Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 17 Rabi' I 1443 | Na: HTS 1443 / 08 |
M. Jumapili, 24 Oktoba 2021 |
Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
[وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ بِشَيْءٍ مِنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِنَ الأمْوَالِ وَالأنْفُسِ وَالثَّمَرَاتِ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ * الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]
“Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri * Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.”[Al-Baqarah: 155-156]
(Imetafsiriwa)
Kwa nyoyo zinazonyenyekea kwa Qadhaa na Qadar ya Mwenyezi Mungu (swt), na kwa macho yanayobubujika machozi, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan inamuomboleza aliyesamehewa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt):
Sheikh Ibrahim Adam Muhammed Ahmed
Kutoka katika kizazi cha kwanza, ambaye alitumia ujana wake, na akajitolea maisha yake katika kufanya kazi ya kurudisha mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha dola ya Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume, akijitolea nafsi yake, wakati wake na mali yake kwa ajili ya Dawah. Misikiti inamjua kama msema kweli, asiyeogopa lawama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Daima alikuwepo katika shughuli na amali za Hizb licha ya uzee wake. Alikutana na watu kwa uso wa bashasha akifurahia fadhila za Mwenyezi Mungu na ushindi Wake aliouahidi, hadi Ajal isiyoepukika ilipomalizika na akafariki dunia mnamo siku ya Jumamosi, tarehe 16 Rabi’ Al-Awwal 1443 H sawia na 23/10/2021 M.
Twamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola Mlezi wa Arshi Tukufu ambariki kwa Rehema Zake Kubwa, amsamehe, ayakirimu mashukio yake, na aupanulie muingio wake. Na kuwabaraki jamaa zake na kizazi chake, na atutie ilhamu sisi, na ndugu zake wabebaji Dawah na familia yake na jamaa zake kwa subira na faraja njema. Hakika macho yanalia na nyoyo zinahuzunika, na sisi tunahuzunika kwa kukupoteza ewe ami yetu Ibrahim, lakini hatusemi ila yale yanayomridhisha Mola wetu Mlezi:
]إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعونَ]
“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqarah: 156].
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: |