Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
H. 22 Rabi' II 1444 | Na: 1444/07 |
M. Jumatano, 16 Novemba 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kongamano la Nchi Zinazozungumza Kifaransa Lililofanyika nchini Tunisia ni Kongamano la Kufeli na Usaliti
(Imetafsiriwa)
Kongamano la 18 la marais wa nchi na serikali zinazoshirikiana matumizi ya lugha ya Kifaransa, linaloitwa Kongamano la Nchi Zinazozungumza Kifaransa (Francophone), litafanyika katika kisiwa cha Djerba mnamo Novemba 19 na 20, 2022, baada ya vikwazo vya mara kwa mara tangu ilipotangazwa mnamo 2020 kwamba litafanyika katika nchi yetu.
Sisi, katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia, tunapenda kuwakumbusha umma mambo yafuatayo:
1- Kwa kuwa Ufaransa inafahamu vyema athari ya lugha kwa watu na katika kuboresha thaqafa na fahamu zao, inajitahidi leo kuyaregesha makoloni yake kupitia kueneza thaqafa yake na kulazimisha lugha yake kwa baadhi ya nchi, ikiwemo Tunisia ili kukazanisha mshiko wake juu yake na kuitawala kwa mujibu wa hadhara yake. Kongamano hilo la ‘Francophone’ sio chochote zaidi ya kuwa ni chombo ambacho Ufaransa hukitumia kuimarisha miguu yake miongoni mwa dola kubwa zinazofanya kazi kumiliki na kudhibiti ulimwengu.
2- Francophone leo ni nyenzo mojawapo ya ukoloni katika mapambano yake na Umma wa Kiislamu, na ni sehemu ya mpango wake wa kuendeleza utawala kwa sababu ubabe juu ya fikra za watu, ikiwa ni pamoja na lugha zao, fikra zao na maadili uliyobeba, huwafanya wawe chini ya upofu. Mawazo ya Magharibi, na hii inaelezea msisitizo wa Rais wa Ufaransa, hata wasiwasi wake wa kulazimisha lugha ya Kifaransa. Alipotembelea Tunisia mwaka wa 2018, alithibitisha kwa uwazi, badala yake kwa usemi mbaya, kwamba "Francophone sio mradi wa zamani, lakini ni mradi wa siku zijazo, kwani kuzungumza lugha ya Kifaransa ni fursa ya kweli, katika viwango vya lugha, kiuchumi na kitamaduni. " Mradi huo, basi, ni mradi wa kisiasa na wa kistaarabu ambao unalenga kuwadhoofisha watu na kuwavua tamaduni zao, na kuzingatia nchi za Kiislamu zinazoasi nchi za Magharibi hasa kuna dalili zaidi ya moja: unalenga kupenya kiutamaduni; sio siri kwa mtu yeyote kwamba Ufaransa inapigana vita dhidi ya Uislamu kwani uungaji mkono wake kwa wale wanaomtukana Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ni maarufu, na uadui wake dhidi ya Uislamu ni dhahiri na unajirudia mara kwa mara, na sheria zake ilizoziweka kupigana kila. udhihirisho wa Uislamu nchini Ufaransa unajulikana kwa ulimwengu wote.
2- Uzungumzaji Kifaransa leo ni nyenzo mojawapo ya ukoloni katika mapambano yake na Umma wa Kiislamu, na ni sehemu ya mpango wake wa kuendeleza utawala kwa sababu ubabe juu ya fikra za watu, ikiwemo lugha yao, fikra zao na maadili inayoyabeba, huwafanya wawe wafuasi kiupofu wa fikra ya Kimagharibi, na hili linafafanua msisitizo wa Rais wa Ufaransa, hata kupagawa kwake na kulazimisha lugha ya Kifaransa. Alipotembelea Tunisia mwaka wa 2018, alithibitisha kwa uwazi, bali kwa usemi mbaya, kwamba “Uzungumzaji Kifaransa sio mradi wa zamani, bali ni mradi wa mustakbali, kwani kuzungumza lugha ya Kifaransa ni fursa halisi, katika viwango vya lugha, kiuchumi na kithaqafa.” Mradi huo, basi, ni mradi wa kisiasa na wa kihadhara unaolenga kuwalemaza watu na kuwavua thaqafa yao, na kuzingatia nchi za Kiislamu zinazoasi dhidi ya Magharibi hasa kuna ishara zaidi ya moja: inalenga kupenya kithaqafa; sio siri kwa mtu yeyote kwamba Ufaransa inapigana vita dhidi ya Uislamu kwani uungaji mkono wake kwa wale wanaomtukana Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ni maarufu, na uadui wake dhidi ya Uislamu ni dhahiri na unajirudia mara kwa mara, na sheria zake ilizoziweka kupiga vita kila udhihirisho wa Uislamu nchini Ufaransa unajulikana kwa ulimwengu wote.
3- Bourguiba alikuwa mmoja wa wasaidizi wa Francophone katika nchi yetu na mashuhuri zaidi kati ya wasomi hao ambao walinyimwa utashi wao na kupoteza uwezo wao wa kuona na kuona mbele. Sio siri kwamba alitoa huduma kwa Francophone, sio tu Tunisia, lakini katika Maghreb yote. Pendekezo lake mnamo 1965 lilikuwa kuanzisha “Jumuiya ya Madola ya Ufaransa ambayo inajumuisha watu wote wanaozungumza Kifaransa.” Alijivunia kuwa baba wa kiroho wa Francophone huko Maghreb. Alisema katika moja ya mahojiano yake: “Mustakabali wetu unafungamanishwa na mustakabali wa Magharibi kwa jumla na mshikamano na mustakabali wa Ufaransa hasa... Leo tunaelekea tena Ufaransa. Ni mimi niliyeongoza vuguvugu la kutaka Francophone; uhusiano wa kilugha unaounganisha nchi mbalimbali za Kiafrika una nguvu zaidi kuliko tabianchi au jografia.”
4- Leo Rais Kais Saied anafuata nyayo za Bourguiba, lakini labda anashindana naye. Kwake, Ufaransa sio koloni wala mhalifu, bali ilikuja Tunisia kuilinda (hivyo tu!), na hakomi kupigania kongamano la nchi za Francophone na kuwatishia wale wanaojaribu kulitibua, huku akitupia tuhuma dhidi ya pande ambazo hakuzitaja majina ambazo zinalenga kuvuruga juhudi za nchi yake kuandaa kongamano hili.
Enyi watu wa Tunisia:
Sisi katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia tunathibitisha kwamba ukoloni umefeli vibaya katika nchi yetu, licha ya uwezo wake mkubwa wa kimada na licha ya jeshi la vibaraka na wale waliopagawishwa na thaqafa ya Kimagharibi kama Bourguiba, licha ya kwamba haikuweza kuwatoa Watunisia kutoka katika Uislamu. Hawakuweza kuung'oa kutoka kwa nafsi na nyoyo, na kuvunjika moyo kwao kulikuwa kukubwa. Kila kitu walichokifanya kuwatuliza watu kiliambulia patupu, na mapinduzi yalikuwa dhidi ya urithi huu wa kikoloni wenye chuki, na watu wakajitokeza wakitaka kupinduliwa kwa serikali; utawala huu ambao ulianzishwa na Wazungu na kutabikishwa na Bourguiba na Ben Ali. Kisha wakaja watawala wapya waliodandia wimbi la mapinduzi, na wote walifanya kazi ya kuwahadaa watu kufanya mabadiliko na kuhifadhi "faida za mapinduzi." Hata hivyo, uingiliaji wao ulifichuliwa upesi, na ikafichuliwa kwamba walikuwa tu ni njia mbadala ambazo Magharibi ilikuwa imezitunga na kuzisukuma kwenye safu za mbele ili kuhakikisha kuendelea kutawala kwake. Ndio maana watu wetu wa Tunisia waliwakataa na kukataa kujisalimisha kwao. Mapinduzi bado yanatokea na hayatasimama mpaka yaung’oe ushawishi wa Magharibi na kuwaondoa pamoja nao vibaraka na watumishi wa ukoloni, na kisha isimamishwe dola halisi inayowawakilisha Waislamu na kuwachunga kwa hukmu za Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Mwenyezi Mungu (swt) asema:
(الَّذِينَ يَتَرَبَّصُونَ بِكُمْ فَإِنْ كَانَ لَكُمْ فَتْحٌ مِّنَ اللَّهِ قَالُوا أَلَمْ نَكُن مَّعَكُمْ وَإِنْ كَانَ لِلْكَافِرِينَ نَصِيبٌ قَالُوا أَلَمْ نَسْتَحْوِذْ عَلَيْكُمْ وَنَمْنَعْكُم مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ فَاللَّهُ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَن يَجْعَلَ اللَّهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلاً)
“Wale ambao wanakungojeeni, mkipata ushindi unao toka kwa Mwenyezi Mungu wao husema: Si tulikuwa pamoja nanyi vile? Na ikiwa ni sehemu ya makafiri kushinda wao huwaambia: Hatukuwa ni waweza wa kukushindeni, nasi tukakukingeni na hawa Waumini? Basi Mwenyezi Mungu atahukumu baina yenu Siku ya Kiyama, wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [An-Nisa:141].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Tunisia |
Address & Website Tel: 71345949 / 21430700 http://www.ht-tunisia.info/ar/ |
Fax: 71345950 E-Mail: tunis@htmedia.info |