kutimiza bishara ya Mtume (saw). Kwa hivyo ni nani leo atakayefuata nyayo za al-Fatih katika vikosi vya jeshi la Pakistan, kupata heshima ya kutimiza bishara nyingine ya Mtume (saw), ile ya kurudi kwa Khilafah kwa Njia ya Utume?

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu