Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 2 Rajab 1445 | Na: HTS 1445 / 18 |
M. Jumapili, 14 Januari 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir Wilayah Sudan Wakutana na Sheikh Haran kwenye Msikiti wake mjini Al Qadarif
(Imetafsiriwa)
Kama sehemu ya amali wakati wa mwezi mtukufu wa Rajab, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir Wilayah Sudan mjini Kassala ulimtembelea Sheikh Idris Haran, Imam na khatibu wa Msikiti wa Ibrahim Musa katika Soko Kuu la Al Qadarif. Ziara hiyo ilifanyika mnamo Jumamosi ya kwanza ya Rajab 1445 H, ikiongozwa na Ustadh Mohamed Al-Hassan Ahmed, Mjumbe wa Baraza la Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan. Ujumbe huo pia ulijumuisha Montasser Karar, Abdel Samad Al-Tayeb, na Nasr Al-Din Al-Hajj, wanachama wa Hizb ut Tahrir. Mwanzoni mwa mkutano, Ustadh Montasser Karar, Mratibu wa Kamati ya Mawasiliano ya Amali mjini Al Qadarif, alizungumza, akiutambulisha ujumbe huo na kuelezea madhumuni ya ziara hiyo.
Kisha, Mohamed Al-Hassan, kiongozi wa ujumbe huo, alizungumza juu ya mwezi wa Rajab, ambayo Dola ya Kiislamu, Khilafah, ilibomolewa. Kwa kupotea kwake, Ummah wa Kiislamu ulipata kipindi cha mporomoko na shida za vita vilivyochochewa na makafiri wakoloni wa Magharibi, na kuvuruga na kuusumbua Ummah huku Magharibi yenyewe ikiishi kwa usalama. Matunda machungu ya vita hivi yanaonekana hivi sasa nchini Sudan, Palestina, na nchi zengine za Kiislamu. Mohamed Al-Hassan alihitimisha kwa kusisitiza kwamba suluhisho msingi kwa masuala yanayowakabili Waislamu liko tu katika kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Alisisitiza kwamba kutafuta suluhisho kiraka la muda mfupi kamwe sio halali.
Halafu, Sheikh Haran akazungumza kwa uzuri, akielezea kukinaika kwake katika usimamishwaji Khilafah kama dhamana ya nusra kwa Waislamu. Mwisho wa mkutano, Sheikh Haran alialikwa kuhudhuria amali zilizoandaliwa na Hizb ut Tahrir wakati wa mwezi wa Rajab, zikitumika kama ukumbusho kwa Ummah wa janga la kuvunjwa kwa Khilafah, zikilenga kuliweka hai wazo la Khilafah katika akili za Waislamu.
Kabla ya ujumbe huo kuondoka msikitini, Sheikh Haran alionyesha shukran zake kwa ziara hiyo, akaipongeza Hizb ut Tahrir, na akawatakia mafanikio.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: |