Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
H. 13 Rabi' II 1444 | Na: 1444/05 |
M. Jumatatu, 07 Novemba 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uombaji Uliopangwa wa Watawala wa Tunisia kwa Badali ya Kufeli Kulikopangwa
(Imertafsiriwa)
Rais wa Tunisia, Kais Saied, akimpokea katika Kasri la Carthage, mnamo Ijumaa, Novemba 4, 2022, Dkt. Abdel Rahman bin Abdullah Al Hamidi, Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfumo wa Fedha wa Waarabu, mbele ya Mkurugenzi wa Benki Kuu, Marwan Al Abbasi.
Katika hotuba yake, Al-Hamidi alisema kuwa mkutano huo, kwa ujumla, unaangazia mabadiliko makubwa yanayotokea nchini Tunisia katika suala la kupitisha mpango wa kiuchumi na kukubaliana na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa kuhusu mpango huu, na kuzingatia kuwa hii itakuwa "mwanga kwa ajili ya mageuzi makubwa yatakayofanyika katika nchi hii katika kufikia viwango vya juu vya ukuaji na kuvutia uwekezaji kutoka nje.”
Siku hiyo hiyo, Waziri Mkuu Najla Boudin Ramadan alimkaribisha katika Kasri la Serikali huko Kasbah. Mkutano huu ulifanyika baada ya kutiwa saini kwa makubaliano ya "mkopo wa kawaida" kati ya Tunisia na Mfuko wa Fedha wa Waarabu, chini ya kiasi cha dolari milioni 74 za Kimarekani.
Enyi Watu nchini Tunisia, sisi katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia, kuhusiana na hili, tunasema yafuatayo:
1. Uhalisia wa hali unaonyesha na kuthibitisha kwamba mikopo hii inaifunga serikali, inafukarisha nchi na watu, na kuuweka rehani utashi wake kwa wengine. Deni lilikuwa - na lingali ni - chaguo la kwanza na rasmi la kiuchumi kwa dola ya Tunisia, na liliongezeka kwa mtindo, kwa idadi na ubora baada ya mapinduzi, ambapo kiasi cha deni kiliongezeka maradufu kati ya 2011 na 2022 kufikia takwimu hii ya juu (dinari bilioni 115), sawa na asilimia 80 ya pato la taifa.
2. Hotuba ya Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Fedha wa Waarabu, Abdul Rahman Abdullah Al-Hamidi, ni hotuba ya kibepari kwa bora wake, na kwa lugha ya tawala maiti za Kiarabu ambazo zimeendelea kufuata mantiki ya duara za kigeni na dola za kikoloni zilizopora neema za nchi yetu.
Hata alipozungumzia mikakati na taratibu, kama vile "mageuzi ya kiuchumi" ambayo serikali ya rais inakuza kwa kufuata maagizo ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Fedha wa Waarabu hakuweza kuficha mawazo hayo ya tawala zilizopo katika nchi yetu ambazo zinajumuisha migawanyo ya Sykes-Picot, kwani ni tawala zile zile ambazo zimekuwa zikipora mali ya Ummah, na kumiliki mali zake za umma za mafuta na madini, na kuzisafirisha kwa magendo hadi Magharibi ya kikoloni.
3. Kuweka matumaini kwenye sera ya ombaomba inayofuatwa na serikali ya rais hakuwezi kutatua mgogoro wa Tunisia! Uharibifu mkubwa ulioletwa kwa nchi yetu kwa sababu ya sera hii ya kudhalilisha umekuwa wazi kwa kila mtu, na meza za kupendeza ambazo duara za uporaji huficha pazia zao zimefichuliwa, na uharibifu ulioikumba Tunisia kama matokeo ya hili sio chochote ila ushahidi bora.
Enyi Watu nchini Tunisia: Aibu iwe kwa wale wanasiasa ambao hawakuridhika na miaka hii yote duni ya uharibifu wa masanduku ya uporaji. Je, mpaka lini nyinyi watoto wa Tunisia ya kijani mtabeba mzigo wa hawa watawala waliozipa mamlaka nchi za kikoloni kwa nchi zenu na uwezo wake, wakifanya ufisadi ndani yake?!
Masuluhisho ya matatizo ya kiuchumi ya Tunisia na nchi nyinginezo za Kiislamu si kwa kukopa kwa msingi wa riba, na kuchukua kile ambacho Mwenyezi Mungu Mtukufu amekikataza kwa haramisho kali pale aliposema:
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبا إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ فَإِنْ لَمْ تَفْعَلُوا فَأْذَنُوا بِحَرْبٍ مِنَ اللَّهِ وَرَسُولِهِ)
“Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizo bakia, ikiwa nyinyi ni Waumini. Basi mkitofanya jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilmali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe!” [Al-Baqarah 2:278-279]. Bali, ni kwa kutekeleza mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu kwa kuchuma rasilimali za dola kama vile Mwenyezi Mungu alivyohalalisha na kuruhusu; kuanzia zaka ya biashara, fedha, rikaz (hazina iliyozikwa), kharaj, ushri, ngawira, na mali za umma kama vile mafuta, gesi, madini na nyinginezo, na kuzitumia katika malengo ambayo sheria iliyapitisha. Pamoja na kutatua matatizo mengine ya maisha ya kisiasa na kijamii, siasa za kimataifa na elimu chini ya Dola ya Khilafah, inayobeba masuluhisho sahihi na yenye ufanisi kwa matatizo yetu na matatizo ya dunia nzima.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Tunisia |
Address & Website Tel: 71345949 / 21430700 http://www.ht-tunisia.info/ar/ |
Fax: 71345950 E-Mail: tunis@htmedia.info |