Jumanne, 13 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  21 Sha'aban 1444 Na: 1444 / 04
M.  Jumatatu, 13 Machi 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ushoga ni Agenda ya Wamagharibi, Matunda ya Mfumo Wake wa Kidemokrasia

(Imetafsiriwa)

Kufuatia kampeni inayo endelea dhidi ya ushoga na mapenzi ya jinsia moja nchini Tanzania inayofanywa katika mikoa mbalimbali na Waislamu ikiwemo Hizb ut Tahrir Tanzania, tungependa kubainisha  yafuatayo:

Kwanza, ni mfumo wa kidemokrasia ambao hutumika kama farasi kupitia dhana za ‘uhuru wa kibinafsi’ unaohubiri na kutetea ajenda ya Wasagaji, Mashoga, Wapenda jinsia mbili, Wanaobadili jinsia na Wanaochanganya jinsia (LGBTQ) na kila aina ya uovu, mfumo ambao ni hatari na tishio kwa ustawi wa ubinadamu, na kimsingi ni aina mpya ya dini ambayo inalazimishwa juu yetu kuacha nguvu zote za kidini, ili kuleta aina mpya ya uharibifu wa maadili. Hiyo ni dalili ya wazi inayoonesha kutofaa kwa mfumo wa kidemokrasia katika kuwahudumia wanadamu.

Kwa wafuasi wa demokrasia, wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu, badala ya kupokea na kuhubiri kila kitu kwa upofu, ni muhimu kuelewa kwamba mfumo wa kidemokrasia wa kisekula unaohubiri ‘uhuru wa kibinafsi’ haukuibuka kwa msingi wa hoja, lakini uliibuka juu msingi wa kupatiliza kijanja na kwa mtazamo wa kijuha baada ya mapambano makali baina ya wanamageuzi dhidi ya makasisi juu ya nafasi ya dini katika maisha. Kilichotokea ni kuja na suluhisho la muwafaka ya kati na kati (kuridhisha pande zote mbili) ambapo kila upande ulipata kitu, kwamba watu wa dini (makasisi) watabakia na dini yao katika maeneo ya ibada, ilhali wanamageuzi watakuwa ndio wenye haki ya maamuzi nje ya mahali pa ibada, kwa mujibu wa matakwa ya demokrasia.

Pili, vitendo vya ushoga vinakuzwa na mataifa ya Magharibi kwa kutegemea Tamko la Kimataifa la Haki za Kibinadamu. Kusema kwamba vifungu vya Haki za Binadamu ni kwa watu wote (universal) ni uwongo wa wazi. Mwenye haki pekee ya kutangaza jambo kwamba ni kwa watu wote ni Muumba wa ulimwengu na wanadamu pekee, na hakuna hata mmoja katika waliotayarisha tamko hilo amewahi kudai ubora huo, badala yake wale walioandika tamko hilo wamepita zamani (walikufa). Hiyo ni dalili ya wazi kwamba tamko hilo sio kwa watu wote (kiulimwengu), kwa sababu liliandikwa na wachache miongoni mwa viumbe na sio yule aliyeumba ulimwengu.

Tatu, ajenda ya LGBTQ inaonyesha kwa uwazi hali duni ya jinsi nchi zinazoendelea zilivyo, kukosa mamlaka halisi ya kujitawala licha ya kuwa na ‘uhuru wa bendera’. Maamuzi yote yawe ya kisiasa, kiuchumi, na hata kijamii kama ilivyo katika suala hili, ni kwa mujibu wa matakwa ya mamlaka ya wakoloni wa kibepari ambao hupuuza ubinadamu au maadili.

Nne, kampeni za kuunga mkono ushoga zinamdhalilisha na kumdhuru binadamu na ustawi wake, kwa kuwa kwa mchakato huu binadamu anatumiwa kama kifaa cha majaribio. Hapo awali, vitendo vya ushoga vilikuwa havikukubalika hata ndani ya nchi za kibepari za Ulaya, lakini baada ya kampeni kubwa sasa ni jambo linalokubalika. Asili ya mwanadamu hakuumbwa kama kifaa cha majaribio.  Hali ya kufanya majaribio katika asili ya binadamu ni dalili ya wazi ya kutofaa hizi zinazoitwa haki za binadamu, kwa kuwa asili ya mwanadamu haiwezi kubadilika. Jambo hili lina madhara na matokeo mabaya kwa ubinadamu.

Uislamu unamtazama mwanadamu kuwa kiumbe bora kilichotukuzwa kuliko viumbe vingine vyote, ambapo asili yake ya kimsingi haibadiliki, na kamwe si kifaa cha majaribio. Mwanadamu huyu kwa kuwa ni kiumbe ana udhaifu, ikiwa ni pamoja na mipaka ya ujuzi wake, kutetea maslahi yake binafsi na kuathiriwa na mazingira. Udhaifu huu unamnyima binadamu uwezo wa kutunga sheria (kwa usahihi). Ni Muumba pekee kwa Rehema zake ndiye ana uwezo wa kulibeba jukumu la kutunga sheria (kwa usahihi) za kumuongoza mwanadamu katika kila nyanja ya maisha yake.

(يُرِيدُ اللّهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمْ وَخُلِقَ الإِنسَانُ ضَعِيفًا)

“Mwenyezi Mungu anataka kukupunguzieni taabu, kwa kuwa mwanaadamu ameumbwa dhaifu”

[4:28]

Masoud Msellem

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania

 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu