Afisi ya Habari
Tanzania
| H. 30 Rajab 1447 | Na: 1447 / 05 |
| M. Jumatatu, 19 Januari 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Tanzania Yafanya Semina kwa Mnasaba wa Kumbukumbu ya Miaka 105 ya Kuvunjwa kwa Khilafah
(Imetafsiriwa)
Katika kumbukumbu ya miaka 105 ya kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah iliyotokea mnamo Rajab 1342 H / Machi 1924 M, jana, Jumapili, 29 Rajab 1447 H / 18 Januari 2026 m, Hizb ut Tahrir / Tanzania ilifanya semina fupi katika Masjid Taqwa, Ilala Bungoni katika jiji la Dar es Salaam.
Semina hiyo iliyoanza saa 3 asubuhi hadi saa 12 jioni iliwahusisha washiriki 80 hasa Maimamu, Maustadh, Masheikh na watu wengine mashuhuri kutoka maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam na viunga vyake.
Semina hiyo ilifunguliwa na Sheikh Mussa Kileo, Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir Tanzania, ambapo mada tatu ziliwasilishwa: Khilafah ni nini? Kuvunjwa kwa Khilafah, na Njia ya Kusimamisha tena Khilafah.
Washiriki walipata fursa ya kuuliza maswali, kutoa maoni na kushiriki katika majadiliano kuhusu mada hizo, na walipewa nakala za kila mada pamoja na nakala ya hotuba ya hivi karibuni ya Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa na sheikh Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah, kwa mnasaba wa kumbukumbu hii mahususi.
Hatimaye, semina hiyo ilihitimishwa na Masoud Msellem, Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania ambaye aliwasisitiza washiriki na Ummah wa Kiislamu kujiunga na Hizb ut Tahrir ili waweze kushughulika pamoja nayo katika kadhia nyeti ya faradhi ya kusimamisha tena Dola ya Khilafah ambayo inapaswa kuanza katika ulimwengu wa Kiislamu, ngao ya Waislamu na rehema kwa wanadamu wote.
Tunaomba kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aruzuku washiriki wote thawabu nyingi, na kuifanya semina hii kuwa nyongeza ya mwamko zaidi na ushindi kwa Ummah wetu mtukufu. Amin.
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Tanzania

-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
https://hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari/tanzania/5273.html#sigProIdfa57a37efc
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tanzania |
Address & Website Tel: +255778 870609 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz |



