Jumatatu, 27 Rajab 1446 | 2025/01/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  6 Jumada II 1446 Na: 07 / 1446 H
M.  Jumapili, 08 Disemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mumempindua Dhalimu wa ash-Sham, Basi Msikubali Chochote baada ya Dhalimu huyo Zaidi ya Utawala wa Uislamu na Dola yake, Khilafah
(Imetafsiriwa)

Allahu Akbar... Allahu Akbar... Allahu Akbar, la illaha illa Allah... Allahu Akbar, Allahu Akbar wal Hamdulillah. Allahu Akbar, viti vya enzi vya madhalimu na nguzo za wahalifu zimetikiswa.

Baada ya miaka kumi na nne ya mihanga mikubwa ya watu wa Syria katika mapinduzi yao yaliyobarikiwa, Damascus ilikuwa kwenye miadi ya ushindi alfajiri ya leo, Jumapili 8 Disemba 2024, kwa Idhini ya Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) alitubariki kwa kupinduliwa kwa dhalimu Assad, baada ya zama za dhulma, uhalifu na udhalimu wa familia ya Assad katika utawala wake wa chuki, wa kimadhehebu kwa muda wa miaka 54. Katika zama zao, walipiga vita Dini, Shariah na waja wa Mwenyezi Mungu (swt). Waliwatia watu kila aina ya mateso. Hakuna ushahidi bora zaidi wa hili kuliko idadi ya kutisha ya wafungwa ambao waliachiliwa huru kutoka kwa magereza yake ya dhulma, maovu. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[فَقُطِعَ دَابِرُ الْقَوْمِ الَّذِينَ ظَلَمُوا وَالْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ]

“Ikakatwa mizizi ya watu walio dhulumu - na wa kuhimidiwa ni Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.” [Surah Al-Anaam 6:45].

Kwani Mwenyezi Mungu (swt) ni Msifiwa yote na kutoka kwake ni Fadhila na Ruzuku zote.

Ndio, dhalimu wa ash-Sham, Farauni wa zama hizi, dikteta wa mhalifu, ameanguka. Alifikiri kwamba washirika wake, ambao Amerika iliwaleta kumlinda asianguke, wangezuia kuanguka kwake kwa kishindo. Hata hivyo, Mwenyezi Mungu (swt) aliwashughulisha na nafsi zao. Kwa hivyo alikutana na hatima yake isiyoepukika. Hivyo aliungana na wale waliomtangulia miongoni mwa watawala wa tawala za madhara, waliovunjika moyo, waliodhalilishwa, waliolaaniwa na kushindwa.

Kuanguka huku kukubwa kunajiri huku kukiwa na majaribio ya kidiplomasia ya baadhi ya washirika wake kutaka kumhifadhi. Kuna jiri baada ya mkutano wa Doha uliohudhuriwa na viongozi wa Mchakato wa Astana, Urusi, Uturuki, Iran, na wengineo, wakicheza na wakati uliopotea. Walisisitiza, “kusimamisha operesheni za kijeshi kwa maandalizi ya kuanzisha mchakato wa kisiasa.”

Tunawapongeza watu wa ash-Sham na wanamapinduzi wanyoofu na mujahidina kwa ushindi huu mkubwa. Tunathamini juhudi zao, kujitolea na historia wamelioiandika. Tunapofanya hivyo, tunawaonya juu ya njama kubwa inayopangwa dhidi yao ya kuvuruga kujitolea kwao, na kuturudisha alifu kwa kijiti. Hii ni kupitia juhudi za maadui zetu kufanya mabadiliko ya juu juu katika nyuso, huku wakidumisha utawala wa kisekula, iwe ni jamhuri ya kirais au bunge, almuradi isimamie dola ya kiraia, inayoutenga Uislamu na utawala na dola.

Enyi Waislamu wa Ash-Sham, Kitovu cha Makao ya Uislamu:

Hapana shaka kwamba kumuondoa dhalimu wa Syria kwenye eneo la tukio kunatufurahisha sote. Ni siku kuu ambayo Nguvu za Mwenyezi Mungu, Mkuu, Mwenye hekima zilidhihirika. Hata hivyo, misimamo muhimu zaidi ya mapinduzi yaliyobarikiwa ya Syria ni kupinduliwa kwa utawala wa kisekula wa jinai pamoja na nguzo na madhihirisho yake yote, katiba yake, wahalifu wake, na taasisi zake za kidhalimu, usalama na kijeshi. Serikali badali lazima iwe msingi wa imani yetu, na sio iliyoundwa na maadui zetu. Ni lazima tuendelee mpaka tutimize lengo letu, kwani hiyo ndiyo njia ya maisha, inshaAllah. Hii ni ili maafa ya baada ya mapinduzi ya Misri, Tunisia, Libya na Yemen yasirudiwe tena miongoni mwetu. Hakika, mapinduzi nusu ni hatari, na kutegemea tawala za sasa ni maangamivu.

Kama kilele cha kujitolea kwa mashahidi milioni mbili, na ili tusiwe “kama yule anayetengua uzi uliosokotwa, baada ya kusokota kwa nguvu,” tunamshukuru Mwenyezi Mungu (swt) kwa Neema, Fadhila na Nasr yake kwa kuendelea kufanya kazi ya kutabikisha Shariah Yake juu ya magofu ya mfumo wa kisekula uliofeli. Ni kupitia kufanya kazi ya kusimamisha utawala wa Uislamu, katiba yake, na dola yake, Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume. Ni kwa njia ya Khilafah Rashida pekee ndipo tunaweza kumridhisha Mola wetu, kulinda heshima yetu, na kukomboa matukufu yetu. Kusimamisha Khilafah Rashida ni faradhi, hakika ni taji la kupatikana kwa faradhi zote. Kwa kheri kubwa kama hii, hebu wale wanaofanya kazi na wafanye kazi.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atujaalie ushindi wa kweli na furaha kubwa siku ambayo utawala wa Uislamu utakaposimamishwa chini ya kivuli cha Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume, hivi karibuni, inshaAllah.

Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

[وَنُرِيدُ أَنْ نَمُنَّ عَلَى الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا فِي الْأَرْضِ وَنَجْعَلَهُمْ أَئِمَّةً وَنَجْعَلَهُمُ الْوَارِثِينَ * وَنُمَكِّنَ لَهُمْ فِي الْأَرْضِ وَنُرِيَ فِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَجُنُودَهُمَا مِنْهُمْ مَا كَانُوا يَحْذَرُونَ]

“Na tukataka kuwafadhili walio dhoofishwa katika nchi hiyo na kuwafanya wawe waongozi na kuwafanya ni warithi. * Na kuwapa nguvu katika nchi, na kutokana na wao kuwaonyesha kina Firauni na Hamana na majeshi yao mambo yale waliyo kuwa wakiyaogopa.” [Surah Al-Qasas 28:5-6].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: +8821644446132 Skype: TahrirSyria
www.tahrir-syria.info
E-Mail: media@tahrir-syria.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu