Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  18 Sha'aban 1443 Na: HTS 1443 / 28
M.  Jumatatu, 21 Machi 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali Yaiba Haki yetu ya Mafuta na Kuongeza Bei ya Mafuta Kila Wiki!!
(Imetafsiriwa)

Ongezeko la bei ya mafuta liliendelea kwa mara ya nne mfululizo. Hapo jana serikali ilipandisha bei ya lita moja ya petroli hadi pauni 672 na kufanya bei ya galoni kufikia pauni 3044 na bei ya lita moja ya gasoline kufikia pauni 642 na kufanya bei ya galoni kufikia pauni 2889. Ongezeko hili la mfululizo lilianza tangu tarehe tano ya Februari iliyopita, wakati bei ya lita moja ya petroli ilikuwa pauni 362, na bei ya lita moja ya gasoline ilikuwa pauni 346; kwa maana nyengine, bei zilipanda chini ya mwezi mmoja hadi zaidi ya 100%!

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan tunathibitisha ukweli ufuatao:

Kwanza: Sudan, kama inavyotambuliwa na serikali yenyewe, inazalisha zaidi ya asilimia 58 ya petroli, na zaidi ya asilimia 40 ya gasoline. Halafu wanatuuzia kwa bei wanazoziita za kimataifa, na kwa bei ya dolari iliyoiponda pauni ya Sudan na kuifanya kuwa chini kabisa kwa sababu ya sera mbaya za serikali za Mfuko wa Fedha wa Kimataifa.

Pili: Mafuta ya petroli yanayozalishwa hapa nchini si mali ya serikali, bali ni mali ya umma, na ni aina ya tatu ya mali ambayo Shariah iliifanya kuwa umiliki wa umma wa Kiislamu, na ni madini yanayohesabika ambayo hayaishii, yaani, hayana kikomo kwa wingi na hayawezi kwisha mithili ya mafuta, na ushahidi kuwa mafuta hayo ni mali ya umma na haijuzu kumilikiwa na mtu binafsi, ni yale yaliyosimuliwa na Al-Tirmidhi kutoka kwa Abyad bin Hamal:

«أَنَّهُ وَفَدَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ ﷺ، فَاسْتَقْطَعَهُ الْمِلْحَ فَقَطَعَ لَهُ، فَلَمَّا أَنْ وَلَّى قَالَ رَجُلٌ مِنْ الْمَجْلِسِ: أَتَدْرِي مَا قَطَعْتَ لَهُ؟ إِنَّمَا    قَطَعْتَ لَهُ الْمَاءَ الْعِدَّ. قَالَ: فَانْتَزَعَهُ مِنْهُ»

"Kwamba alimwendea Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akamuomba amtengee hifadhi (timbo) ya chumvi. Akamtengea. Alipokuwa anaondoka, mtu mmoja aliyekuwa kikaoni akasema: Je, unajua kile ulichomtengea? Hakika umemtengea maji yasiyo malizika. Yeye (Shumair) akasema: akaiondoa kutoka kwake."

Kwa hivyo, haijuzu kwa dola kumiliki mafuta na madini ambayo hayakatiki kwa mtu binafsi au makampuni, na dhamira yake ni kuyachimba mafuta haya kwa manufaa ya wananchi na si kwa maslahi yake binafsi, wala kwa maslahi ya makampuni ya kibepari, kama ilivyo leo.

Hivyo basi, inaonekana kwamba serikali inatuibia haki yetu ya mafuta, na licha ya hayo, inaongeza bei yake kila wiki ili yenyewe na baadhi ya makampuni yafaidike kwa gharama yetu!

Tatu: Hata mafuta yanayoagizwa na makampuni, serikali inapandisha bei yake kwa ushuru unaozidi 25% ya bei ya mafuta na kwa kukiri kwake yenyewe, na hili limeharamishwa kwa sababu ni ushuru usio wa moja kwa moja unaoongeza bei. Na yeye (saw) ameharamisha kuwaongezea bei Waislamu, hivyo yeye (saw) akasema:

«مَنْ دَخَلَ فِي شَيْءٍ مِنْ أَسْعَارِ الْمُسْلِمِينَ لِيُغْلِيَهُ عَلَيْهِمْ فَإِنَّ حَقّاً عَلَى اللَّهِ تَبَارَكَ وَتَعَالَى أَنْ يُقْعِدَهُ بِعُظْمٍ مِنْ النَّارِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ»

Yeyote anayetia kitu katika bei za Wailsmau ili awaongezee, basi ni haki kwa Mwenyezi Mungu (swt) amkalishe katika Moto Siku ya Kiyama.”

Nne: Kupanda kwa bei ya mafuta (petroli na gasoline) moja kwa moja husababisha bei zote za bidhaa na huduma kupanda, na hili ndilo linalotokea siku hizi la kupanda vibaya kwa bei, na kuporomoka mfululizo kwa thamani ya pauni ya Sudan, ambayo amefanya maisha kuwa hali isiyoweza kuvumilika.

Kwa kutamatisha, tunawaambia watu wetu nchini Sudan, kwamba kilichotufikisha katika hali hii ya gharama kubwa ya maisha na ugumu wa maisha ni kuwa mbali mwelekeo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutabanniwa kwa mbinu za Makafiri katika siasa, uchumi, na mambo mengine, na maisha yetu hayatakuwa ya raha isipokuwa tutakaporegea kwa Mola wetu, na tufanye kazi pamoja na watoto wenye ikhlasi wa Ummah huu kusimamisha haki na uadilifu wa serikali; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume ambayo huyafunga maisha kwenye kamba madhubuti ya Mwenyezi Mungu (swt), na kuregesha, hukmu za Mola wa walimwengu, haki yetu iliyoibiwa.

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.[Al-Anfal: 24]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu