Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
H. 30 Rajab 1443 | Na: 1443 / 09 |
M. Alhamisi, 03 Machi 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Enyi Waislamu! Je, Haijatosha kwamba Mumekaa Karne Moja bila ya Khilafah?!
(Imetafsiriwa)
Khilafah, iliyowaunganisha Waislamu na iliyokuwa ngao ya ulinzi ya Ummah, ilivunjwa mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H, sawia na Machi 3, 1924, na nchi za Magharibi zikiongozwa na Uingereza na kwa msaada wa vibaraka wao wa ndani. Katika tarehe hii, Waislamu wakawa hawana mchungaji wala mamlaka. Baada ya kuondolewa kwa Khilafah, Waislamu waliteseka sana na kushuhudia uvamizi na uharibifu mwingi. Waingereza hawakuivunja tu Khilafah bali pia walipeana ardhi za Msikiti wa Al-Aqsa uliobarikiwa kwa Mayahudi walioikalia kwa mabavu mwaka 1948. Uvamizi wa nchi za Kiislamu na mateso ya Waislamu katika karne iliyopita bila ya Khilafah hauhesabiki kutokana na wingi. Wafaransa walitekeleza mauaji ya halaiki nchini Algeria na kuua Waislamu zaidi ya milioni moja. Mamilioni ya Waislamu, watoto, wazee, wanawake na wanaume, waliuawa na makafiri wakati wa uvamizi wa Bosnia, Afghanistan, Iraq, Turkestan Mashariki na Kashmir. Takriban Waislamu milioni moja wameuawa katika muongo huo pamoja na vita vya Syria, na mamilioni wamehamishwa kwenda katika nchi nyingine kama wakimbizi. Damu ya Waislamu haijawahi kumwagika kwa urahisi na kutelekezwa kiasi hiki wakati wowote katika historia. Nchi za Magharibi pia zimepora na kunyonya mali chini ya ardhi na juu yake katika nchi za Kiislamu katika karne iliyopita.
Baada ya kuwa na nguvu chini ya Khilafah, tumedhoofika bila yake, na baada ya kuwa na mali tumekuwa masikini, kama vile tulivyotumbukia kwenye unyonge na fedheha baada ya kuwa katika adhama na Khilafah. Baada ya sisi kuwa Ummah mmoja na dola moja ndani ya Khilafah, kwa kuvunjwa kwake, tulichanwa na kugawanywa. Pia, chini ya Khilafah, tulikuwa na Makhalifa wachamungu, wenye hadhi na mashujaa, na kisha watawala walioteuliwa walikuwa ni watawala waoga wa kikoloni na wasaliti watiifu kwa Magharibi. Kadhalika chini ya Khilafah, furaha na huzuni ya Waislamu ilikuwa moja, lakini baada ya [kutoweka] Khilafah hata nyoyo ziligawanyika. Wengine wakawa wataifa, wengine wazalendo, wengine wa wasekula na wanademokrasia, na wengine wakawa wanamambo sasa na Wamagharibi…
Enyi Waislamu: Baada ya karne moja ya kurasa nyeusi, wakati umewadia wa kufungua ukurasa msafi na mweupe kwa Umma wa Kiislamu. Wakati umewadia wa kuikomboa Palestina, kukomesha dhulma nchini Syria, na kukabiliana na mauaji ya watoto nchini Iraq na Afghanistan. Pia ni wakati wa kusimama kwa ajili ya Turkestan Mashariki na kuitikia wito wa Myanmar na Moreh!! Ni wakati wa kuunganisha Kashmir, Pakistan, India na Bangladesh. Na wakati umefika wa kufungua milango ya Makka bila ya masharti kwa Waislamu wote, na kushibisha matamanio ya Madina Al-Munawwara! Kufanya kazi ya kusimamisha Khilafah ni faradhi ya Mwenyezi Mungu kwa Waislamu wote, na hata ni taji la faradhi zote. Kwa kuwa kusimamisha Khilafah ni ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) na bishara njema ya Mtume wake (saw). Hapana shaka kuwa ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli na bishara njema ya Mtume wake hakika zitatimia. Kwa Waislamu, Khilafah si ndoto, bali ni uhalisia. Kwa kuisimamisha, tutakombolewa! Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:
«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»
“Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume”.
Enyi Waislamu: Simameni kufanya kazi na Hizb ut-Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, basi furahieni kupatikana kwa bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Hizb ut-Tahrir inakulinganieni kwenye njia pekee itakayowaokoa wanadamu, na wanakutakia kheri na kupata radhi za Mwenyezi Mungu kwa kukukumbusheni juu ya mambo mulioyasahau. Wakati umefika wa kuchukua hatua, wakati umefika wa kuvunja ukimya, wakati wa mapambano, na wakati wa Khilafah basi simameni na mfanye kazi ya kusimamisha Khilafah tena.
Enyi watu wenye nguvu na uwezo: Hizb ut Tahrir inawalingania muipe nusra ili kusimamisha dola ya Khilafah Rashida. Hizb ut Tahrir inawalingania muwe washirika katika kheri hii kubwa, basi endeleeni kumtegemea Mwenyezi Mungu (swt) Peke Yake, sio Marekani, Muungano wa Ulaya na NATO, na maregeo yenu na yawe ni Uislamu na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) si Ulaya au Urusi. Je, mtaitikia wito huu utakaokupeni nguvu, kinga, na utukufu kwa mara nyingine tena kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) na Uislamu?
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki
#ReturnTheKhilafah #YenidenHilafet #الخلافة_101 أقيموا_الخلافة#
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Uturuki |
Address & Website Tel: |