Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  17 Rabi' II 1446 Na: HTS 1446 / 14
M.  Jumapili, 20 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Minawi Aidekeza Marekani na Kufumbia Macho Matendo ya Wale Wanaojitahidi Kusimamisha Khilafah, Kutangaza Uislamu Mtukufu!
(Imetafsiriwa)

Katika semina iliyofanyika katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, Arko Minawi, kiongozi wa Vuguvugu la Ukombozi wa Sudan na gavana wa jimbo la Darfur, alitoa kauli kadhaa, mashuhuri zaidi ni:

1. Alitoa wito wa kufanyia mageuzi taasisi ya kijeshi na kuunda jeshi la umoja.

2. Alidai kwamba wanaharakati wa Kiislamu nchini Sudan sasa wamegawanyika kimakabila na kieneo, na kwamba Uislamu wa kisiasa hauna uwepo halisi nchini humu.

3. Alisema hawatakubali kuvunjwa kwa serikali iliyoanzishwa mwaka 1956, kwa kuwa iliundwa kwa juhudi za mababu zao.

4. Alikariri shukurani zake kwa Amerika kwa kusimama na watu wa Sudan.

Kwa kujibu jumbe hizi, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ingependa kuangazia yafuatayo:

Kwanza: Kuunda taasisi moja ya kijeshi ni wajibu kwa Waislamu, misheni yake ikiwa ni jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kulinda mipaka. Uwepo wa majeshi tofauti, kama ilivyo leo, haukubaliki. Minawi mwenyewe anaongoza kikosi cha jeshi kilichojitenga na jeshi la serikali, lakini anazungumzia kuunda taasisi ya kijeshi yenye umoja! Jeshi hilo litafanyiwa mageuzi pale tu litakapokuwa jeshi la Kiislamu, sio la kitaifa, kama ilivyokusudiwa na wakoloni.

Pili: Madai kwamba Uislamu wa kisiasa haupo tena nchini yako mbali na ukweli. Uislamu wa Kisiasa, unaoregelea Uislamu unaozungumzia utawala na siasa na utekelezaji wa sheria za Mwenyezi Mungu duniani, ni matarajio ya Umma (jamii ya Kiislamu). Minawi na mabwana zake wa kikoloni wanajua kwamba Hizb ut Tahrir inafanya kazi pamoja na ndani ya Ummah kusimamisha utawala wa Mwenyezi Mungu kwa kusimamisha tena Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ahadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na bishara njema ya Mtume wake (saw). Hata hivyo, Minawi na walio nyuma yake wanataka kuficha ukweli huu, kama Mwenyezi Mungu alivyosema:

[يُرِيدُونَ أَن يُطْفِؤُواْ نُورَ اللهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللهُ إِلاَّ أَن يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ]

“Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia.” [Surat At-Tawba:32]

Tatu: Hiyo iitwalo “Dola ya 1956,” ambayo Minawi anadai iliundwa kwa juhudi za mababu, kwa hakika, ni dola iliyoundwa na mkoloni Muingereza na kukabidhiwa kwa vibaraka wake. Vibaraka hawa wamehifadhi mfumo wa Kiingereza wa kikafiri, unaotawala kwa katiba ya Bw. Stanley Baker. Wanaotaka kusambaratisha dola hii si wengine ila wakoloni wenyewe, kupitia vibaraka wao kutoka miongoni mwa watu wetu. Baada ya kujitenga kwa Sudan Kusini kwa kisingizio cha amani ya uongo, mkoloni anataka kuisambaratisha zaidi na kuigawanya Sudan katika vidola dhaifu ambavyo vinaendelea kutumikia kazi ya zamani na mpya ya kuhifadhi urithi wa mkoloni na kutimiza matakwa yake ya udhibiti, ushawishi na uporaji rasilimali.

Nne: Kutoa shukrani mpya kwa Amerika kwa kusimama na watu wa Sudan ni aina ya unafiki wa kisiasa. Amerika ndiyo iliyoanzisha vita nchini Sudan ili kusambaratisha Muundo wa Makubaliano na, kwa hayo, kuondoa ushawishi wa Uingereza, ambao unawakilishwa na raia na baadhi ya wale wanaoitwa harakati za mapambano ya silaha, ikiwa ni pamoja na harakati ya Minawi.

Kwa kumalizia: Mzozo unaoendelea nchini Sudan ni vita vya wakala kwa Amerika, ambayo haijali sana mauaji, kuhamishwa, na mateso ya watu wa Sudan, mradi tu lengo lake la kutokomeza ushawishi wa Uingereza nchini Sudan lifanikiwe, bila kujali gharama kubwa, inayolipwa na Wasudan kwa njia ya kuhamishwa makao, njaa, na magonjwa. Mgogoro huu utasitishwa pale tu watu wa Sudan watakapofahamu njama zinazosukwa dhidi yao, wakafanya kazi ya kubatilisha athari zake, na kuunganisha nguvu zao na watu wenye ikhlasi ili kusimamisha jengo kubwa la Uislamu, Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu