Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki

H.  12 Muharram 1444 Na: 1444 / 01
M.  Jumatano, 10 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kulaani Umbile Vamizi la Kiyahudi Pekee Si Chochote Ila tu Udhaifu
(Imetafsiriwa)

Waislamu 46 waliuawa shahidi katika mashambulizi yaliyofanywa na umbile vamizi la Kiyahudi katika Ukanda wa Gaza nchini Palestina mnamo Ijumaa, 5/8/2022, ambayo yalidumu kwa siku 3. Na Waislamu wengine watatu waliuawa shahidi katika shambulizi la majeshi ya Kiyahudi kwenye mji wa Nablus katika Ukingo wa Magharibi. Wakati huo huo, mbunge wa Kiyahudi Itamar Ben Gvir na makundi ya Kiyahudi yenye itikadi kali walivamia Msikiti wa Al-Aqsa chini ya ulinzi wa polisi wa Kiyahudi. Mbele ya mashambulizi hayo yaliyogharimu maisha ya watoto wadogo na wachanga, na kujeruhi mamia ya Waislamu, wazee kwa vijana, watawala wa nchi za Kiislamu wamenyamaza kimya kama kawaida. Msikiti wa Al-Aqsa umenajisiwa na Mayahudi, na watawala hawafanyi lolote. Hata hivyo, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu ilitoa taarifa ikilaani mashambulizi na uvamizi huo, ikisema kuwa dola hiyo ya Kiyahudi lilizidisha uhasama na kukiuka sheria za kimataifa. Kadhalika Iran, ambayo inasema kuwa imeunga mkono upinzani wa Palestina kwa miaka mingi, haijalitupia hata jiwe moja umbile la Mayahudi hadi leo. Badala yake, ilitoa taarifa mithili ya hiyo ya kulaani na kurudia uwongo ule ule kwamba inaunga mkono upinzani. Vile vile, Dola za Jumuiya ya Kiarabu na Saudi Arabia pia zilijifunga tu na kauli za kulaani. Ama Uturuki haikuridhika na kauli ya kulaani! Badala yake, ilisisitiza umuhimu wa kuhalalisha mahusiano ili kuhamisha hisia kuelekea katika suala la Palestina kwa umbile la Kiyahudi. Akizungumza katika Mkutano wa 13 wa Mabalozi, Waziri wa Mambo ya Nje Cavusoglu alisema, baada ya kulaani umbile la Kiyahudi, "Mazungumzo yetu na 'Israel' yanaturuhusu kuhamisha hisia zetu kuelekea Palestina moja kwa moja kwao." Ama kuhusu Rais Erdogan, alisema katika kikao cha chakula cha jioni alichokifanya kwa ajili ya mabalozi hao: "Pia tunatumia uhusiano wetu na 'Israel' ambayo imeregea katika mkondo wake sahihi, kutetea haki za ndugu zetu wa Palestina".

Mamlaka zinazo jumuisha Uturuki na nchi za Kiarabu, zinazoongozwa na watawala watiifu, waoga, hazifanyi chochote isipokuwa kutumikia usalama wa umbile la Kiyahudi ambalo limenyakua Msikiti wa Al-Aqsa na Al-Quds. Kwa kuwa wao si chochote ila ni watabikishaji wa sera za Marekani za kuhakikisha usalama wa umbile la Kiyahudi. Pia, kazi ya watawala hawa si lolote ila kutoa tamko la kulaani baada ya mauaji na mashambulizi yanayofanywa na umbile la Kiyahudi na kulifikisha hilo kwake. Wala hawasiti kufichua misheni zao. Wakati huo huo, watawala hawa wapewa jukumu la kuzuia hasira za Waislamu dhidi ya Mayahudi wanyakuzi na kuwakandamiza watu wao. Hii ndio sababu kuu iliyo nyuma ya uhalalisha mahusiano wa nchi za Kiarabu na Uturuki na umbile la Kiyahudi.

Enyi Waislamu: Tunawahutubia; kwa sababu watawala hawa hawako tayari kuchukua ushauri, kupenda kwao madaraka kumewalevya. Hivyo wamefumba macho yao wasiuone ukweli na wakaziba masikio yao wasisikie ushauri. Macho yao yakaigeukia Amerika, na masikio yao hayasikii isipokuwa simu kutoka Washington. Kutokana na kazi waliyonayo, watawala hawa wanaweza tu kuwa walinzi wa Tel Aviv, sio Al-Quds. Kwa njia hii, hawawezi kuwa walinzi wa watu wa Palestina, bali wa Mayahudi wanyakuzi. Ama nyinyi, hamuko hivyo enyi Waislamu. Tunajua kwamba masaibu ya Waislamu huko Al-Quds, Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni masaibu yenu pia, na kwamba huzuni yao ni huzuni yenu, na machozi yao ni machozi yenu. Basi kwa nini musiweke hisia zenu katika vitendo na musonge kwa ajili ya mabadiliko, na mushirikiane nasi kusimamisha tena Khilafah Rashida ambayo itaikomboa Palestina kwa viongozi mashujaa kama Salah Al-Din Al-Ayyubi aliye utakasa Msikiti wa Al-Aqsa na Al-Quds kutokana na Makruseda, na kuonja heshima ya utiifu kwa Khalifa Mwongofu atakayezilinda ardhi hizi, ambazo Mwenyezi Mungu (swt) amezibariki kutoka kwa makafiri, kutokana na makafiri, kama maswahaba watukufu walivyoonja heshima yake?! Wala msisahau kwamba hilo haliko mbali, na kwamba kesho iko karibu kwa wanao ingojea, na Mwenyezi Mungu akipenda, zitatimia bishara njema za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَلَتَعْلَمُنَّ نَبَاَهُ بَعْدَ ح۪ينٍ]

“Na bila ya shaka mtajua khabari zake baada ya muda” [Sad: 88].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu