Jumamosi, 13 Sha'aban 1445 | 2024/02/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  22 Sha'aban 1440 Na: 1440/06
M.  Jumapili, 28 Aprili 2019

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Katika Urasilimali Vita Dhidi ya Ufisadi ni Mwito Mtupu

Ripoti ya hivi karibuni ya ukaguzi nchini Tanzania imefichua zaidi kwamba katika mfumo wa kirasilimali unaojifunga na kipimo cha maslahi, kadhia ya kupambana na ufisadi inasalia kuwa maneno matupu bila ya uhalisia wowote hata ingawa baadhi ya watu ndani ya nidhamu hii wanadai kuwa makini katika kupambana nao. Uhalisia ni kuwa huwezi kusafisha uchafu ikiwa wewe mwenyewe umo ndani yake.

Serikali ya sasa ya Tanzania inayojisifu kuwa mpiganaji wa ufisadi haionekani kwenda popote mithili ya serikali zilizo tangulia, au hata kuwa hali mbaya zaidi.

Ripoti hiyo mpya ya ukaguzi ya Mhasibu Mkuu wa serikali (CAG) ya mwaka 2017/2018 inafichua kuwa kuna ufujaji mkubwa sana wa serikali wa trilioni za shilingi kupitia mikataba na miamala isiyo eleweka kama vile uagizaji haramu na matumizi mabaya kupitia hazina ya nchi.

Ufichuzi huu unaonyesha kuwa kwa jumla, Tsh trilioni 1.3 (sawia na dolari milioni 562, "zilifujwa". Kati ya kiwango hiki, hazina inakabiliwa na maswali katika ukaguzi huo ya kiasi cha Tsh trilioni 885 (sawia na dolari milioni 382.7). Tsh. bilioni 432.7, sawia na dolari milioni 188, zilifujwa kupitia uagizaji bidhaa na huduma kutoka kwa taasisi tano ambao wasambazaji wake ima hawakuidhinishwa au hawakusajiliwa kihalali.    

Pia inapaswa kukumbukwa kuwa mnamo 2018, Kamati ya Uhasibu wa Umma (PAC) ya Bunge la Taifa, baada ya kuisoma ripoti ya CAG ya mwaka 2016/17, iligundua kuwa Tsh trilioni 1.5 (dolari milioni 640) "zilikosekana". Huku serikali ikikosa kuwa na maelezo yoyote ya maana. Pindi ukaguzi mpya ulipofanywa mnamo Februari 2019, dosari zaidi zilifichuka, huku kiwango cha fedha zilizo kosekana kikiongezeka hadi Tsh trilioni 2.4 (dolari bilioni 1.03).

Dhati ya wanasiasa wote wa kidemokrasia ni kuitumia serikali ili kujinufaisha kibinafsi kutokana na fedha za umma kwa jina la kuwatumikia watu. Kamwe hawajali kuhesabiwa na watu wala Mwenyezi Mungu, kwani kiuhalisia fikra yao ya kisekula haijali muongozo wa Mwenyezi Mungu.

Katika Uislamu siasa ni kuchunga mambo ya watu na ni amana kubwa sana ambayo mwanasiasa ni lazima afuatiliziwe na raia wa kawaida, taasisi imara ya Mahakama ya Madhalim na juu ya yote yeye atahesabiwa vikali Akhera. Hivyo basi katika Uislamu siasa sio biashara ya kujinufaisha bali ni jukumu linalo hitaji kubebwa kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu (swt).

Ni jambo la kimaumbile basi chini ya utawala wa Kiislamu wa Khilafah Rashidah kuwa uchafu wa ufisadi hautakuweko kama ulivyo leo katika nidhamu ya kirasilimali.

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu