Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 29 Jumada I 1444 | Na: HTS 1444 / 19 |
M. Ijumaa, 23 Disemba 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hotuba ya Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan katika Kongamano la Omdurman Al Thawra Al Hara 42
"Khilafah Pekee ndio Dola ya Waislamu"
(Imetafsiriwa)
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliyemtuma Mtume wake kwa uongofu na Dini ya haki ili kuifanya ishinde Dini zote ijapokuwa washirikina watachukia, na rehma na amani zimshukie mjumbe huyo kama rehema kwa walimwengu wote, aliyesimamisha dola ya kwanza ya Uislamu, ukitabikisha hukmu za Mola Mlezi wa walimwengu wote, rehma na amani za Mola wangu Mlezi ziwe juu yake, na jamaa zake na maswahaba wake watukufu, waliounda jengo la Khilafah Rashida, kwa njia ya Utume, na wanaowafuata kwa wema mpaka Siku ya Kiyama.
Wahudhuriaji wa Heshima... Assalamu Alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu,
Mtume (saw) aliondoka kwenda kwa Rafiki wa Juu baada ya kumaliza kuunda dola tukufu inayojulikana na historia, kwa uadilifu na rehema, kisha akawabainishia watu kwamba jambo baada yake ni Khilafah Rashida kwa njia yake. Kwa hivyo, Khilafah ilijulikana na kushuhudiwa kwa zaidi ya karne kumi na tatu, ilihuisha umati na watu, na kuwainua kielimu, kitamaduni, kisayansi, na kijeshi, kisha maadui wa makafiri wakoloni wakaishambulia, wakisaidiwa na vibaraka kutoka ndani mpaka walipoipindua Dola ya Khilafah miaka 102 Hijria iliyopita. Nchi za Kiislamu zilisambaratika, na hukmu za Mola wa walimwengu mahali pake zikachukuliwa na hukmu za makafiri, kiasi kwamba watu wengi hawaoni madhara yoyote katika mifumo hii iliyotungwa na wanadamu iliyo kinyume na Uislamu, na ambayo inawazuia kutokana na mwamko wa kweli na maisha ya staha chini ya ridhaa ya Mwenyezi Mungu.
Ndugu Wapendwa, dola ya Uislamu ni Khilafah, na ndio uongozi mkuu kwa Waislamu duniani, unaotabikisha Uislamu nyumbani, na kuubeba kwa ujumbe wa uongofu na nuru kupitia da’wah na jihad kwa ulimwengu potofu. Khilafah ni faradhi, bali ni taji la faradhi, kwa kukosekana kwake, hukmu za Uislamu zimetoweka katika utawala, siasa, uchumi nk., na kwa kuwepo kwake, hukmu hizi na nyenginezo huwepo katika maisha ya watu.
Na nadharia ya kusimamisha Khilafah leo (kwa sababu haipo) imethibitishwa kuwa ni faradhi kwa kauli yake Mola Mtukufu:
(وَأَنِ احْكُمْ بَيْنَهُمْ بِمَا أَنْزَلَ اللَّهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَنْ يَفْتِنُوكَ عَنْ بَعْضِ مَا أَنْزَلَ اللَّهُ إِلَيْكَ فَإِنْ تَوَلَّوْا فَاعْلَمْ أَنَّمَا يُرِيدُ اللَّهُ أَنْ يُصِيبَهُمْ بِبَعْضِ ذُنُوبِهِمْ وَإِنَّ كَثِيراً مِنَ النَّاسِ لَفَاسِقُونَ)
“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka, basi jua kwamba hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwasibu kwa baadhi ya dhambi zao. Na hakika wengi wa watu ni wapotofu.” [Al-Ma’idah 5:49]. Bali, Mwenyezi Mungu amefanya kuhukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kuwa sawia na Imani. Yeye (swt) amesema:
(فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّى يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنْفُسِهِمْ حَرَجاً مِمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيماً)
“La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenyekee kabisa.” [An-Nisa 4:65].
Na kuhukumu kwa Uislamu kunaweza kuwepo tu ndani ya dola ya Uislamu pekee, ambayo Mtume (saw) ameifafanua kama Khilafah pindi aliposema (saw):
«كَانَتْ بَنُو إِسْرَائِيلَ تَسُوسُهُمْ الْأَنْبِيَاءُ كُلَّمَا هَلَكَ نَبِيٌّ خَلَفَهُ نَبِيٌّ وَإِنَّهُ لَا نَبِيَّ بَعْدِي وَسَتَكُونُ خُلَفَاءُ تَكْثُرُ قَالُوا فَمَا تَأْمُرُنَا قَالَ فُوا بِبَيْعَةِ الْأَوَّلِ فَالْأَوَّلِ وَأَعْطُوهُمْ حَقَّهُمْ فَإِنَّ اللَّهَ سَائِلُهُمْ عَمَّا اسْتَرْعَاهُمْ»
“Banu Israil siasa zao zilikuwa zikiendeshwa na Mitume. Kila mtume mmoja alipofariki, mwengine alimrithi; lakini baada yangu hakutakuwa na nabii na kutakuwepo na makhalifa na watakuwa wengi sana kwa idadi. Maswahaba zake wakasema: Unatuamrisha tufanye nini (tukifika kuwa na Khalifa zaidi ya mmoja)? Akasema: Mpeni bay’ah (ahadi ya utiifu) mmoja baada ya mwengine. Na muwape haki zao zinazostahiki (yaani watiini). Kwa hakika Mwenyezi Mungu (Mwenyewe) atawauliza juu ya wale aliowakabidhi.” Na yeye (saw) amesisitiza Khilafah kwa kusema:
«... فَإِنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ يَرَى بَعْدِي اخْتِلَافاً كَثِيراً فَعَلَيْكُمْ بِسُنَّتِي وَسُنَّةِ الْخُلَفَاءِ الرَّاشِدِينَ الْمَهْدِيِّينَ، وَعَضُّوا عَلَيْهَا بِالنَّوَاجِذِ وَإِيَّاكُمْ وَمُحْدَثَاتِ الْأُمُورِ فَإِنَّ كُلَّ مُحْدَثَةٍ بِدْعَةٌ وَإِنَّ كُلَّ بِدْعَةٍ ضَلَالَةٌ»
“Hakika mwenye kuishi muda mrefu ataona fitna kubwa miongoni mwenu, basi shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Khulafa ar-Rashidiyn (Makhalifa Waongofu), wale wanaoongoza kwenye njia iliyonyooka. Zikamateni kwa majego. Jihadharini na mambo mapya [katika dini], kwani hakika kila bid'ah (uzushi) ni upotofu.”
Mpito wa kidemokrasia ni uzushi na upotofu, utawala wa kijeshi ni uzushi na upotofu, serikali ya kiraia ni uzushi na upotofu, na jamhuri ni uzushi na upotofu. Na kila mfumo usiokuwa wa Khilafah ni uzushi na upotofu kwa sababu yote hayo hayatokani na Sunnah za Mtume (saw), wala katika Sunnah za Khulafa ar-Rashidun kwani ni wajibu kwetu sote kufanya kazi kwa bidii katika kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, vyenginevyo sisi ni wakosefu kama Mtume (saw) alivyosema:
«مَنْ خَلَعَ يَداً مِنْ طَاعَةٍ لَقِيَ اللَّهَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا حُجَّةَ لَهُ وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً»
“Mwenye kuondoa mkono katika utiifu atakutana na Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama bila ya hoja yoyote, na mwenye kufa bila ya kiapo cha utiifu shingoni mwake amekufa kifo cha kijahiliya.” Kifo cha Jahiliyah (kabla ya Uislamu) ni kifo cha dhambi, na dhambi haitaondolewa kwetu isipokuwa tufanye kazi kwa umakini na ikhlasi pamoja na wafanyi kazi ili kuregesha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.
Enyi Waheshimiwa, vipi tutaridhika kuongozwa na Makafiri wakoloni Wamarekani, Waingereza na wengineo? Je, tunawezaje kukubali kwamba watu hawa wapotofu watutungie katiba yetu kwa niaba yetu ambayo tunatawaliwa nayo? Je, tunawezaje kukubali kwamba watuweke ndani ya mfumo wao kwa msingi wa kutengwa kwa dini, na uanzishwaji wa maisha kwa kutenganisha dini na maisha?! Hali imepinduka miguu juu kichwa chini, hivyo badala ya sisi kuwa ndio tunaobeba kwao imani sahihi na mifumo ya haki, tunakubali kwamba watubebee imani yao potofu na mifumo mbovu!
Ndugu wapendwa, Umma wa Kiislamu, na nyinyi kama sehemu yake muhimu, huko nyuma hamkukubali ukafiri na hukmu zake, na sidhani kama mnakubali. Historia ya Umma wa Kiislamu ilikuwa ni historia ya utukufu na adhama, Umma wa ushindi mkubwa na ufunguzi, Ummah ambao viongozi wake walikuwa wakiwahutubia mabeberu na wafalme, wakisema: “Mwenyezi Mungu ametutuma kuwatoa watu kutoka katika ibada za watu wengine hadi kwenye ibada ya Mola wa watu, na kutoka katika dhulma za dini hadi kwenye uadilifu wa Uislamu, na kutoka kwenye ufinyo wa dunia hadi kwenye upana wa dunia na Akhera.” Basi, rudini kwenye maisha yenu ya awali.
Enyi Watu waheshimiwa, tumeahidiwa kuuongoza ulimwengu kwa kheri na uadilifu kama babu zetu walivyouongoza, na hapa tunaona kuanguka kwa hadhara ya Kimagharibi kifikra na kimaadili, mpaka kulingania matendo ya watu wa Lut, Mwenyezi Mungu akulindeni nao, zikawa ni haki zilizolazimishwa kwa dola na watu, kwani ni hadhara ya kimakosa na kuvunja familia, hadhara ambayo inakusanya pesa na kuwafukarisha watu.
Ama hadhara ya Kiislamu, ndiyo inayowanyanyua walimwengu, kwa sababu asili ilikuja kama rehma kwao. (وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِلْعَالَمِينَ) “Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.” [Al-Anbya 21:107]. Na ni hukmu za Mola Mlezi wa Walimwengu ambayo ilikuja pamoja na wahyi wa imani kwa Mtume mtukufu (saw).
Na huu sasa ndio wakati wa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) aliyesema,
(وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئاً وَمَنْ كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُولَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ)
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur 24:55].
Ni bishara njema ya Mtume (saw) aliyesema:
«تَكُونُ النُّبُوَّةُ فِيكُمْ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً عَاضّاً فَيَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ، ثُمَّ سَكَتَ»
“Utume utakuwepo kwenu muda wote apendao Mwenyezi Mungu kisha atauondoa anapotaka kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume. Itakuwepo muda apendao kuwepo kisha ataiondoa apendapo kuiondoa. Kisha utakuwepo utawala wa kurithishana (ufalme), utakuwepo muda apendao Mwenyezi Mungu kuwepo, kisha utauondoa apendapo kuuondoa. Kisha utakuwepo utawala wa kutenza nguvu, utakuwepo muda atapendao Mwenyezi Mungu uwepo kisha atauondoa apendapo kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume’. Kisha akanyamaza.”
Lakini inawahitajia wanaume na nyinyi mnaweza, Mwenyezi Mungu akipenda, basi Khilafah na isimamishwe mikononi mwetu, ili tuwe miongoni mwa washindi mbele ya Mwenyezi Mungu, kwani hatuna izza isipokuwa kwa kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu, na hatuna izza isipokuwa kwa Uislamu, na hatuna utukufu isipokuwa kwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, basi njooni, muwe waungaji mkono wake na wafanyi kazi kwa ajili yake.
Ndugu Wapendwa, Hizb ut Tahrir inakualikeni kufanya kazi nayo ili kuregesha maisha kamili ya Kiislamu, kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume kwani hakuna maisha ya Kiislamu isipokuwa ndani ya Khilafah. Hizb ut Tahrir imetayarisha rasimu ya katiba kwa ajili yake yenye vifungu 191, vinavyodhibiti nyanja zote za maisha. Katika utawala, uchumi, mfumo wa kijamii, sera ya elimu, sera ya kigeni nk., hadi maisha yarudi kuwa maisha ya Kiislamu yanayomridhisha Mola wetu Mlezi, na kututoa katika maisha duni.
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ)
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal 8:24]
Wassalamu Alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu,
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: |