Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  28 Dhu al-Hijjah 1440 Na: 1440 / 07
M.  Alhamisi, 29 Agosti 2019

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Maadhimisho ya Miaka 100 ya Jeshi la Polisi la Tanzania Hakuna cha Kujivunia

Jeshi la Polisi la Tanzania limetangaza sherehe ya maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwake.

Muda huu mrefu tangu kuanzishwa kwake sio kitu cha kujivunia kwa sababu ya rekodi mbaya ya taasisi hii, hususan katika miaka ya hivi karibuni.

Licha ya madai ya Polisi kuwa kazi yake ni kuhifadhi na kulinda maisha ya watu, mali na heshima kiuhalisia huu ni mwito mtupu ulio mbali na ukweli. Limenyanyasa wengi kwa jumla huku jamii ya Waislamu wakiwa ndio waathiriwa wakubwa zaidi. 

Kila uchao tunashuhudia madhila yasio kikomo kama vile wimbi la utekaji nyara, mauwaji, mateso kwa wahubiri na wanaharakati wa Kiislamu, wananchi wa kawaida, wanasiasa, watu mashuhuri, wafanyi biashara, wanahabari nk.

Pia kuna wimbi la kupotea kwa mamia ya waliotekwa nyara katika Wilaya za Kibiti na Mkuranga katika Maeneo ya Pwani ambao mpaka sasa taarifa zao hazijulikani. Bila ya kutaja kupatikana kwa miili ya watu waliokufa katika fukwe za Mto Ruvu na Bahari Hindi na uwepo wa magereza ya mateso chini ya Kitengo cha Polisi wa Kupambana na Ugaidi kikiwatesa Waislamu wanaoshukiwa kwa ugaidi na wafungwa wengineo, ambao vilio vyao vimepazwa mara nyingi.

Yote haya yanadhihirisha waziwazi sio tu utepetevu na kufeli kwa vyombo vya usalama hususan Jeshi la Polisi kuhifadhi na kulinda maisha ya watu, mali na heshima, bali kiburi kikubwa cha taasisi hii ambayo ipo kupitia pesa za walipa ushuru.

 (وَاسْتَكْبَرَ هُوَ وَجُنُودُهُ فِي الأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ إِلَيْنَا لاَ يُرْجَعُونَ)

“Na alipanda kiburi yeye na majeshi yake katika nchi bila ya haki, na wakadhania kuwa hawatarudishwa kwetu.”

(وَأَتْبَعْنَاهُمْ فِي هَذِهِ الدُّنْيَا لَعْنَةً وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ هُمْ مِنَ الْمَقْبُوحِينَ)

“Na tukawafuatishia laana katika dunia hii, na Siku ya Kiyama watakuwa miongoni mwa wanao chusha.”

Jeshi la Polisi na vyombo vinginevyo vya usalama kama jeshi na taasisi za ujasusi duniani chini ya mfumo wa kisekula wa kirasilimali huendeshwa kupitia ubaguzi wa rangi, ukatili, jeuri, ghasia na unyama pasi na kujali hata maadili yao wenyewe ambayo wanadai kuyaenzi, kwa sababu vinafanyia kazi nidhamu iliyotungwa na wanadamu isiyokuwa na thamani ya kiroho.

Kitu pekee cha kumaliza uchungu na kukomesha kiburi cha vyombo vya dola ikiwemo majeshi ya Polisi, ulimwengu unahitaji kuuondoa mfumo wa kirasilimali kupitia kuubadilisha kwa nidhamu pana na adilifu ya Uislamu chini ya Dola yake ya Khilafah.

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu