Jumatano, 13 Rabi' al-awwal 1443 | 2021/10/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  23 Dhu al-Hijjah 1441 Na: 08 / 1441 H
M.  Alhamisi, 13 Agosti 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uzinduzi wa kampeni: "Hapana kwa Uhalifu wa Suluhisho la Kisiasa; Ndio Kuangushwa kwa Serikali na Kusimamishwa Khilafah!"

Hakika Wamagharibi makafiri chini ya uongozi wa Amerika wamedumu katika kupanga dhidi ya "mapinduzi" ya Ash-Sham na watu wake kwa muda wa miaka tisa iliyopita, na wametumia katika hilo mbinu na mitindo katika kuwaumiza watu wa Ash-Sham na kuwapeleka katika kichinjio kile kinacho itwa "Suluhisho la Kisiasa"; suluhisho hili linamakinisha ukoloni wa Wamagharibi makafiri kwa ardhi ya Ash-Sham kwa viwango vyake vyote; miongoni wake, kisiasa, kiuchumi na hata kithaqafa, katika upande wa kumbadilisha kibaraka mmoja kwa kibaraka mwengine katika hali iliyo bora zaidi, ikiwemo kuziangusha harakati zao na kuzalisha tena upya nidhamu ya kisekula inayo tenganisha Uislamu na maisha; na kujaalia kujitolea kote kwa watu wa Ash-Sham katika maisha haya kuwe kumepotea bure; bila ya kupatikana lile ambalo watu wa Ash-Sham walikuwa wanaliendea nalo ni kuiangusha serikali ya kihalifu kwa nguzo na alama zake zote na kusimamisha utawala wa Uislamu mahali pake.

Wamagharibi wanajua vyema kwamba nguvu ya Waislamu inaweza kuzalisha nidhamu mpya ya kisiasa ambayo Aqeedah ya Kiislamu ndio itakayokuwa msingi wake, na wanajua kwamba kusimama kwa Khilafah Rashidah kwa Njia ya Utume ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alibashiria kurudi kwake itakuwa ni hatari kubwa kwao; bali itaondoa ushawishi wao sio tu katika ardhi ya Ash-Sham pekee; bali katika nchi zote za Waislamu, na itawafuata kati ardhi yao huku ikibeba Uislamu kama Uongofu na Nuru kwa wanadamu wote. 

Na vipi Wamagharibi makafiri na zana zao wasiyapige vita "mapinduzi" ya Ash-Sham;  na ilhali wao ndio waliofanya kazi kwa bidii na kwa miongo kadhaa katika kuiangamiza Dola ya Khilafah ambayo iliwaunganisha Waislamu wote; na ilikuwa ndio ngome yenye kuukinga Uislamu na Waislamu?! Basi kwa hilo walikuwa waangalifu mno katika makongamano yao mingi yanayo husiana na Ash-Sham juu ya kuwepo dola ya kisekula na ya kizalendo ili kudhamini utenganishaji wa Uislamu na maisha na jamii; na kuzihifadhi serikali vibaraka na za kihalifu.

Na hakika walianzisha tume ya kuunda katiba ya kisekula na wakachagua wanachama wake; ili kudhamini utungaji katiba iliyo fafanuliwa vipimo vyake; inayo hifadhi maslahi yao na yenye kuhakikisha malengo yao na kumakinisha utiifu kwao, ni hili pekee ndilo linalo waridhisha, na kumkasirisha Mola wa Walimwengu na hakuna uhalifu wala uovu mkubwa zaidi ya huu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(وَلَنْ تَرْضَىٰ عَنْكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ  قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّهِ هُوَ الْهُدَىٰ  وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُمْ بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ  مَا لَكَ مِنَ اللَّهِ مِنْ وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ).

"Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu." [al-Baqara: 120]

Na kwa hayo yote; hakika sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Syria; tunatangaza kuanza kwa kampeni kwa anwani: "Hapana kwa Uhalifu wa Kisiasa; Ndio Kuangushwa kwa Serikali na Kusimamishwa Khilafah!" Tutajaribu katika kampeni hii kuonyesha uhalifu huu na athari zinazotokana nao na kuwatahadharisha watu wetu na ndugu zetu kutokana na kukubali suluhisho hili na kutumbukia ndani yake.

Na tunawaomba wote wenye ikhlasi miongoni mwa ndugu zetu na watu wetu, ili kujitolea kwa watu wa Ash-Sham kusipotee bure kwenye barabara za njama za kimataifa, kufanya kazi kwa bidii ili kuzuia kutokea kwa uhalifu huu wa kuchukiza; ambao utawarudisha upya watu wa Ash-Sham katika minyororo ya utumwa, maonevu, dhulma na ukandamizaji, na ikiwa Wamagharibi makafiri chini ya kiongozi wao Amerika wanabeba bendera ya vita dhidi ya Uislamu na Waislamu vipi basi yatakuwa matokeo ya masuluhisho yao wanayodai?!!! Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(مَا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَلَا الْمُشْرِكِينَ أَنْ يُنَزَّلَ عَلَيْكُمْ مِنْ خَيْرٍ مِنْ رَبِّكُمْ  وَاللَّهُ يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَنْ يَشَاءُ  وَاللَّهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ).

"Walio kufuru miongoni mwa watu wa Kitabu na washirikina hawapendi mteremshiwe kheri yoyote kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na Mwenyezi Mungu humkusudia kumpa rehema yake ampendaye. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kubwa" [al-Baqara: 105]

Basi tahadharini na adui wenu; na kataeni masuluhisho yake; na simameni upande wa Ummah wenu; na mtazameni Mwenyezi Mungu katika nafsi zenu kwa kheri; na mswadikisheni atakutimizieni ahadi yake na tamkini; na muamini kwamba hilo linakuja wala haliepukiki.  

Alama Ishara za Kampeni:

#لا_لجريمة_الحل_السياسي

#نعم_لإسقاط_النظام_وإقامة_الخلافة

Ahmad Abdul Wahhab

Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu