Jumatano, 08 Rajab 1446 | 2025/01/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  9 Sha'aban 1444 Na: HTS 1444 / 37
M.  Jumatano, 01 Machi 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan Wakutana na Jaji Mkuu na Wasaidizi wake

(Imetafsiriwa)

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan ukiongozwa na Ustaadh Nasir Ridha - Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan, akifuatana na Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil), Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, na Ustaadh Mwanasheria Ahmed Abkar - Mjumbe wa Baraza la Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, na Ustadh Mwanasheria Faqir Haj Muhammad Ahmed - Mwanachama wa Hizb ut Tahrir ulikutana na Jaji Mkuu, mbele ya Katibu Mkuu wa Masuala ya Majaji, na Mkurugenzi Mtendaji wa Afisi ya Jaji Mkuu, siku ya Jumanne, tarehe 8 Sha'ban 1444 AH sawia na 28/02/2023, ndani ya muundo wa kampeni ya hizb ya kupambana na mihadarati, ambayo ilizinduliwa na Shirika la Habari la Sudan (SUNA) mnamo Januari 22, 2023.

Baada ya mapokezi na kufahamiana, mkuu wa ujumbe huo, Ustadh Nasir Ridha, aliitambulisha Hizb ut Tahrir, na kwamba lengo lake ni kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume, na akaashiria kwamba ziara hii inakuja ndani ya kampeni ya Hizb ya kupambana na dawa za kulevya, ikionyesha hatua ambayo Hizb imefanya katika suala hili katika maeneo yote ya Sudan, na kwamba mkutano wetu na mahakama kama mamlaka ya juu zaidi ya mahakama nchini, ili kuonyesha ruwaza yetu katika suala la mihadarati, kwamba si biashara ya muda mfupi tu, bali ni moja ya vita vya kisasa, ambavyo viko chini wa vita vya kizazi cha tano, na kwamba ni lazima kupiganwa, na kwamba hukumu za mahakama lazima ziwe kuzuia na kukemea, na jinsi Magharibi kafiri yenyewe ilivyoanza kurekebisha sheria, hasa zile zinazohusiana na kunyongwa nchini Sudan, na kwamba mahakama ina jukumu muhimu katika vita hivi. Alihitimisha hotuba yake kwa kusema kwamba dola haifanyi inavyotakiwa, kwa sababu inatumikia ajenda ya Wakoloni wa Magharibi, na lazima kuwe na dola yenye misingi ya itikadi ya Uislamu mtukufu, Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, kukabiliana na vita hivi.

Kisha Jaji Mkuu akazungumza, akithamini dori ya Hizb, na kuashiria udhaifu wa dola, na kwamba wametoa maagizo kwa vyombo vyote vya mahakama katika majimbo, kuzingatia pakubwa kesi za mihadarati, na kuwateua majaji wanaohusika hasa na kesi hizi. Kwa kumalizia, alikabidhiwa baadhi ya machapisho ya Hizb.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu