Alhamisi, 14 Dhu al-Hijjah 1445 | 2024/06/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki

H.  3 Rabi' II 1444 Na: 1444 / 06
M.  Ijumaa, 28 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mustakabali Bila Shaka ni kwa Uislamu na Sio kwa Jamhuri ya Kisekula!
(Imetafsiriwa)

Jamhuri, mfumo wa Kikafiri, ilitangazwa mnamo tarehe 29 Oktoba 1923. Wakati huo, wale waliojulikana kwa utashi wao wa kusimama dhidi ya historia yetu tukufu, maadili matakatifu ya Uislamu, na umoja na nguvu ya Ummah, walishirikiana pamoja na Uingereza na Makafiri wote wa kikoloni wa Kimagharibi dhidi ya Khilafah Uthmani, na wakaivunja Khilafah na kuwachoma Waislamu visu mgongoni katika kipindi kifupi kisichozidi miezi 4 baada ya kutangazwa kwa Jamhuri.

Na hivyo tu; miaka hii 99 ambayo imepitia masaibu, ujinga, ukatili, madhara, machafuko na misukosuko, ni karne nyeusi kwa Waislamu wote wanaoishi katika nchi za Kiislamu, hasa nchini Uturuki. Ambapo Waislamu na wanadamu wote katika karne hii wamenyimwa hukmu za Uislamu, uwezo wake, heshima yake, rehema yake, baraka zake, utukufu wake na uadilifu wake. Kwa sababu wamiliki wa mfumo huu mpya, kupitia tangazo la jamhuri na kuondolewa kwa Khilafah, waliangamiza mamlaka ya Wauthmani na kuulenga umoja wa Ummah. Kupitia kupiga marufuku lugha ya Kiarabu, lugha ya Qur’an, walivunja uhusiano wa Waislamu na Uislamu, na kushambulia maadili ya Uislamu na Waislamu. Pia waliweka sheria ya kulazimisha uvaaji wa kofia za chepeu na mavazi ya Kimagharibi kwa Waislamu na kuwanyonga wale waliowapinga. Pia walifunga shule na mikusanyiko ya elimu na kuzuia ufundishaji wa Qur'an. Na wakaigeuza misikiti kuwa mazizi na wakaadhini kwa Kituruki.

Watawala ambao wamesahau maovu yote ambayo Jamhuri imeufanyia Uislamu na Waislamu wanaisifu leo. Wanasema wataendelea kufanya kazi ya kulinda na kuendeleza mapinduzi ya jamhuri, ambayo wanayaona kuwa ni mafanikio. Msemaji wa AKP Omer Celik alisema, “Jamhuri na demokrasia yetu ni miongoni mwa mafanikio yetu makubwa katika historia tukufu ya Ummah wetu. Na Jamhuri ya Uturuki milele itakuwa mchangiaji wa hili.” Kuhusu Rais Erdogan, alisema: "Tunajiandaa kwa maadhimisho ya miaka 100 ya jamhuri yetu kwa hamu, shauku na msisimko mkubwa." Kwa bahati mbaya, watawala wanajaribu kuwahalalisha wahusika wakuu mbele ya Waislamu kwa kulaumu miaka 100 ya kubaki nyuma, umasikini na utegemezi kwa wageni, sio kwa mfumo wa jamhuri na waasisi wake, bali kwa wapinzani wao wa sasa wa kisiasa kwa kampeni mpya wanayoiita "Karne ya Uturuki". Kwa hivyo, wanataka kuwaacha Waturuki kwenye vichochoro vya giza vya Jamhuri kwa karne nyingine.

Enyi Waislamu: Makafiri wa Magharibi walioiangamiza Khilafah walitawala katika nchi zetu kwa miaka mingi pamoja na viongozi wao wateule, na madikteta vibaraka walioshirikiana nao. Waliziita serikali hizi majina mbalimbali, baadhi yao ni ufalme na baadhi ni jamhuri. Wakati mwingine ziliitwa serikali za kiraia na wakati mwingine za kijeshi. Hata hivyo, Uturuki au nchi nyingine za Kiislamu haziwezi kutoa mwelekeo zaidi kwa jografiahii kwa jamhuri, ufalme au tawala za kidikteta kwa sababu Waislamu sasa wanatamani mfumo unaowalinda na kuwaletea ustawi na amani.

Enyi Waislamu: Je, hamtaki kuregesha nguvu ambazo babu zenu walizipoteza miaka 100 iliyopita? Je, hampendi kutumia Uislamu na Khilafah kuondoa kiza cha jamhuri ya miaka 100? Je, humtaki kuishi katika nchi yenye uadilifu na amani? Je, hamtaki kuwa na mtawala anayegawanya kwa haki, na asiyechukua kutoka kwa maskini na kuwapa matajiri?

Enyi Waislamu: Kwa hakika mustakabali ni kwa Uislamu, si kwa jamhuri ya kisekula. Je, hamtaki kushuhudia karne ya Uislamu baada ya mwisho wa karne ya ubepari? Je, hamtaki kuwa mojawapo wa waanzilishi wa Khilafah Rashida ambao mutaacha alama yake katika karne hii? Basi msizubae, na jitahidini kusimamisha Khilafah, ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na bishara njema ya Mtume Wake, amani iwe juu yake!

[وَفِي ذَٰلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ الْمُتَنَافِسُونَ]

Na katika hayo washindanie wenye kushindana.” [Al-Mutaffifin:26]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu