Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
H. 4 Muharram 1443 | Na: 1443/01 |
M. Alhamisi, 12 Agosti 2021 |
Mashambulizi ya Wahujumu wa Ubaguzi wa Rangi Hayawezi Kuharibu Udugu wa Kiislamu!
(Imetafsiriwa)
Mfululizo wa matukio ya machafuko ulianza mnamo Jumanne jioni, 10/08/2021, baada ya kuuawa kwa kijana mmoja mwenye umri wa miaka 18 wakati wa vita katika wilaya ya Altindağ ya Ankara, ikifuatiwa na kurusha mawe katika nyumba za wahamiaji kutoka Syria na uporaji maduka yao. Wanawake na watoto wasio na hatia walivamiwa na kupigwa ndani ya nyumba zao. Lakini, matukio haya yalikuwa ni matokeo ya mfululizo wa uchochezi, na hayaakisi mwelekeo wa Waislamu wa Uturuki. Haya ni mashambulizi mabaya na yasiyokubalika, yaliyofanywa na wahujumu wachache ambao walioghadhabishwa na kuchochewa na matamshi ya kibaguzi. Wakati huo huo, ni wazi kwamba wanasiasa wanaonasibisha mgogoro wa uchumi nchini Uturuki, ongezeko la kiwango cha ukosefu wa ajira, na kushuka kwa thamani kusiko kuwa na budi kwa lira ya Uturuki, kwa ujio wa ndugu zetu wa Syria na Afghanistan haswa kwa Uturuki, wanasiasa hao ambao hutangaza kuwa watawauzia wakimbizi hao maji mara kumi zaidi, na kujaribu kuwafukuza Wasyria katika kila fursa, wao ndio wachochezi wa matukio haya.
Watu wa Uturuki ni watu wanaowakumbatia ndugu zao Waislamu waliokimbilia kwao na kushirikiana na katika mkate na masurufu yao, licha ya njama zote dhidi yao, mfumo wa kisekula wa kirasilimali unaotabikishwa juu yao na mmomonyoko wa kithaqafa waliosibiwa nao kwa karne. Bila shaka, kuna sehemu kadhaa za jamii zinazoipenda Magharibi, ambao wanahadaiwa na maneno ya kibaguzi na ambao kuuamini mfumo wa kisekula.
Maneno yetu yanaelekezwa kwao: Je! Muuaji ambaye hivi karibuni aliangamiza familia ya watu 7, wakiwemo wanawake, huko Konya na kuchoma nyumba zao, alikuwa Msyria? Na yule wa miaka 23 ambaye alimnyanyasa kingono na kumnyonga jirani yake mwenye umri wa miaka 92, alikuwa ni Msyria? Na muuaji aliyemuua mtalaka wake katika jiji la Kirikale kwa kumchinja katikati ya barabara karibu na mtoto wake, je, alikuwa ni Msyria? Hapana! Wote waliofanya mauwaji haya walikuwa ni Waturuki. Lakini Mahmud, ambaye alichimba kutoka kwenye mabaki kwa kucha zake kwenye tetemeko la ardhi la Elazig na kuokoa familia ya Aydin kutoka chini ya vifusi kwa gharama ya maisha yake, bila shaka alikuwa Msyria! Omar Khaled, ambaye aliandamana barabarani dhidi ya mapinduzi usiku wa jaribio la mapinduzi mnamo Julai 15, alipigwa risasi mbele ya Manispaa ya Istanbul na kupotewa na fahamu, pia alikuwa Msyria. Vilevile, Qusai mwenye umri wa miaka 23, ambaye alipata begi lenye simu yenye thamani ya lira 100,000 katika jiji la Sanlıurfa na kumkabidhi mmiliki wake, pia alikuwa ni Msyria ...
Kama Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alivyosema, wanadamu hawaainishwi kulingana na mataifa yao, bali kulingana na hadhi yao kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu:
«فَالنَّاسُ رَجُلاَنِ رَجُلٌ بَرٌّ تَقِيٌّ كَرِيمٌ عَلَى اللَّهِ وَفَاجِرٌ شَقِيٌّ هَيِّنٌ عَلَى اللَّهِ وَالنَّاسُ بَنُو آدَمَ وَخَلَقَ اللَّهُ آدَمَ مِنْ تُرَابٍ»
“Hivyo, watu ni aina mbili: mtu ambaye ni mchaMungu mkarimu mbele ya Mwenyezi Mungu, na mtu muovu mwenye mateso na duni mbele ya Mwenyezi Mungu. Watu ni wana wa Adam na Mwenyezi Mungu amamuumba Adam kutokana na mchanga” [Tirmidhi, Abu Daud].
Ubaguzi wa rangi ni maradhi ya watu wenye akili finyo. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:
«لَيْسَ مِنَّا مَنْ دَعَا إِلَى عَصَبِيَّةٍ وَلَيْسَ مِنَّا مَنْ قَاتَلَ عَلَى عَصَبِيَّةٍ وَلَيْسَ مِنَّا مَنْ مَاتَ عَلَى عَصَبِيَّةٍ»
“Si katika sisi anayelingania ‘Asabiyyah, si katika sisi anayepigana kwa ajili ya ‘Asabiyyah, na si katika sisi anayekufa juu ya ‘Asabiyyah” [Abu Daud].
Bila shaka, serikali inapaswa kuchukua hatua zote zinazotakikana kukabiliana na kisa hiki jijini Ankara, na kuzuia visa kama hivyo kutokea. Na ikiwa mtu atafanya uhalifu, iwe ni Msyria au Afghani au yeyote yule, basi bila shaka anapaswa kuadhibiwa kwa kuzingatia shakhsiya ya mhalifu huyo. Wakati huo huo, wanasiasa wachochezi ambao wanajaribu kupata faida za kisiasa kwa kuwatumia ndugu zetu Waislamu wahamiaji ili kusalia kwenye mandhari hiyo kwa maneno ya kibaguzi wanapaswa kuadhibiwa. Hakuna shaka kwamba dola ya Khilafah Rashidah ndiyo pekee itakayotokomeza ugonjwa wa ubaguzi wa rangi, kuondoa mipaka bandia ambayo iliwekwa kati ya Waislamu, kuwarudisha kama ndugu na kuwaunganisha tena kama mwili mmoja, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Uturuki |
Address & Website Tel: |