Afisi ya Habari
Uingereza
H. 17 Rajab 1444 | Na: 1444 H / 05 |
M. Jumatano, 08 Februari 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
ZUIA UHAKIKI - Sera iliyofeli ambayo daima itashindwa kuuzuia Uislamu!
(Imetafsiriwa)
Hongera kwa Waislamu wa Uingereza! Serikali ya Uingereza imelazimishwa KWA MARA NYENGINE TENA kupitia upya sera yake ya aibu ya Zuia inayoonyesha kuwa haifai kwa madhumuni.
Kushikamana kwenu na maadili matukufu ya Kiislamu na tabia yenu njema kumefichua uwongo ulio katikati ya sera ya Zuia, na kuilazimu kurudi mwanzo kwenye uundaji kwa mara nyingine tena. Kadiri wasiokuwa Waislamu walivyozidi kuwafahamu Waislamu nchini Uingereza, ndivyo walivyozidi kuukataa ulaghai wa chuki ambao watu kama Gove na Jamii ya Henry Jackson wamekuwa wakinadi; kwamba Waislamu wote ni magaidi watarajiwa na kuongezeka kushikamana kwetu na shariah ya Mwenyezi Mungu kunapaswa kutufanya sote tuogope.
Kwa hakika, kadiri Waislamu walivyoonyesha kujali kwao mambo ya kisiasa ya watu, hususan ummah wa Kiislamu wa kiulimwengu, ndivyo tulivyozidi kupata heshima ya watu, kwani kanuni zetu zilionyesha kwamba sisi sio tatizo, bali sisi ni sehemu ya suluhisho.
Waingereza wanaweza kuona migongano katika kuwaita watu 'walio na misimamo mikali' au 'wenye itikadi kali' - hasa wakati maneno haya yanapozidi kutumiwa kufuta watu wengine wote wanaotilia shaka dori ya Uingereza katika ukoloni, uharibifu wa mazingira usio wa kawaida, na ulazimisha wa mfumo huria wa LGBTQ+.
Ni jambo la aibu kwamba Waislamu kwa mara nyingine tena wanatumiwa kama mbuzi wa kafara ili kupurukusha umakini kutokana na kufeli kwa ubepari kunako endelea: mgororo mchungu wa gharama za maisha, mgogoro wa kawi unaolaumiwa vita vya hivi majuzi badala ya mibabe wa kawi na ukosefu wa mipango, ufisadi wa wazi wa kipote cha mabepari wa Uingereza. Urasilimali hauwezi kushughulikia tsunami ya migogoro, iwe katika kitambulisho, uchumi, au sera ya kigeni.
Inabidi mtu aulize ni mara ngapi sera ya Zuia inapaswa kuundwa upya kabla ya wendawazimu wa kisekula katika serikali ya Uingereza kutambua hawawezi kuficha kufeli kwa mfumo wao?
Ripoti hiyo mpya inafichua baadhi ya migawanyiko inayozidi kuongezeka katika jamii ya Kiingereza, ikiakisi hali ya kutoridhika inayoongezeka ambayo watu wanaihisi kuelekea kwenye mfumo wa kipote cha wana huria.
Licha ya kubainisha kuwa misimamo mikali ya mrengo wa kulia na itikadi ya Incel zinaongezeka, uhakiki unafichua kuwa mpango wa Zuia kamwe haukukusudiwa kushughulika nazo. Kujumuishwa kwao kuliwahi kufichwa tu na majaribio ya Zuia ya kuupaka matope na kuudhi Uislamu na Waislamu. Lengo halisi la kuulenga Uislamu na kuwazuia watu kuuelekea kwa ajili ya kupata muongozo limekuwa wazi sana tangu kuasisiwa kwake.
Kampeni ya kuzuia kurudi kwa Uislamu kwenye jukwaa la dunia haikuanza na "vita dhidi ya ugaidi". Kipote cha mabepari wa Uingereza kina ushindani na chuki ya kale dhidi ya Uislamu, ambayo hatimaye iliwafanya kula njama na vibaraka wao kuivunja Khilafah ya Kiuthmani mwaka 1924. Tangu wakati huo, wamelazimisha na kuunga mkono kila aina ya madikteta na tawala ovu kutumikia ulafi wao wa kikoloni na kumtesa Muislamu yeyote anayelingania kukomeshwa kwa jinai hizo dhidi ya wanadamu.
Pindi Waislamu walipoanza kuhamia Uingereza kutoka makoloni ilitarajiwa kwamba wangevutiwa sana na Uingereza ya kisekula na Uislamu wao ungefifia kwa haraka. Hilo halikutokea. Bado tungali tunauamini Uislamu na maadili yake matukufu. Umma hapa na ng’ambo ya nchi una moyo mmoja unaopiga kwa pamoja, kama inavyoonyeshwa na uungaji mkono kwa Palestina, ambao unalengwa na Zuia. Sote tunarudi kwenye Dini yetu licha ya ukandamizaji wa tawala, ubadikaji majina ya kirongo kwetu kama watu wenye msimamo mkali, na sera kama vile Zuia ambazo zimesafirishwa kwenda kwa ulimwengu wa Kiislamu.
Kufeli huko kunatusaidia sisi tu kuyaona wazi zaidi maneno ya Mwenyezi Mungu,
[وَمَا هَٰذِهِ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا لَهْوٌ وَلَعِبٌ وَإِنَّ الدَّارَ الْآخِرَةَ لَهِيَ الْحَيَوَانُ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ]
“Na haya maisha ya dunia si chochote ila ni pumbao na mchezo. Na nyumba ya Akhera ndiyo maisha khasa; laiti wangeli kuwa wanajua!” [Al-Ankabut: 64]
Tunawasisi Waislamu na wasiokuwa Waislamu vilevile kuendelea kuipinga sera hii kandamizi, ambayo imefeli waziwazi na itaendelea kufeli kuwapotosha watu kutoka katika Uislamu - kama anavyosema Mwenyezi Mungu katika Quran.
[إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ يُنفِقُونَ أَمْوَٰلَهُمْ لِيَصُدُّوا۟ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ فَسَيُنفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ]
“Hakika wale walio kufuru hutoa mali yao ili kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watayatoa, kisha yatakuwa juu yao majuto, na kisha watashindwa.” [Al-Anfal: 36].
Yahya Nisbet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uingereza
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Uingereza |
Address & Website Tel: +44 (0) 7074 192400 www.hizb.org.uk |
E-Mail: media@hizb-ut-tahrir.info / press@hizb.org.uk |