Jumatano, 15 Rajab 1446 | 2025/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  12 Rajab 1444 Na: 1444/16
M.  Ijumaa, 03 Februari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kukamatwa Miongoni mwa Wanachama wa Hizb ut Tahrir

Je, Vinywa Visemavyo Ukweli Huzibwa Kwa Manufaa ya Nani?!
(Imetafsiriwa)

Kufuatia usambazaji wa toleo la Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia, lenye kichwa: "Kuporomoka kwa Dola ya Usasa, Hakuna Wokovu Isipokuwa katika Dola ya Khilafah", jana, Alhamisi 01/02/2023, Eneo la Usalama katika Nyumba ya Tamim lilimkamata mwanachama wa Hizb ut Tahrir, Ndugu Adil Al-Ansari, baada ya wito kutumwa kwake. Kikosi hicho hicho kilimkamata hapo awali na kumhamishia kwenye kikosi cha Ferjani, kisha akaachiliwa. Inatarajiwa kuwa safari hii pia atapelekwa kwenye kikosi cha Ferjani!

Gari la usalama la eneo la Walinzi wa Kitaifa huko Muhammadiyah pia lilivamia nyumba ya mwanachama Muhammad Ali Zakari kutokana na kusambaza toleo hilo na kumpeleka katika eneo lililotajwa hapo juu. Kisha aliachiliwa baada ya kuhojiwa na kutia saini ripoti kwa sababu ya kazi yake katika safu za Hizb ut Tahrir!

Sisi katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Tunisia, mbele ya dhulma hii wanayofanyiwa wanachama wa hizb, tunaeleza yafuatayo:

1- Kukamatwa kwa Mashababu wanaoeneza jumbe za kisiasa ni kashfa ya serikali ambayo inathibitisha kutokuwa na mshikamano kwa wale wanaoisimamia, na kufichua uwongo wa madai yao ya kuzingatia udhibiti wa kikatiba na kisheria ambao waliuweka kwa mikono yao wenyewe.

2- Tunaionya mamlaka dhidi ya kamatakamata hii ya mara kwa mara ya wanachama wa hizb, na tunaikumbusha serikali ilioingia madarakani ikiwaahidi watu wa Tunisia, kuacha sera za tawala zilizong’atuka zilizoitangulia, zilizowakandamiza watu hawa kwa miongo kadhaa, kisha zikaondoka bila ya huruma (kutoka kwa watu). Sera ya ukandamizaji, kunyamazisha midomo na kuzuia shughuli za hizb na kulenga mizizi yake ya kina ndani ya Umma wa Kiislamu, na ambayo ulinganizi wake wa dhati umeenea katika pembe zote za dunia, hautadhoofishwa na vitendo vilivyo chakaa na serikali zilizofilisika, wala haitadhoofisha azma ya wanachama wake.

3- Je, si jambo la aibu kwamba wanachama wetu wanakamatwa, huku wakiuangaza Ummah, na kuishauri serikali kuwa njia ya izza sio kufuata maamrisho ya mfuko wa uporaji fedha wa kimataifa, wala kuusujudia, bali badala yake, ni kuitikia wito wa kuhukumu kwa Uislamu chini ya kivuli cha dola yenye nguvu na isiyoweza kupenyeka, inayojitenga na tawala za kisekula na zilizofilisika ambazo zimezidisha tu Tunisia na watu wake taabu na dhiki?!

4- Vile vile tunawakumbusha watoto watiifu wa Ummah huu katika huduma za usalama kwamba wakoloni makafiri wanazunguka katika nchi hii, wakifanya kazi kwa bidii kukutumieni kama fimbo nzito dhidi ya ndugu zenu, na kuiweka nchi yenu chini ya ushawishi wake, na kupora neema zake, kula mali yake, na kuvuruga hatima yenu na hatima ya watoto wenu.

Hivi munawezaje kuwakamata wale wanaomfichua adui yenu mkoloni kwa ajili yenu na kile anachopanga dhidi yenu na nchi yenu?! Je, sio ajabu kwamba munamkamata mtu anayekufichulieni ukweli na kukunyoosheeni mkono wa dhati ili musiingie kwenye mitego ya wakoloni?!

Tunakariri: Vitendo hivyo vya ukandamizaji havitawavunja moyo wanachama wa Hizb ut Tahrir kuendelea mbele katika harakati za kisiasa ili kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kupitia kusimamisha Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

[وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنقَلَبٍ يَنقَلِبُونَ]

“Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.” [Ash-Shu’ara: 227]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

 #HakikiDeğişimHilafetle

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu