Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  6 Dhu al-Qi'dah 1443 Na: 03 / 1443
M.  Jumapili, 05 Juni 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tangu Lini Kafiri Magharibi Huaminiwa kwa Haki za Binadamu
(Imetafsiriwa)

Makamu wa Rais wa Baraza Huru la Utawala, Mohamed Hamdan Dagalo (Hemedti), alithibitisha dhamira yao ya kushirikiana na mifumo yote ya Umoja wa Mataifa na Baraza la Haki za Binadamu, kukuuza na kuendeleza haki za binadamu nchini. Hemedti alionyesha nia yao ya kufuatilia utabikishaji wa mapendekezo yote yanayohusiana na kukuuza hali ya haki za binadamu nchini. (Saudi News Agency 04/06/2022).

Sisi katika Kitengo cha Wanawake cha Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan tunaonyesha ukweli ufuatao:

Kwanza: Wazo la haki za binadamu ni wazo kamili la Kimagharibi, kwani Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitabanni Mkataba wa Umoja wa Mataifa na Tangazo la Kiulimwengu la Haki za Kibinadamu, ambayo wanayachukulia kuwa ndio msingi wa kile kinachojulikana kama haki za binadamu. Tangu wakati huo, Umoja wa Mataifa umepanua sheria ya haki za binadamu ili kujumuisha viwango maalum kwa wanawake, watoto na walemavu, makabila madogo madogo na makundi yaliyo hatarini. Kwa hivyo, haki za binadamu ni vigezo maalum kwa mujibu wa mtazamo wa kirasilimali wa Kimagharibi na itikadi yake ya kutenganisha dini na maisha, na ni kielelezo cha mtazamo wa mabepari juu ya mtu binafsi na mujtamaa na umewekwa kwa wanawake na watoto. Ama makundi mengine yaliyosalia, umeyataja kuwa ni kurusha majivu machoni. Nchi za Magharibi zimechagua haki za binadamu kama kauli mbiu ya kumetameta inayobeba uchawi wake katikati ya wanawake wengi wasio na ufahamu, kutokana na dhulma na ukandamizaji unaofanywa juu yao kwa kukosekana kwa mifumo ya usawa ya Kiislamu. Nchi za Magharibi zimenyanyua kauli mbiu ya “kuwalinda wanawake na watoto na kulinda uhuru” lakini kwa njia yao wenyewe na kwa mujibu wa mtazamo wao wa maisha, unaogongana na mfumo unaokubaliwa na Uislamu; dini ya watu wa Sudan.

Pili: Kinachothibitisha urongo wa haki hizi za binadamu, ni mara ngapi shirika hili linalodai kutetea haki za binadamu limekusanyika na kuamua na kutangaza bure bilashi kuyeyusha masuala muhimu ambapo binadamu hususan Waislamu wanauawa kinyama, kama yalitokea katika mauaji ya Jeshi, na katika nchi mbalimbali za Waislamu, damu ilimwagwa na mamia ya maelfu kujeruhiwa na kufungwa na mamilioni ya watu kukimbia makaazi yao na kuwa wahamiaji, ambapo linapiga domo tupu kwa haki za binadamu, bila ya Magharibi kunyosha kidole, na hili halishangazi, kwa sababu wale wanaouawa na kuteseka ni Waislamu, na kwa sababu muuaji ni mtumishi wa Magharibi, mhifadhi wa maslahi yake na mpigaji vita dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na wale wanaotaka kuregesha na kuhukumu kwa sheria ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka.

Wanasiasa wanapiga domo tupu la udumishaji wa haki za binadamu, na wao ndio wanaozikanyaga haki za binadamu, zinazowaka moto wa urasilimali na ukandamizaji wake. Licha ya utajiri wa nchi hii, wengi wa watu wake, wale ambao hawakufa katika mizozo inayowashwa na Magharibi na wapambe wake, wanakufa kwa njaa na umaskini katika wakati ambapo mabepari na wanasiasa wateja wachache wanafurahia uwezo na mali ya nchi hii, yote kwa sababu ya dhulma ya mfumo wa kirasilimali na ulafi wa watu wake.

Tatu: Kwa yakini, haki za binadamu ni uongo mtupu, kauli mbiu ya kumetameta, na neno legelege linalotumiwa na wanasiasa wanaoshikana mikono yao na adui wa Umma, Magharibi mrasilimali, wakiwakaribisha wale wanaotumia haki za binadamu kama kisingizio cha kuingilia kati masuala ya nchi hii, kufuja mali na kuwafanya watumwa watu wake, neno linalopigiwa debe na vyombo vya habari potoshi na vilivyoingizwa siasa vinavyopotosha ukweli na kuufanya mtazamo wa wanawake kwa mujibu wa mtazamo wa Sharia ni shambulizi dhidi ya haki zao, kama pigo kwa nafasi ya mwanamke wa Kiislamu katika jamii, ili awe kama wanawake wachafu wa Magharibi kwa sababu ya uhuru.

Hatimaye, kuregesha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume kusikoepukika imekuwa ni jambo la dharura la kuuondolea ulimwengu maovu ya urasilimali, kuondoa dhulma, na kuregesha haki kwa watu wake. Hivyo dunia itajaa uadilifu baada ya kuwa imejaa dhulma.

Msemaji Rasmi wa Kike wa Kitengo cha Wanawake
katika Hizb ut Tahrir Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu