Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uingereza

H.  16 Jumada I 1444 Na: 1444 H / 04
M.  Jumamosi, 10 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Majibu kwa Gazeti la ‘The Sunday Telegraph’

na Tuhuma ya Kiupendeleo ya Misimamo mikali

(Imetafsiriwa)

Mwandishi wa habari kutoka gazeti la ‘The Sunday Telegraph’ aliwasiliana na Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Uingereza akiuliza kuhusu shughuli za chama na maoni ya hivi majuzi ya Mbunge mmoja ambaye alisema ana wasiwasi na ukaribu wa shughuli za wanachama wa Hizb ut Tahrir wanaoomba hifadhi katika jiji hili.

Vyombo vya habari vya Uingereza na wabunge wenye mawazo finyo husukuma simulizi za uwongo wakitumai kupata sifa duni kwa kutupa lebo ya itikadi kali. Kwa kweli ni bao la kujifunga wenyewe, kwani taasubi ya Uingereza ya kikatili na isio na huruma kwa wahamiaji unafichuliwa kwa mara nyengine tena. Sera za nimby za wanasiasa kama hao zinaonyesha kwamba wanawaona wahamiaji wenyewe kama tatizo, badala ya sera za kigeni za ukoloni mamboleo za Uingereza ambazo serikali zilizofuata zimezitabanni kwa miongo kadhaa hadi leo hii.

Wakimbizi wengi nchini Uingereza watakuwa wameteseka mikononi mwa tawala za kidikteta ambazo Uingereza imezilea na kuziunga mkono. Wanaweza kuwa tayari wanafahamu kazi ya Hizb ut Tahrir katika ardhi za Kiislamu, kwani ndicho chama pekee kinachofanya kazi kwa dhati kukomesha utawala wa kikoloni na kutabikisha tena mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kwa njia ya Utume.

Swali la kipuzi kuhusu lebo za itikadi kali ambazo vyombo vya habari vya Uingereza na wanasiasa wanapenda kutupa linafichua tu kiburi kikubwa cha wanaotuhumu. Je, wanamchukulia Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani zimshukie, kuwa ni mtu mwenye msimamo mkali, kwa kuwa alijifunga na kanuni zisizobadilika na viwango vya maadili vilivyotumilizwa kwake kama Wahyi? Je, wanawachukulia Maswahaba wa Mtume kuwa pia wanaitikadi kali kwa kushikamana na mafundisho ya Mtume (saw)? Ni tuhuma chafu ilioje hii!

Hata hivyo wanafiki hao wakubwa wanajikuta wanaweza kumbandika jina yeyote anayetaka kukomesha maovu ya ukoloni wa Uingereza kuwa ni mwenye msimamo mkali. Kwa hivyo, uhalisia wa tuhma ya uwongo umefichuliwa. Yeyote anayepinga matakwa ya kipote cha walio na upendeleo mkubwa wanaitwa watu wenye msimamo mkali, huku watu waoga na wapambe wanaoeneza uzushi na kunyamazisha sio wenye msimamo mkali.

Yahya Nisbet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Uingereza

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uingereza
Address & Website
Tel: +44 (0) 7074 192400
www.hizb.org.uk
E-Mail: media@hizb-ut-tahrir.info / press@hizb.org.uk

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu