Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  7 Safar 1446 Na: HTS 1446 / 06
M.  Jumatatu, 12 Agosti 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Marekani Yarefusha Vita ili Kufikia Ajenda yake, Kuteketeza Watu, Miti, na Mawe - Hakuna Njia ya Kutoweka Isipokuwa Kupitia Khilafah!

 (Imetafsiriwa)

Mnamo Jumapili, Agosti 11, 2024, mikutano ya Jeddah ilikamilika kati ya wajumbe kutoka serikali ya Sudan na Mjumbe Maalum wa Marekani nchini Sudan, Tom Periello, bila kufikia maelewano yoyote kuhusu ajenda ya mazungumzo na waangalizi. Baada ya kuregea kwa wajumbe wa mazungumzo, serikali ilitoa taarifa ikibainisha kushindwa kwa ujumbe wa Marekani kuwasukuma wanamgambo wa waasi kujitolea kutekeleza Azimio la Jeddah, ambalo linajumuisha dhamira ya kulinda raia nchini Sudan. Taarifa hiyo iliongeza, “Ujumbe wa Marekani haukutoa uhalali wowote wa kuunda jukwaa jipya,” na ulitegemea taarifa zisizo sahihi katika kutathmini hali nchini Sudan.

Serikali ya Sudan, inayoongozwa na jeshi, inafahamu kikamilifu kwamba chanzo cha mateso ya nchi hiyo ni dola hii ya kikoloni iliyo na chuki kubwa dhidi ya Uislamu na Waislamu; Marekani, ambayo imewaadhibu watu wa Sudan kwa zaidi ya miaka kumi chini ya serikali iliyopita, kisha ikagawanya kusini na kuandaa maeneo mengine ya Sudan kujitenga kupitia Mkataba wa Naivasha, na kudhibiti kuporomoka kwa Sudan baada ya vuguvugu la mapinduzi dhidi ya utawala wa Wokovu. Marekani ilifanya kazi kuunda migogoro kati ya wanajeshi na raia, na kusababisha ombwe hili la kisiasa na uharibifu wa kiuchumi. Serikali ya Sudan inayajua yote haya, lakini badala ya kukata kamba za wakoloni, kujinasua kutoka kwa mkoloni kafiri, na kuikomboa nchi kutoka katika minyororo yao, viongozi wa kijeshi wanaendelea kufuata amri za Marekani, kutekeleza ajenda yake na kuhifadhi maslahi yake!

Watawala, wawe wa kijeshi au wa kiraia, na wajue kwamba utawala katika Uislamu ni jukumu na usimamizi wa mambo kwa mujibu wa hukmu za Uislamu. Ni wajibu wa watawala kutatua matatizo ya watu na kusimamia mambo yao kwa mujibu wa Uislamu. Kuendelea kwa vita hivyo ni adhabu kwa wananchi, kuwadhalilisha na kuleta maafa nchini, kuwapa uwezo makafiri kutengeneza njaa na umaskini wa makusudi.

Ingawa viongozi wa jeshi na Vikosi vya Msaada wa Haraka wana uwezo wa kusitisha vita na kuweka usalama, hawafanyi hivyo isipokuwa kwa maelekezo kutoka kwa Marekani, ambayo inashikilia kamba za mchezo wa kisiasa nchini Sudan. Viongozi hawa wajihadhari na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, kwani Yeye (swt) atawahisabu kwa umwagaji damu usio na hatia, uvunjifu wa heshima, na wizi wa mali. Watubu kwa Mwenyezi Mungu na watimize wajibu wao katika kusimamia mambo ya watu, kwa kuanzia na kusitisha vita hivi vya kikatili na kisha kuwapa nusra wale wanaofanya kazi ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Muslim amepokea kutoka kwa Mama wa Waumini, Aisha (ra), kwamba Mtume (saw) amesema:

«اللَّهُمَّ مَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئاً فَشَقَّ عَلَيْهِمْ فَاشْقُقْ عَلَيْهِ، وَمَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئاً فَرَفَقَ بِهِمْ فَارْفُقْ بِهِ»

“Ewe Mola mfanyie dhiki yule ambaye amepewa mamlaka juu ya Umma wangu kisha akawatia taabu, na uwe mpole kwa yule ambaye amepewa mamlaka juu ya Umma wangu na akawa mpole kwao.”

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu