Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  28 Muharram 1445 Na: HTS 1446 / 05
M.  Jumamosi, 03 Agosti 2024

Taarifa ya Habari
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Yaandaa Maandamano mjini Al-Qadarif Kutaka Kukomeshwa kwa Vita na Umwagaji damu ya Waislamu
(Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Ijumaa, Agosti 2, 2024, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan iliandaa maandamano katika mji wa Al-Qadarif baada swala ya Juma’a karibu na Jami’ Al-Atiq (Msikiti Mkongwe) katika Soko la Al-Qadarif. Maandamano hayo yalitaka kukomeshwa kwa vita na umwagaji damu ya Waislamu, na kuuangaza Ummah kuhusu uhalisia wa njama za Magharibi zinazoongozwa na Marekani na Ulaya za kutaka kudhibiti mamlaka yao. Maandamano hayo yaliwataka wenye ikhlasi kushikamana na maamrisho ya Mwenyezi Mungu badala ya matakwa ya Kafiri Magharibi.

Mashababu walibeba mabango yenye maandishi yanayosomeka:

1. Hizb ut Tahrir inatoa wito wa kukomesha vita na uwajibikaji kwa wale wanaokula njama dhidi ya watu wetu nchini Sudan.

2. “Iwapo Waislamu wawili watakutana na panga zao, muuaji na aliyeuawa wote wamo Motoni.”

3. Komesheni uingiliaji wa Marekani katika ardhi za Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

4. Khilafah inalinda ardhi na kulinda heshima; isimamisheni enyi Waislamu.

5. Komesheni vita kwa kumtii Rahman, sio matakwa ya Wamarekani.

6. Maadui wa Uislamu wasingechochea vita kati ya Waislamu lau kama Waislamu wangekuwa na Khalifa.

7. Kuangamia kwa Al-Kaaba jiwe kwa jiwe ni sahali kwa Mwenyezi Mungu kuliko tone la damu ya Muislamu.

8. Lau sio kwa ushirika wa watawala, damu tukufu isingemwagika; kwa Khilafah, damu ya Waislamu inalindwa.

9. Vita vya Sudan ni vita vya kung’ang’ania madaraka kati ya Marekani na Ulaya, na wahanga ni watu wa Sudan.

Watu wetu katika mji wa Al-Qadarif waliingiliana na maandamano hayo na wakasifu juhudi za Mashababu wa Hizb, wakiomba ushindi na uthabiti wa Hizb.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu