Jumatatu, 27 Rajab 1446 | 2025/01/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  19 Safar 1446 Na: HTS 1446 / 07
M.  Jumamosi, 24 Agosti 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mlima Geneva Umefanya Kazi Na Kuzaa Panya Aliyekufa!!
(Imetafsiriwa)

Jana, Ijumaa, Agosti 23, 2024, mkutano wa Geneva, ulioanza Agosti 14 kujadili mgogoro wa Sudan, ulihitimishwa kwa kuunda “Muungano wa Umoja wa Kimataifa” ili kumaliza vita nchini Sudan. Kwa mujibu wa Mjumbe Maalum wa Marekani nchini Sudan, Tom Prillo, muungano huo unajumuisha, pamoja na Marekani, Umoja wa Mataifa, Muungano wa Afrika, IGAD, pamoja na Uswizi, Saudi Arabia, UAE na Misri. Hata hivyo, pamoja na urefu wa majadiliano ya Geneva, matokeo hayana thamani ya halisi katika kusimamisha vita vya kikatili vinavyoendelea nchini Sudan.

Katika muktadha huo huo, shirika la habari la Agence France-Presse iliripoti kwamba jeshi na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vilikubali kutoa njia mbili salama kwa ajili ya misaada ya kibinadamu. Nchi zinazopatanisha pia zilithibitisha kwamba zilipata dhamana kutoka pande zote mbili za mzozo ili kuhakikisha usalama wa njia hizo, ambazo ni kivuko cha Adré katika eneo la Darfur na barabara ya Dabba kaskazini mwa Sudan.

Marekani haiko makini katika kumaliza vita kabla ya kufikia ajenda zake nchini Sudan. Kwa hivyo, inataka kuongeza muda wa vita ili kuweka mzozo kati ya pande zake mbili, uongozi wa kijeshi na uongozi wa RSF, na hivyo kudhibiti matokeo ya mzozo, kama ilivyo sasa. Kwa hivyo, upinzani tiifu kwa Uingereza na Ulaya bado umepooza, kama ilivyo tangu mzozo huo kuzuka. Zaidi ya hayo, Marekani inalenga kuondoa vuguvugu la waasi, au wanaoitwa vuguvugu la mapambano ya silaha zenye uhusiano na Uingereza. Kwa hivyo, kuporomoka kwa El Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini na kitovu cha serikali ya kikanda inayoongozwa na Minawi, ilikuwa ni jambo lisiloepukika. Hii inalazimu kukamatwa kwake na RSF ili Darfur yote iwe chini ya udhibiti wa RSF, na kusababisha uharibifu wa vuguvugu zilizounganishwa na Uingereza ambazo sasa zinaitetea vikali El Fasher, ikijua kwamba kuanguka kwake kunaonyesha mwisho wao. Marekani haitasimamisha vita hadi Darfur iwe mikononi mwa RSF, na kuiruhusu, iwapo maslahi ya Marekani yatataka baadaye, kutenganisha Darfur kupitia wateja wake wa RSF.

Imekuwa wazi tangu kutangazwa kwa jukwaa la Geneva kwamba Marekani haitaki kumaliza vita nchini Sudan. Hii imethibitishwa na taarifa ya mjumbe wa Umoja wa Mataifa, Ramtane Lamamra, wakati wa mkutano wa Baraza la Usalama mnamo Julai 29, 2024, kuhusu mkutano wa Geneva ambao Marekani iliuitisha mnamo Agosti 14, 2024, akielezea majadiliano ya Geneva kama hatua ya kwanza ya kutia moyo mchakato mrefu na ngumu zaidi. Kwa hili, alitangaza kwamba mkutano wa Geneva hautafikia suluhu bali ulikuwa gumzo tu kwenye kingo za Rhône jijini Geneva! Ukweli sasa unathibitisha kwamba Marekani haikukusudia Geneva kusuluhisha mzozo wa Sudan, na kwa hivyo mazungumzo ya Geneva yalimalizika na matokeo: Mlima Geneva umefanya kazi na kuzaa panya aliyekufa!

Watu wenye ikhlasi ndani ya jeshi na wananchi lazima wachukue hatua ili kuzuia njama za nchi za kikoloni, Marekani na Uingereza, katika ardhi yetu, wawaondoe vibaraka wasaliti, na wainusuru Hizb ut-Tahrir kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo itakata mikono ya makafiri wakoloni, kurudisha heshima ya Umma, nguvu, na ubora, na kuwa vile Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyokusudia kuwa: Umma bora ulioletwa kwa ajili ya wanadamu.

Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Surat Al-Anfal:24].

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu