Alhamisi, 09 Rajab 1446 | 2025/01/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  19 Shawwal 1444 Na: HTS 1444 / 41
M.  Jumanne, 09 Mei 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kwa Kuregea kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, Tutamaliza Vita, Sio kupitia Mazungumzo Yanayofadhiliwa na Marekani, Adui wa Uislamu na Waislamu!
(Imetafsiriwa)

Baada ya wiki tatu za mauaji na uharibifu, Marekani inaamuru watu wake wafanye mazungumzo jijini Jeddah baada ya mamia kuuawa, maelfu kujeruhiwa, miundombinu kuharibiwa, maisha kuvurugika, watu kuhamishwa kutoka kwa makazi yao, kutangatanga, kuzingirwa na kifo, njaa na magonjwa. Marekani haikuingilia kati kukomesha vita isipokuwa kwa masaa machache tu ili kuwahamisha raia wake, wafanyikazi wa ubalozi wake na wafanyikazi wa balozi nyinginezo, na kuwaacha watu wakiuawa na kuhamishwa, kana kwamba watu wa Sudan hawastahili maisha kama ya wale waliohamishwa!

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan, na kwa kuzingatia uhalisia huu, tunathibitisha yafuatayo:

Kwanza: Mzozo baina ya Jeshi na Vikosi vya Msaada wa Haraka lazima uelekezwe kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume Wake (saw) na sio Marekani, adui wa Uislamu na Waislamu. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللّهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللّهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ ذَلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلاً]

“Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.” [An-Nisa 4:59], and He (swt) says: ﴿وَمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِن شَيْءٍ فَحُكْمُهُ إِلَى اللَّه“Na mkikhitalifiana katika jambo lolote, basi hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu.” [Ash-Shuraa 42:10].

Pili: Marekani, kinara wa ukafiri, hatutakii kheri yoyote na hii ndio dini ya makafiri, kama alivyosema (swt):

[مَّا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُواْ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَلاَ الْمُشْرِكِينَ أَن يُنَزَّلَ عَلَيْكُم مِّنْ خَيْرٍ مِّن رَّبِّكُمْ]

“Walio kufuru miongoni mwa watu wa Kitabu na washirikina hawapendi mteremshiwe kheri yoyote kutoka kwa Mola wenu Mlezi.” [Al-Baqarah 2:105]. Kwa hivyo tunawezaje kusubiri kheri kutoka kwa mazungumzo yaliyoamriwa na kufadhiliwa na Amerika?!

Tatu: Vita vinavyoendelea hivi leo kati ya jeshi na Vikosi vya Msaada wa Haraka, kama Al-Burhan alivyoeleza, ni vita vya kipuuzi, na ndivyo ilivyo. Washindwa pekee ndani yake ni Waislamu wa nchi hii, na mshindi pekee ndani yake ni Amerika, ambayo, kupitia vita hivi, inataka kuhifadhi ushawishi wake nchini Sudan, kupitia jeshi, na kuzuia muundo wa makubaliano unaokusudiwa kuhamisha nguvu halisi nchini Sudan kwa vibaraka wa Uingereza.

Ama Marekani na vibaraka wake katika eneo hili, hivi sasa wanatoa wito wa dharura wa kujumuishwa kwa kila mtu katika mchakato wa kisiasa baada ya kusimamisha vita, na hili ndilo ambalo Vikosi vya Uhuru na Mabadiliko vililikataa na kuliita "kufa maji" kwa hofu ya watu wa Marekani kuingia madarakani.

Nne: Vibaraka wote wa Marekani na Uingereza wote wana nia ya kukaa tu kwenye viti vinavyosimamiwa na mabwana, hata kama ni juu ya mafuvu na mizoga.

Kwa kumalizia, watu wa Sudan lazima wafahamu njama za Makafiri zinazopangwa kwa ajili yao, zinazofanywa na wale waliouza Dini yao kivitendo kwa vibaraka wengine wenye ngozi zetu, hivyo tunaungane na ndugu zetu ambao sera za vibaraka zilifanikiwa nchini Syria, Libya na Yemen na nyuma yao mabwana zao, ni lazima tukatae pande zote mbili; Vibaraka wa Marekani na Uingereza, na kufanya kazi ya kuwapindua wote, na kusimamisha jengo kuu la Uislamu, Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume, ili kuziokoa ardhi zetu kutokana na vibaraka, kuziimarisha na kuzilinda kutokana na vitimbi vya Makafiri.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُم]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal 8:24]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu