Afisi ya Habari
Tanzania
H. 5 Rabi' II 1445 | Na: 1445 / 02 |
M. Ijumaa, 20 Oktoba 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mwito kwa Majeshi ya Ulimwengu wa Waislamu Kuinusuru Gaza
‘Harakisheni Majeshi Yenu Kuikomboa Gaza Na Al-Aqsa’
(Imetafsiriwa)
Leo Ijumaa 20 Oktoba 2023 Miladi / 05 Rabi’ al-Akhir 1445 Hijria baada ya Swala ya Ijumaa, Hizb ut Tahrir Tanzania ilifanya visimamo vya maandamano baridi (picketing) sehemu mbali mbali nchini kutoa mwito kwa majeshi ya nchi za Waislamu kuchangamsha majeshi yao kuikomboa Gaza, Palestina na Masjid Aqsa.
Mwito huo uliolengwa kwa majeshi ya nchi za Waislamu hususan Jeshi la Misri umeyataka majeshi hayo kuingilia kati kwa haraka sana kwenda kuikomboa Ardhi Tukufu ya Palestina, ardhi ya Israa na Miraj na kung’oa kijidola kiovu na najisi cha Mayahudi.
Mwito huo umeyakumbusha Majeshi ya nchi za Waislamu kwamba wao ni sehemu ya Ummah na ni wajukuu wa maswahaba wakubwa kama: Khalid ibn Walid, Abu Ubaidah, Ali ibn Abi Talib nk., bali pia wanatokana na vizazi vya mashujaa kama Salahudiin Ayoub, Muhammad Al-Fathi nk. Basi wanapaswa kuwa thabiti, kuamka na kuandama nyayo za wazee wao kuikomboa Palestina na kuchangamsha majeshi kukifuta kabisa kijidola cha Mayahudi haraka bila ya kusitasita.
Mwito huo ulibainisha wazi kwa Majeshi ya nchi za Waislamu kwamba ujumbe huo mtukufu wa Jihad ni mwito kutoka kwa Ummah mzima, kutoka kwa watoto, wanawake na wazee chini ya vifusi vya majengo yanayoporomoshwa kwa uadui na mabomu na kijidola cha Mayahudi, bali kubwa zaidi mwito huo ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu Taala, Muumba aliyewapa hao majeshi ujuzi wa kijeshi na nguvu ya kijeshi kuwa amana mikononi mwao, ili waulinde, waunusuru Ummah wao na kuzikomboa ardhi zao.
Mwito huo kwa Majeshi ya nchi za Waislamu uliangazia kwa kina kwamba maumivu ya Ummah wetu ni mazito, yamerefuka yasiokuwa na mfano yanayotendwa na kijidola duni, dhaifu, kioga cha Mayahudi, ambapo udhaifu wake umedhihirika mbele ya macho yao (wanajeshi). Hata hivyo, kijidola cha Mayahudi kinadiriki kutenda ukatili, unyama, mauaji na uadui kwa kulindwa na vibaraka katika ulimwengu wa Kiislamu, na kwa kuungwa mkono kikamilifu tena wazi wazi na dola za Makafiri za Magharibi ikiwemo Marekani, Uingereza na nchi nyingine za Ulaya nk. Hivyo, Majeshi ya nchi za Waislamu wana dhima na jukumu kutoka kwa Muumba kupeleka majeshi yao haraka kuukomboa Ummah wetu kutokana na maumivu, udhalilishaji, mateso, mauaji nk.
Kwa kumalizia, mwito huo uliyataka majeshi katika ulimwengu wa Kiislamu kujitenga mbali na watawala vibaraka wasioujali Ummah wetu, kwa kuwa viongozi hao ni wakala, walinzi na waungaji mkono wa kijidola cha Mayahudi kwa kisingizio cha ‘mchakato wa amani’ (peace process) na mchakato wa ‘uhalalishaji mahusiano’ (normalization). Na badala yake Majeshi katika ulimwengu wa Kiislamu yana jukumu la kutoa Nusra kwa Ummah ili kurejesha tena dola ya Kiislamu (Khilafah). Kwa dola hiyo, Uislamu, Waislamu, ardhi na matukufu yote yatalindwa ipasavyo.
Tunamumomba Mwenyezi Mungu Mtukufu Atie Tawfiq katika amali hizi na nyengine ulimwenguni kote. Kwake Tunategemea Nusra Yake ili kurejesha tena Khilafah ya Pili kwa Njia ya Utume. Amin
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania
- Click to open image! Click to open image!

https://hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari/tanzania/3525.html#sigProId9ce4477369
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tanzania |
Address & Website Tel: +255778 870609 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz |