Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  20 Jumada I 1446 Na: 05 / 1446 H
M.  Ijumaa, 22 Novemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uvamizi Mpya wa Hay'at Tahrir al-Sham kwa Wanachama wa Hizb ut Tahrir: Hatua ya Kuelekea Uhalalisha Mahusiano au Kuelekea Kujisalimisha?!
(Imetafsiriwa)

Uvamizi mpya wa Huduma ya Kuu ya Usalama yenye uhusiano na Hay'at Tahrir al-Sham (HTS) kwa wanachama wa Hizb ut Tahrir ulikuja baada ya jina kupendekezwa kwa Ijumaa ya 22/11/2024: “Yeyote Anayelinda Mipaka ya NATO, Kuzuia Ufunguzi wa Vita na Kulinda Mipaka ya Utawala.” Huduma Kuu ya Usalama, baada ya uhamasishaji mkubwa iliyoufanya mnamo Ijumaa usiku, iliteka nyara idadi mpya ya wanachama wa Hizb ut Tahrir, ambao ni wakili Muhammad al-Sharif na Fateh al-Tarmanini kutoka mji wa Tarmanin, pamoja na mwanachama Omar Rahhal kutoka mji wa Kafr Nouran, na ndugu wawili, wanafunzi Bashar Abdul-Hay Samsoum na Ahmad Abdul-Hay Samsoum kutoka mji wa Atarib. Hapo awali, Sheikh Amir Salim, ambaye alihamishwa kutoka Jimbo la Daraa, alitekwa nyara.

Jina la Ijumaa hii lilikuja baada ya matamshi ya Ahmad Zidan ambapo alitaja kuwa Hay'at ilikuwa na dori kubwa katika kulinda mipaka ya NATO kwa kulinda mipaka ya Uturuki, mwanachama wa muungano huo, ambao ulisababisha hali ya chuki ya wananchi eneo hilo kwa wanamapinduzi, hasa Mujahidina.

Maneno ya Zidan ndani yao yalibeba kisu cha wazi kwa Mujahidina, ambacho ni kisingizio ambacho Hay'at imekuwa ikikitumia kuwadunga wale wanaopinga sera na fikra zake. Hivyo inadhihirika kutokana na maneno ya Zidan nani anawachoma kisu Mujahidina kwani Zidan katika kauli yake aliwaweka Mujahidina katika nafasi ya walinzi wa mipaka ya NATO na kuwafanya watekelezaji wa ajenda za nchi za Magharibi zinazo kula njama dhidi ya mapinduzi ya Ash-Sham, na anajua kwa yakini kwamba Mujahidina wa mapinduzi ya Ash-Sham hawakutoka ila kwa ajili ya jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu na kupindua utawala wa kihalifu jijini Damascus.

Enyi Watu wetu katika Mapinduzi ya Ash-Sham, Enyi Mujahidina: Mnaona kila siku, kwa macho yenu wenyewe, jinsi uongozi wa Hay'at na wananadharia wake wanavyowaona nyinyi. Hawakuchukuliini chochote isipokuwa zana wanazotumia kutekeleza ajenda walizopangiwa ili kukomesha jihad yenu, mapinduzi yenu na kujitolea kwenu. Kwa hiyo, mutafanya nini?!

Enyi Mujahidina: Uongozi wa Hay’at na wananadharia wake wanakuhujumuni na matendo yenu kwa ufidhuli, na wanafanya kazi ya kukuzuieni kuwazunguka wale wanaofanya kazi ya kukulindeni, jihad yenu, na mihanga yenu.

Leo, mapinduzi yanapita kwenye njia panda hatari. Ima mubakie kwenye njia ya uongozi wa Khay’at na viongozi wanaoshirikiana nao, na hivyo watekeleze kupitia nyinyi mipango na njama za nchi wanazozisuka wakati wa makongamano yao, au mumtegemee Mola wenu na mushikamane na kamba ya Mwenyezi Mungu peke yake, na mushikamane na misimamo ya mapinduzi yenu, na muendelee na uongofu na ufahamu pamoja na kiota chenu cha mapinduzi na watu wenu ambao wana shauku kwenu kufikia matunda ya jihad yenu kupindua utawala wa kihalifu nyumbani kwake, Damascus, na kusimamisha utawala wa Uislamu juu ya magofu yake.

Enyi Mujahidina: Jueni kwamba nyinyi ndio tumaini la watu wenu na kiota chenu. Hakika historia inarekodi misimamo, basi chagueni misimamo ya heshima kwa ajili yenu, watu wenu, kiota chenu, na Ummah wenu unaotamani kuwa nanyi mpaka Mwenyezi Mungu Atukirimu sote kwa ushindi na tamkini. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[يا أَيُّهَا الَّذينَ آمَنُوا استَجيبوا لِلَّهِ وَلِلرَّسولِ إِذا دَعاكُم لِما يُحييكُم وَاعلَموا أَنَّ اللهَ يَحولُ بَينَ المَرءِ وَقَلبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيهِ تُحشَرونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: +8821644446132 Skype: TahrirSyria
www.tahrir-syria.info
E-Mail: media@tahrir-syria.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu