Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  11 Jumada II 1444 Na: HTS 1444 / 21
M.  Jumatano, 04 Januari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Burhan, Unamlalamikia Nani Kuhusu Hatari ya Dawa za Kulevya kwa Vijana, na Wewe ndiye Mtawala na Mwenye Jukumu?!
(Imetafsiriwa)

Katika mkutano ulioongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala, Luteni Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan, mnamo Jumanne, tarehe 03/01/2023, kwenye Uongozi Mkuu wa Majeshi, mbele ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Jizouli Daffallah, waziri mkuu wa zamani na mkuu wa kampeni ya kitaifa ya kupambana na dawa za kulevya, pamoja na mawaziri wa mambo ya ndani, sheria, elimu ya juu na elimu ya umma, na gavana wa jimbo la Khartoum, pamoja na baadhi ya viongozi wa idara za usalama, Al-Burhan alivishutumu vyama kwa kuhamasisha dawa za kulevya baada ya kupata fedha chini ya pazia la kusaidia mpito, na kufichua kuwa baadhi ya mashirika ya kimataifa yametoa msaada wa kifedha kwa mashirika ya vijana kwa lengo la kusaidia mpito, lakini zikatumiwa kukuuza na kutumia dawa za kulevya miongoni mwa vijana.

Luteni Jenerali Al-Burhan anazungumza kana kwamba hahusiki na kasoro hii kubwa katika muundo wa serikali, ambayo sasa yeye ndiye rais na mtawala wake. Nani aliyeruhusu mashirika ya kimataifa na mengine kulipa pesa kwa hayo unayoyaita mashirika ya vijana?! Na serikali ilikuwa wapi na wewe ulikuwa wapi mtawala wa kwanza nchini wakati pesa hizi zikiingia? Baya zaidi ni kwamba sasa unakiri kuwa pesa hizo zilitumiwa kupigia debe na kutumia dawa za kulevya, hivi ulichukua hatua gani dhidi ya uovu huu mkubwa? Je, umewawajibisha waliofanya kitendo hiki? Na mtu yeyote katika nchi hii anayeteswa na watawala wake, wanyonge, anajua kwamba dawa za kulevya zimekuwa janga ambalo limeenea miongoni mwa vijana na dola na wewe ukiwa rais wake unafanya mikutano na kulalamika tu bila kufanya kile ambacho lazima ufanye kama mtawala. Mwenyezi Mungu atakuuliza juu yao Siku ya Kiyama!

Pindi Uislamu ulipokuwa na dola na Khilafah, Khalifa Mwongofu Omar bin al-Khattab, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, alisema: “Lau nyumbu angejikwaa katika njia ya Iraq, ningeogopa kwamba Mwenyezi Mungu ataniuliza mimi kwa nini hukumtengenezea njia, ewe Omar.” Ummah ulipotea siku ambayo Khilafah yake ilivunjwa, na suala hilo katika nchi za Kiislamu likachukuliwa na vibaraka wa Ruwayabidhah wa wakoloni makafiri wa Magharibi wanaotii amri zao, hata kama hilo litasababisha kuangamizwa kwa vijana na kuwapoteza vijana wa nchi hii. Khilafah itakayosimamishwa hivi karibuni haitaruhusu kuwepo kwa uhusiano wowote kati ya vyama, kambi, au watu binafsi wa Ummah, na baina ya mashirika ya kigeni au balozi. Ibara ya 182 ya Rasimu ya Katiba ya Dola ya Khilafah iliyotayarishwa na Hizb ut Tahrir inasema: “Ibara ya 182 – Haijuzu kwa mtu binafsi, chama, kambi au kikundi chochote kuwa na uhusiano na nchi yoyote ya kigeni hata kidogo. Uhusiano na dola umewekewa mipaka kwa dola pekee, kwa sababu peke yake ndiyo yenye haki ya kuchunga mambo ya Ummah kivitendo. Umma na makundi lazima waihisabu serikali juu ya uhusiano huu wa nje.”

Enyi watu wa Sudan: Imethibiti kivitendo kwamba watawala wenu ndio waliowapoteza vijana wenu, na wao ndio walioruhusu kuenea kwa madawa ya kulevya kisha wakaja wakilia kwa upotovu na bure, basi shirikianeni na wafanyikazi kuiondoa nchi hii na watu kutokana na hasara na udhalilifu kuregesha tena mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, kwani ndio njia pekee ya wokovu wenu kuzuia kupotea kwa vijana na matatizo ya maisha, na ndio mwokozi Siku ya Kiyama kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na sababu ya radhi za Mwenyezi Mungu na kuingia Pepo yake.

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ)

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal 8:24]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu