Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 13 Rabi' I 1443 | Na: HTS 1443 / 07 |
M. Jumatano, 20 Oktoba 2021 |
Majibu kwa Vyombo vya Habari
(Imetafsiriwa)
Ndugu Mpendwa / Mhariri Mkuu wa Gazeti la Al-Sayha
Assalam Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh
Mada: Jibu kwa mwandishi wa makala: “Uislamu wa Kisiasa... Shajara za Baruti na Damu”
Tulipitia makala ya mwandishi Ahmed Musa Qurei'i yenye kichwa "Uislamu wa Kisiasa... Shajara za Baruti na Damu" katika gazeti lenu la Al-Sayha Toleo 2411 la tarehe 20/10/2021, ambamo alishambulia kwa tuhma, na hata matusi dhidi ya makundi ya Kiislamu, na chuki yake iliyofichika haikuonekana tu kwa vyama na harakati hizi bali zaidi, chuki yake dhidi ya Uislamu mtukufu ni miongoni mwa mikunjo ya makala yake, kama vile alipokuwa akisema, “Katika kukinai kwangu kuna dhamira moja tu ambayo ndio sababu ya huu “msiba wa Kiislamu,” dhamira hii ni utukufu wa Uislamu wa kale” Utukufu wa Uislamu kwa mujibu wa mwandishi ni “msiba”, La Hawla Wala Quwwata Illa Billah (hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu)!
Mwandishi aliitaja Hizb ut Tahrir miongoni mwa makundi mengine ya Kiislamu na akasema, “Makundi haya yanatofautiana katika mitazamo, fikra, miondoko na misimamo mikali, kila moja kulingana na uwezo wake wa kifikra, chanzo cha ufadhili, na mbinu za “udanganyifu na uovu”. Baadhi yao hawatosheki na ndoto zao, kama vile Hizb ut Tahrir, ambayo inataka kusimamisha Khilafah ya kimataifa kwa njia ya Utume…
Kwa mujibu wa haki yetu ya kujibu, tunakuomba uchapishe jibu lifuatalo kwa mwandishi huyo:
Kwanza: Mwandishi alisema: “Neno Uislamu wa kisiasa lilionekana kuelezea harakati za Kiislamu zinazoamini kuwa Uislamu si dini tu, bali ni mfumo wa kisiasa, kijamii, kisheria na kiuchumi ambao unafaa kwa utawala na ujenzi wa taasisi za dola, lakini je! Ni sababu na dhamira zipi zilizopelekea kuibuka kwa neno hili hatari... Tunasema katika kujibu hilo, Uislamu ni dini kamili iliyoletwa na Mtume Muhammad (saw) ili kupanga maisha ya mwanadamu, iwe ya kisiasa, kiuchumi, kijamii au mengineyo, na hili linajulikana kutoka katika dini kwa udharura, isipokuwa kwa wale ambao macho yao yamepofushwa na Makafiri wa Magharibi ya kikoloni, na ufahamu wao umezibwa kwa kufuata matamanio ya makafiri, Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
[الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الإِسْلاَمَ دِيناً]
“Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini. Na mwenye kushurutishwa na njaa, bila ya kupendelea dhambi, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye kurehemu.” [Al-Maida 5:3]. Na Yeye (swt) pia asema:
[وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ تِبْيَاناً لِكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً وَبُشْرَى لِلْمُسْلِمِينَ]
“Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu,na rehema, na bishara kwa Waislamu.” [An-Nahl 16:89].
Zaidi ya hayo, Mustafa kipenzi alisimamisha dola kwa msingi wa Uislamu yenye mawazo ya Wahyi mtukufu. Ilikuwa ndio chanzo cha hadhara ya kipekee, ambayo maadui waliishuhudia mbele ya marafiki. Ilikuwa ni dola ya Uislamu iliyodumu kwa zaidi ya karne kumi na tatu. Dola ya kwanza kuhusiana na hadhara, thaqafa na siasa, na iliendelea hadi ilipopinduliwa na Makafiri wa kikoloni kwa msaada wa wasaliti wa Waarabu na Waturuki.
Pili: Hizb ut Tahrir, inayotaka kurudisha mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, haifanyi kazi hii kama ndoto, kama mwandishi alivyodai, bali badala yake inaitekeleza kama faradhi ya kisheria, ambayo Ummah ni lazima uifanye, vyenginevyo itakuwa ni dhambi, kwa sababu Uislamu umebainisha mfumo wa utawala uliowekwa na Mola wa walimwengu wote, na ni mfumo wa Khilafah ambapo Khalifa huteuliwa kupitia utiifu kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu na Sunnah za Mtume Wake kuhukumu kwa yale yote yaliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu.
[فَاحْكُمْ بَيْنَهُمْ بِمَا أَنْزَلَ اللَّهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ عَمَّا جَاءَكَ مِنَ الْحَقِّ]
“Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia.” [Al-Maida 3:48] Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:
«مَنْ خَلَعَ يَداً مِنْ طَاعَةٍ لَقِيَ اللَّهَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا حُجَّةَ لَهُ، وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً» “Yeyote mwenye kuondoa mkono wake katika utiifu atakutana na Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama akiwa hana hoja kwake, na yeyote anayekufa na hana ahadi ya utiifu (Bay'ah) shingoni mwake amekufa kifo cha kijahiliya” [Imepokewa na Muslim].
Mtume (saw) alibainisha kuwa jambo baada yake liwe ni Khilafah, Muslim amepokea kutoka kwa Abu Hazim, amesema: Nilikaa kwa Abu Hurayrah (ra) miaka mitano, na nikamsikia akisimulia kutoka kwa Mtume (saw):
«كَانَتْ بَنُو إِسْرَائِيلَ تَسُوسُهُمُ الْأَنْبِيَاءُ، كُلَّمَا هَلَكَ نَبِيٌّ خَلَفَهُ نَبِيٌّ، وَإِنَّهُ لَا نَبِيَّ بَعْدِي، وَسَتَكُونُ خُلَفَاءُ فَتَكْثُرُ»، قَالُوا: فَمَا تَأْمُرُنَا؟ قَالَ: «فُوا بِبَيْعَةِ الْأَوَّلِ، فَالْأَوَّلِ، وَأَعْطُوهُمْ حَقَّهُمْ، فَإِنَّ اللهَ سَائِلُهُمْ عَمَّا اسْتَرْعَاهُمْ»
“Banu Isra'il walikuwa siasa zao zikiendeshwa na mitume, kila mtume mmoja akifa, akirithiwa na mtume mwengine; na hakika yake hakuna mtume mwengine baada yangu, na kutakuweko na makhalifa wengi. Maswahabu wakauliza: 'Je, watuamrisha nini? Mtume akasema: Mpeni ahadi ya utiifu (Bay'ah) mmoja baada ya mmoja, na muwape haki yao, kwani Mwenyezi Mungu atawauliza juu raia aliowapa usimamizi kwao.”
Ama Ijmaa ya Maswahaba, wao, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, walikubaliana kwa kauli moja juu ya ulazima wa kusimamisha Khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) baada ya kufa kwake, na kwa pamoja wakaafikiana juu ya kumpa ukhalifa Abu Bakr, kisha Omar, na kisha Uthman baada ya kifo cha kila mmoja wao. Uthibitisho wa ijmaa ya Maswahaba ya kusimamisha Khalifa ulionekana kutokana na kuchelewa kwao kumzika Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) baada ya kifo chake, na kushughulika kwao kumteua mrithi kwa mikesha miwili hadi ilipoteuliwa Khalifa, ambayo inathibitisha kwamba uteuzi wa Khalifa ni wajibu zaidi kuliko kuzika wafu. Ijmaa hii ilikuwa ni ushahidi wa wazi na wenye nguvu wa ufaradhi wa kumteua Khalifa.
Tatu: Ama maneno aliyoyaandika mwandishi ambayo hayafai kwa Muislamu, bali yanaashiria kutoweza kwake kutoa hoja na dalili kwa ajili ya ukweli wa kauli yake, hivyo hatutayajibu kwa kufuata Hadithi ya Mtume (saw):
«لَيْسَ الْمُؤْمِنُ بِطَعَّانٍ وَلَا بِلَعَّانٍ وَلَا الْفَاحِشِ الْبَذِيءِ»“Muumini si mrongo, wala si mtu wa kulaani watu, na wala si mchafu mkosefu wa haya.”
Kwa kumalizia tunamwambia mwandishi kuwa wewe ni Muislamu, na asili ya Muislamu ni kujitahidi kwa ajili ya utukufu wa Uislamu na kuwainua Waislamu na kuhuisha kwao Uislamu na Waislamu. Na yakitokea makosa hapa au pale, tunayarekebisha kwa hekima na mawaidha mazuri, na tunajadiliana kwa njia iliyo bora zaidi, ili tusije tukamsaidia Shetani dhidi ya ndugu zetu, na tusiwe upande wa makafiri wanaopanga njama dhidi ya Uislamu na Waislamu.
[إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنْفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ لِيَصُدُّوا عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ فَسَيُنْفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ وَالَّذِينَ كَفَرُوا إِلَى جَهَنَّمَ يُحْشَرُونَ]
“Hakika wale walio kufuru hutoa mali yao ili kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watayatoa, kisha yatakuwa juu yao majuto, na kisha watashindwa. Na wale walio kufuru watakusanywa kwenye Jahannam.” [Al-Anfal 8:36]
Twamuomba Mwenyezi Mungu atuongoze kusema ukweli na kuwa na rai sahihi.
Wassalam Alaikum wa Rahmatullah
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: |