Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  27 Shawwal 1445 Na: HTS 1445 / 36
M.  Jumatatu, 06 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Yakutana na Raisi wa Chuo cha Kiislamu cha Nadwa
(Imetafsiriwa)

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ukiongozwa na Ustadh Nasser Ridha, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan, na wanachama Ustadh Abdullah Hussein, Mratibu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano, na Ustadh Yaqoub Ibrahim, Daoud Abdullah, na Muhammad Mukhtar, wanachama wa Hizb ut Tahrir, walikutana na Dkt. Abdullah Suleiman Ismail, imam na khatibu, na mkuu wa Chuo cha Kiislamu cha Nadwa, afisini kwake Port Sudan, Jumapili, 26 Shawwal 1445 H, sawia na 05/05/2024.

Mkutano huo ulijadili hali ya kisiasa nchini, vita vinavyoendelea, na hali ya mvutano kati ya vipote vya watu wa Sudan, kutoka kwa mapigano ya kikabila, migogoro kwa msingi wake, na maafa ambayo imeleta juu ya nchi na watu, na kwamba njia ya kutoka humo inawezekana tu kwa msingi wa hukmu za Uislamu mtukufu na sheria yake. Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan iko katika mchakato wa kufanya kongamano la kujadili masuala ya nchi hii, yanayotoka ndani yake, na si kutoka nje ya nchi, yanayodhibitiwa na dola za kikoloni ambazo haziitakii mema nchi hii, bali zinalenga kuigawanya na kuipasua.

Kisha Dkt Abdullah Suleiman akazungumza na kusisitiza kwamba utatuzi wa matatizo yetu lazima uwe katika msingi wa Uislamu, na lazima kuwe na mawasiliano na vikosi mbalimbali vinavyopigania maslahi ya Uislamu, ambaye alisema: Tunawashukuru kwa ziara hii, na maendeleo yenu katika jambo hili, kuwaleta watu pamoja imara kwenye kamba ya Mwenyezi Mungu. Tuko pamoja nanyi katika jambo hili na tunashiriki nanyi kwalo.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msema Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

2024 05 06 Sudan OS 2 Pic

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu