Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
| H. 24 Jumada I 1447 | Na: HTS 1447 / 55 |
| M. Jumamosi, 15 Novemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hotuba ya Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan katika Mkutano na Waandishi wa Habari yenye kichwa:
Makubaliano ya Nchi Nne (Quartet) ya Kusitisha Mapigano na Hatari ya Mazungumzo kwa Msingi wa Hadhara ya Kimagharibi
(Imetafsiriwa)
Tangu Quartet—ambayo inajumuisha sambamba na Amerika, Saudi Arabia na Misri na Imarati, ilipotangaza taarifa yake mnamo 12/9/2025 kuhusu mgogoro wa Sudan, watu wengi nchini Sudan wamegawanywa katika mikondo miwili: mkondo unaounga mkono taarifa ya Quartet inayotaka mazungumzo na suluhisho la kisiasa, kwa kisingizio kwamba inaleta amani, na mkondo mwengine unaosema unakataa kile kilichokuja katika taarifa ya Quartet, na kutaka kuendelea kwa vita. Na ijapokuwa pande zote mbili ni Waislamu, hawakuufanya Uislamu kuwa ndio msingi wa kutoka kwao katika kubainisha misimamo yao, wakati ilitakiwa hapo awali jambo hili litokee, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلاً]
“Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.” [Surat An-Nisa:59].
Na Asema Mwenyezi Mungu:
[وَمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِن شَيْءٍ فَحُكْمُهُ إِلَى اللَّهِ ذَٰلِكُمُ اللَّهُ رَبِّي عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ أُنِيبُ]
“Na mkikhitalifiana katika jambo lolote, basi hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Huyo Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi, ninaye mtegemea na kwake Yeye narejea.” [Surat Ash-Shura:10].
Na kuregesha kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ni kuregesha katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu na Sunna za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).
Kuregesha mzozo uliopo na vita vikali nchini Sudani kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume Wake (saw) kunapelekea kwe ukweli ufuatao:
Kwanza: Mwenye faili la vita vya Sudan ni Amerika, na ndiyo inayoongoza Quartet, na kuingizwa kwa baadhi ya dola za Kiarabu ni kutupa vumbi machoni tu, kwani Misri, Saudi Arabia, na Imarati hazimiliki chochote katika mambo yao; jambo hilo liko mikononi mwa Amerika kikamilifu, na ni dola kafiri ya kikoloni, na hairuhusiwi kuingia kati ya Waislamu, kwa sababu ni adui na sio rafiki. Ama kuhusu kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan, Muhyiddin Salim, kwamba Sudan inashughulika na ndugu zake nchini Misri na Sudani na marafiki nchini Marekani, ni kauli inayokanushwa! Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
[إِنَّ الْكَافِرِينَ كَانُوا لَكُمْ عَدُوّاً مُّبِيناً]
“Hakika makafiri ni maadui zenu walio wazi wazi.” [Surat An-Nisa:101].
Basi hakika wao, makafiri hawatutakiini kheri, kama alivyosema Mwenyezi Mungu:
[مَّا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَلَا الْمُشْرِكِينَ أَن يُنَزَّلَ عَلَيْكُم مِّنْ خَيْرٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَاللَّهُ يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَن يَشَاءُ وَاللَّهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ]
“Walio kufuru miongoni mwa watu wa Kitabu na washirikina hawapendi mteremshiwe kheri yoyote kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na Mwenyezi Mungu humkusudia kumpa rehema yake ampendaye. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kubwa.” [Surat Al-Baqarah:105].
Kwa hivyo yeyote asiyetutakia kheri kutoka kwa Mola wetu, kheri itatokaje kwake?! Hasa wakati kafiri ndiye mkuu wa ukafiri, Amerika ambayo mikono yake inatona damu ya Waislamu kote ulimwenguni.
Pili: Hadhara ya Kimagharibi, ambayo Amerika inaiongoza leo, imejengwa juu ya itikadi ya kutenganisha dini na maisha, na ni itikadi inayoegemea suluhisho la kati na kati, kwa hivyo hawana haki na batili; kwa hivyo, daima wanatafuta kutatua migogoro kupitia suluhisho la kati na kati, ikimaanisha maridhiano kati ya pande mbili zinazogombana, ambayo ni kwamba kila upande hufanya makubaliano hadi hizo mbili zikutane katika eneo la katikati, kwa sababu haki kwa mtazamo wao inanyumbuka, sio kamilifu. Kwa hivyo, mazungumzo haya ambayo Quartet inafadhili kwa msingi wa suluhisho la kati na kati yanalenga kuanzisha usawa kati ya serikali na yule iliyoasi dhidi yake, kisha kuchukua makubaliano kutoka kwa kila upande kwa manufaa ya mwengine, ambayo inapelekea kutenganisha Darfur! Kwa sababu mazungumzo yanatokana na suluhisho la kati na kati, sio suluhisho sahihi linalothibitisha haki na kubatilisha batili.
Tatu: Makafiri wakoloni, wanapotafuta kutatua migogoro katika ardhi za Waislamu—migogoro ambayo hapo awali walikuwa chanzo chake, au waliianzisha kupitia vibaraka wao, wanaitatua kwa msingi wa maslahi yao wenyewe na wanachotaka, si kile kilicho kwa maslahi ya watu wa nchi hiyo. Iwe makafiri wanaingilia kati moja kwa moja, au kwa njia ya vibaraka kupitia mashirika yao ya kikanda, Muungano wa Afrika au IGAD au wengine, kutenganishwa kwa Sudan Kusini nasi si mbali, chini ya visingizio vile vile vya uovu, vya kuleta amani na utulivu, waliitenganisha Sudan Kusini, na walikuwa na hamu ya kusambaza maambukizi hadi Darfur ili kuitenga, na vivyo hivyo wanatenda. Na kwa kusudi hili, kutenganishwa kwa Darfur na kugawanyika kwa Sudan, Amerika iliwasha vita hivi vya uharibifu, vilivyochochewa na matukufu ya Waislamu, ikichora kwa damu yao mipaka ya dola ya kikanda au kijamii au hata kikabila kwenye magofu ya Sudan, ambayo Amerika kwa uwongo inayaita marekebisho ya mipaka ya Sykes-Picot. Na Amerika imeshikilia faili hilo kwa miaka miwili na nusu, ikilinganisha kati ya serikali na yule aliyeasi dhidi yake, ikichemsha sahani yake kwenye moto mdogo, ikizunguka kutoka jukwaa moja hadi jengine, hadi Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vilipoimarisha udhibiti wao juu ya eneo lote la Darfur baada ya kuanguka kwa El-Fasher, hivyo Amerika ilizidisha kupitia Quartet wito wa makataba wa kusitisha vita iliyouita wa kibinadamu, kisha mazungumzo ambayo kwa kweli yanaongoza mwishowe kwenye kuitenganisha Darfur, kwa mandhari ile ile ya Kusini, kwa jina la kusimamisha vita na kuleta amani, Amerika inafikia lengo lake la kuichana Sudan kupitia mipaka ya damu.
Nne: Kuendelea kwa vita kwa kasi ya sasa tangu vilipoanza mwaka wa 2023 hakutaondoa Vikosi vya Msaada wa Haraka, bali kutapelekea mandhari ya Libya kwa uwepo wa serikali mbili, na matokeo katika hali zote mbili ni kutenganishwa kwa Darfur, ambalo ndilo Amerika inalotafuta kupitia vibaraka wake!
Huu ndio uhalisia, kwa hivyo suluhisho ni nini basi?
• Suluhisho linatafutwa na Waislamu pekee katika Wahyi Mtukufu, itikadi ya Uislamu, katika Kitabu na Sunnah na yale viliyoyaongoza.
• Suluhisho kubwa la Kiislamu kwa suala lolote halijengwi juu ya suluhisho la kati na kati na maridhiano kati ya pande mbili, bali linajengwa juu ya kuthibitisha haki na kubatilisha batili, kwa hivyo yule aliye na haki hulichukua kikamilifu, bila kulipunguza.
• Ukosefu wa uhalali ni msiba wa misiba, kwani kila mtu aliyebeba silaha na kumiliki nguvu anataka kuwa mtawala juu ya watu, hadi njia rahisi ya kuwa waziri au kuchukua madaraka ikawa ujasusi na mgeni, kubeba silaha, na kukiuka matukufu ya wasio na hatia, na hii hata ikawa desturi inayotambulika ambayo haipati pingamizi, na hata viongozi wa jamii, kutoka kwa wanafikra, wanahabari na wanasiasa, huweka huduma zao miguuni mwa vibaraka wanaofanya ujasusi pamoja na mgeni! Na ili kurekebisha hili, Uislamu unaamuru kanuni kwamba mamlaka ni milki ya Ummah, ambayo inalazimisha kurudisha mamlaka iliyonyakuliwa kutoka kwa Ummah, ili iweze kusimama imara kwa msingi wa itikadi ya Uislamu, kwa kusimamisha mfumo wa Khilafah.
• Tiba ya Uislamu inaamuru kwamba yeyote anayebeba silaha dhidi ya dola inayotabikisha Uislamu na kutoa madai ya dhuluma, dola inamwomba aweke silaha zake chini ili kusikiliza malalamiko yake; ikiwa atafanya hivyo, dola hukaa naye, husikiliza malalamiko yake, na kuyaondoa kwake; na ikiwa anakataa kuweka silaha zake chini, anapigwa vita vya kinidhamu hadi aweke silaha zake chini, na dola hairuhusu dola yoyote ya kigeni kuingia katika jambo hili, achilia mbali kumruhusu yule aliyechochea vita, adui kafiri, kudai upatanishi.
• Tiba ya Uislamu kuhusu suala la uasi na kwenda kinyume na mamlaka ya dola ni tiba ya Shari’ah ambayo inafikia utumwa kwa Mwenyezi Mungu, Mola wa Walimwengu, na zaidi ya hayo ndio tiba sahihi inayotekelezwa kwa uhalisia wa tatizo; Inalinda umoja wa dola na kuzuia kuingilia kati kwa maadui wanaojificha katika mambo yake, kwa hivyo hebu na tufuate mwongozo wa Wapendwa wetu (saw).
Enyi watu wa Sudan, Enyi wenye ikhlasi miongoni mwa watu wenye nguvu na ulinzi:
Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan inaendelea kufanya kazi miongoni mwenu na pamoja nanyi, kwa ajili ya kuhuisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu, na kuwafanya muone na kuvuta umakini wenu kwamba njia ya kutoka katika maisha haya mabaya yenu, ambayo yako katika ghadhabu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, inawakilishwa katika kuunda miongoni mwetu sote lengo moja, ambalo ndilo jinsi wanyoofu miongoni mwa wana wetu kutoka kwa watu wenye nguvu na ulinzi wanavyotoa msaada (nusrah) kwa Hizb ut Tahrir, kuhakikisha utabikishaji wa Uislamu, kuwakomboa watu kutoka kwa ukoloni, na kuubeba Uislamu kwa walimwengu wote. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُون]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Surat Al-Anfal:24].
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb Ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |



