Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  6 Sha'aban 1444 Na: BN/S 1444 / 12
M.  Jumapili, 26 Februari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uhalifu wa Akaba Utaongeza tu Aibu na fedheha ya Mamlaka na Tawala hizo, Na Utaongeza Uovu na Jinai ya Adui
[إِنَّ هَٰؤُلَاءِ مُتَبَّرٌ مَّا هُمْ فِيهِ وَبَاطِلٌ مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ]
“Hakika haya waliyo nayo watu hawa yatakuja angamia, na hayo waliyo kuwa wakiyafanya yamepotea bure.” [Al-A’raf: 139]
(Imetafsiriwa)

Huku damu ya mashahidi wa Nablus ikiwa bado haijakauka, na waliojeruhiwa wakiwa bado wamefinikwa na damu yao wenyewe, ujumbe wa Mamlaka ya Palestina (PA), ambao sasa unaona uhaini kama mtazamo lakini badala yake kama njia ya maisha, unakutana na wahalifu wakubwa wa Kiyahudi chini ya mwavuli wa mkuu wa ukafiri na ukoloni wa kimataifa na mlinzi na mfadhili wa umbile la Kiyahudi, Marekani, na mbele ya uwepo wa mashahidi wa uhaini, tawala mbili za Jordan na Misri!

Wahalifu hawa wamekosa maadili yote na kuikanyaga mistari yote mekundu na manjano na hata mistari ya damu. Kwa hakika, Wallahi wao hawamiliki ulinzi zama za kijahilia, kwa hivyo hawakuiheshimu Dini yetu, wala udugu wala ahadi yetu. Nani angekubali kukaa na muuaji wa watu wake, kupanga naye mipango, na kufunga naye mapatano dhidi ya watu wake, isipokuwa msaliti na kibaraka?! Na nani anayemuunga mkono adui yake dhidi ya watu wake na akaichukulia jihad yao kuwa ni vurugu ambazo lazima zikomeshwe, isipokuwa msaliti muovu?! Aibu na fedheha iwe juu yao duniani, na ole wao na adhabu ya idhalilishayo kesho Akhera. Wanachofanya ni uovu.

Taarifa ya pamoja ilithibitisha, na kile kilichofichwa ndani yake ni kikubwa zaidi, kujitolea kwa makubaliano ya awali, kujitolea kwa pande hizo mbili kupunguza upambaji moto na kuzuia ghasia zaidi, na msisitizo juu ya hadhi ya kihistoria ya Jerusalem. Na umbile la Kiyahudi limejitolea kutojadili uasisishwaji nyumba za makaazi kwa muda wa miezi minne na kutoidhinisha vituo vipya vya nje ndani ya miezi sita. Na kwamba mkutano ufanyike tena mwezi Machi huko Sharm El-Sheikh ili kuthibitisha kufikiwa kwa malengo yaliyotajwa hapo juu.

Kwa kuzingatia hili, tuna nia ya kusisitiza mambo yafuatayo:

1- Mkutano na umbile la Kiyahudi katika wakati ambapo mikono yake inachuruzika damu kutokana na jinai zake huko Nablus, Jenin na kwengineko inachukuliwa kuwa ni kilele cha uhalifu, kutojali, usaliti na njama dhidi ya watu wa Palestina kwa kutafakari na nia mbaya.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَخُونُوا اللَّهَ وَالرَّسُولَ وَتَخُونُوا أَمَانَاتِكُمْ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ]

“Enyi mlio amini! Msimfanyie khiana Mwenyezi Mungu na Mtume, wala msikhini amana zenu, nanyi mnajua.” [Al-Anfal: 27]

2- Kuegemea juu ya kujitolea kwa umbile la Kiyahudi kwenye mikataba ni upuuzi wa kisiasa. Bali, kwenyewe ni kujiweka chini utiifu. Ni mtu gani mwenye akili timamu asiyejaribu kile kilichojaribiwa mara mbili, basi iweje kifanyiwe majaribio kwa miaka thelathini?!

[أَوَكُلَّمَا عَاهَدُوا عَهْداً نَّبَذَهُ فَرِيقٌ مِّنْهُم بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ]

“Je! Ati ndio kila wanapo funga ahadi huwapo kikundi miongoni mwao kikaivunja? Bali wengi wao hawaamini.” [Al-Baqara: 100]

3- Kujitolea kwa Mamlaka ya Palestina katika kupunguza kupamba moto na kuzuia ghasia, pamoja na jinai yake ya kuitaja jihad kuwa ni ghasia, ina maana tu ya kuwasaka na kuwatia mbaroni mujahidina na kuongeza kasi ya uratibu wa usalama katika kuwafuatilia, huku jinai ya Mayahudi itaendelea bila uangalizi au uwajibikaji. Kauli za Hanegbi ni ushahidi bora zaidi, ambao ulithibitisha kwamba hakuna uzuiaji wa makaazi au mabadiliko yoyote katika hali ya msikiti mtakatifu na hakuna vikwazo kwa shughuli za jeshi la Kiyahudi popote pale. Kinachoendelea usiku wa leo katika mji wa Hawara ni ushahidi na dalili tosha.

4- Kuzungumza juu ya kuhifadhi hadhi ya kihistoria ya maeneo matukufu haimaanishi kusimamisha uvamizi wa Mayahudi katika Msikiti wa Al-Aqsa, wala kuwazuia na kuwahangaisha wenye kuabudu. Badala yake, umbile hili la kihalifu litaendelea kutaka kuweka mgawanyiko wa kimaeneo na wa muda, kama lilivyofanya wakati wa serikali iliyopita, ambayo ilikuwa ikitangaza kuhifadhi hadhi ya kihistoria, huku uvamizi na mashambulizi dhidi ya msikiti yakiongezeka kwa wenye kuabudu na wale walio katika itikafu. Makubaliano haya ni idhini ya kimabavu wa Jordan-Misri kwa umbile hili kuendeleza uhalifu na mashambulizi yake, ambayo ilithibitishwa na Hanegbi katika taarifa yake iliyotajwa hapo juu.

5- Mazungumzo kuhusu kufungua njia za mawasiliano na kuimarisha uratibu kati ya pande hizo mbili ina maana tu kwamba PA itatoa huduma za usalama “zinazoheshimika” zaidi kwa umbile la Kiyahudi. Mfuasi anatambua kwamba hakuna suluhu za kisiasa kwa sababu Marekani imejishughulisha na mafaili muhimu zaidi na moto moto, na kwamba lengo la mikutano hii si chochote zaidi ya utulivu unaoifariji Marekani kutokana na shida ya faili hii yenye mwiba.

Enyi Watu wa Ardhi Iliyobarikiwa: Matukio hayo yamedhihirisha usaliti wa Mamlaka na tawala kwa namna ya ajabu, kwani tawala hizi hazikubaki na jani la mtini kufinika baadhi ya uchi wao, bali zaidi hazioni aibu kwa usaliti na ushirikiano wao na wale wanaokuuweni mchana na usiku, kwani wao wako karibu zaidi nao.

[يا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاءَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللَّهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.” [Al-Ma’ida: 51]

Basi jiepusheni nao na sera zao, na muelekeze maombi yenu kwa vikosi vilivyo hai katika Ummah wenu, kilio chenu kiguse masikio ya watu kama vile Al-Muutasim na Swalah ud-Din, na atayakusanya majeshi ya Waislamu ili kulitokomeza umbile la Kiyahudi na wafuasi wao, kutoka katika mizizi yao na kuuondolea Ummah maovu yao. Ambapo itatokea hivi karibuni, Mwenyezi Mungu akipenda, basi iaminini ahadi ya Mwenyezi Mungu na muuamini Ummah wenu, na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi na atakulipeni kwa mema yenu.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تَنْصُرُوا اللَّهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ * وَالَّذِينَ كَفَرُوا فَتَعْساً لَهُمْ وَأَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu * Na walio kufuru, basi kwao ni maangamizo, na atavipoteza vitendo vyao.” [Muhammad: 7-8]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu