Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  27 Shawwal 1444 Na: BN/S 1444 / 15
M.  Jumatano, 17 Mei 2023

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi

[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُواْ مَا عَاهَدُواْ اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُواْ تَبْدِيلاً]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab 33:23]
(Imetafsiriwa)

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina inamuomboleza mmoja wa wanaume wa Hizb kutoka kizazi cha kwanza ambaye alifanya kazi katika safu zake tangu miaka ya 1950, marehemu mbeba da’wah, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

Ustadh Muhammad Abdullah Amr (Abu Abdullah)

Aliyefariki dunia kwenda kwa rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu jana, Jumanne, tarehe 16/5/2023, baada ya kuhangaika na maradhi, alikuwa imara, mvumilivu na mwenye kutaraji hisabu.

Abu Abdullah alikuwa miongoni mwa Mashababu wa Hizb wachamungu na hodari, na alisoma kutoka kwa Marehemu Sheikh Abdul Qadeem Zalloum, Amiri wa pili wa Hizb, na alitumia ujana wake na uzee wake kufanya kazi ili kuregesha maisha kamili ya Kiislamu pamoja na Hizb. Alijulikana kwa ujasiri na uimara wake katika kubeba da’wah, ambayo kwayo alizunguka nayo miongoni mwa mashule, ambapo alifundisha lugha ya Kiarabu na elimu ya Kiislamu, na maisha ya umma baina ya watu, basi Mwenyezi Mungu amlipe kwa niaba yetu.

Mwenyezi Mungu amrehemu maiti wetu, rehema pana, na amjaalie makaazi katika Mabustani yake makubwa. Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutaregea. Mwenyezi Mungu awalipe mema familia na jamaa zake na awape subira na faraja.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu