Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
H. 10 Dhu al-Hijjah 1442 | Na: 1442 / 16 |
M. Jumanne, 20 Julai 2021 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Enyi Waislamu: Njooni Mufanye Kazi Nasi kwa Ajili ya Khilafah Ambayo Kwayo Bishara Njema Hutimizwa na Chini ya Kivuli Chake Idd Zitarudi kama Idd!
Allah Akbar, Allah Akbar, Allah Akbar, La Ilaha Ila Allah, Allah Akbar, Allah Akbar, Wa lillahi Alhamd
(Imetafsiriwa)
Sisi katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Uturuki tunawapongeza kwa dhati Waislamu katika nchi zote za Waislamu, na ndugu na dada zetu Waislamu nchini Uturuki haswa, kwa mnasaba wa Idd al-Adha Al-Mubarak, na tunamshukuru Mwenyezi Mungu (swt) ambaye ametufanya tuishuhudia Idd hii.
Siku za Eid ni siku za umoja na mshikamano, siku za furaha na saada zilizoteuliwa na Mwenyezi Mungu (swt) kwa ajili yetu, na siku za kipekee ambazo uhusiano wa kindugu kati ya Waislamu huimarishwa, tofauti hutatuliwa, uadui kumalizwa, uhusiano wa majirani huhuishwa, Mafungamano ya kizazi hufufuliwa, na watoto na wazee wanaohitaji sana upendo na huruma hufurahi.
Uislamu ndio fungamano pekee linalotufunga katika siku hizi za haja kubwa ya umoja na mshikamano. Itikadi ya Kiislamu ndio iliyotufanya sisi wote ndugu, Waturuki, Wakurdi, Waarabu, wasio Waarabu, waLaza, waCircassi, weupe na weusi. Vivyo hivyo, Uislamu ndio ulioharamisha ukiukaji wa mali, damu na heshima ya Muislamu kwa Muislamu mwengine. Uislamu ndio uliotuamuru sisi Waislamu kupendana, kueneza rehema kati yetu, na kuwa mkono mmoja na kusaidiana katika siku ngumu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:
«المُسْلِمُ أخُو المُسْلِمِ لا يَظْلِمُهُ ولَا يُسْلِمُهُ»
“Muislamu ni ndugu ya Muislamu, hamdhulumu wala hamsalimishi.” [Bukhari].
Wakati Uislamu ulipokuwa ukitawala, na tukawa na dola ya Kiislamu hapo zamani, tulikuwa ni Umma ambao ulisherehekea Idd yake kwa machozi ya furaha, sio ya maumivu na huzuni. Tulikuwa ni Ummah ambao ulikaribisha Idd yetu chini ya bendera ya Tawhid na dola ya Khilafah kwa utulivu, furaha, na bishara njema ya ushindi na ufunguzi. Na sasa huzuni zimebadilisha furaha, Waislamu wametawanyika badala ya umoja wao, na nchi zao zimebadilishwa na ukoloni badala ya amani na usalama, ambapo damu ya Waislamu inatiririka kwa mito, na damu ya watoto wetu wasio na hatia inamwagwa nchini Iraq, Afghanistan, Syria, Turkistan Mashariki na nchi zetu zote za Kiislamu.
Enyi Waislamu: Sisi ni Ummah bora ilioletwa kwa wanadamu, kamwe hatujawahi kupoteza matumaini yetu katika ahadi ya Mwenyezi Mungu, na tunaamini ahadi ya Mwenyezi Mungu kwamba Uislamu utatawala tena maishani mwetu. Na Ummah huu utainuka na kusimama kwa miguu yake tena kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, na wito wa takbeer utarudi kuanzia Indonesia hadi Morocco, sauti yao itajaza ulimwengu wote kwa mara nyengine tena. Na bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) itarudi tena, bendera ya Al-Uqab ikipepea na neno la Tawhid (la Ilaha Ila Allah, (hakuna mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu) katika upeo wa macho, na moto wa fitna unaowagawanya watu, inaharibu udugu na kutufanya tupoteze roho itazimwa na hii.
Wahamiaji ambao wanaanza safari ya kifo kwa sababu ya maisha leo watafurahia amani katika nchi zao. Kwa hili pekee, Msikiti wa Al-Aqsa uliobarikiwa utaachiliwa huru kutokana na utekwaji nyara wake, na tohara yake, usafi na utakatifu wake zitaregeshwa. Ikiwa hii ndio hali, basi turudini kwenye Uislamu, na tutekeleze maamuzi ya Uislamu ambayo ndio kichocheo pekee cha wokovu wetu kutoka katika ile hali tulio, na tujitahidi kwa nguvu zetu ili kuregesha tena mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu. Tuachane na makafiri wa kikoloni na wasaidizi wao, watawala, na tuachane na utaifa, demokrasia, usekula na fikra mbovu nyenginezo. Batili ambayo inatekelezwa na kulazimishwa katika maisha yetu. Na njooni, enyi Waislamu, mufanye kazi nasi kwa ajili ya Khilafah ambayo chini ya kivuli chake Idd zitarudi kama Idd na Bishara Njema kutimizwa na kuwa kweli!
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Uturuki |
Address & Website Tel: http://www.hizb-turkiye.org |
E-Mail: bilgi@hizb-turkiye.org |