Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
H. 28 Rabi' II 1444 | Na: 1444 / 07 |
M. Jumanne, 22 Novemba 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Je, sio Wakati sasa wa Kuiwajibisha Marekani na Nchi za Kimagharibi, Wachochezi wa Ugaidi?!
(Imetafsiriwa)
Mnamo Jumapili, Novemba 13, 2022, shambulizi baya la kigaidi lilifanyika Taksim, Istanbul, ambapo mlipuko uliua watu 6, wakiwemo watoto 2, na kujeruhi watu 81. Mamlaka zilitangaza kwamba shambulizi hilo la kigaidi lilitekelezwa kwa maagizo ya Chama cha Wafanyikazi wa Kurdistan/Chama cha Umoja wa Kidemokrasia/Vitengo vya Ulinzi wa Watu. Kwa hivyo, jioni ya Novemba 19, operesheni ya anga ilizinduliwa dhidi ya vituo vya kigaidi kaskazini mwa Syria. Kisha, Jumatatu, Novemba 21, Syria ilifanya shambulizi la kombora kwenye wilaya ya Karkamish ya Gaziantep, ambapo makombora yalipiga shule na nyumba na kuua mtoto na mwalimu. Matibabu ya mama mjamzito aliyejeruhiwa vibaya bado yanaendelea.
Kwanza kabisa tunamuomba Mwenyezi Mungu awarehemu Waislamu waliofariki katika mashambulizi hayo mabaya, rambirambi na subira kwa familia zao, na tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awape nafuu ya haraka majeruhi ambao wanaendelea kupokea matibabu.
Nchi za Kikoloni za Kikafiri, wahusika halisi wa vitendo hivi vya kigaidi chungu nzima, bila haya walitoa ujumbe wa rambirambi kupitia balozi zao kana kwamba hakuna kilichotokea! Ingawa waziri wa mambo ya ndani alisema hakukubali rambirambi za balozi wa Marekani, Erdogan alikubali rambirambi za Biden na kumshukuru katika Mkutano wa G20. Kila mtu anajua, Amerika ndiye kiongozi wa dola za kikoloni, kwani ilifungua kaskazini mwa Syria kwanza kwa mashirika ya kigaidi ya PKK/PYD ili kukandamiza mapinduzi ya Syria na kuupa uhai utawala katili wa Assad. Pia ilianzisha PKK yake kaskazini mwa Syria, dhidi ya PKK inayounga mkono Uingereza inayoungwa mkono na Barzani kaskazini mwa Iraq, na kuwapa mafunzo na kuwasaidia kwa makumi ya maelfu ya malori ya silaha na risasi. Kwa upande mwingine, maafisa wa Uturuki walitazama kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika kipindi hiki, na hata kufikia hatua ya kukutana na Salih Muslim, mwakilishi wa Chama cha Muungano wa Kidemokrasia, katika ngazi rasmi jijini Ankara.
Sisi, katika Hizb ut Tahrir/Wilayah Uturuki, tunawataka tena watawala suluhisho msingi dhidi ya ugaidi, enyi watawala: Mabomu yanayolipuka katika miji yetu hii leo na matukio yote haya ya kigaidi ni dhihirisho la ushirikiano na Marekani na nchi nyingine za kikoloni. ambayo nyinyi ni marafiki, washirika na washirika wa kimkakati naye. Hata kama kuamiliana mashirika ya kigaidi kutabadilika. Wahalifu wa kweli ni wakoloni. Kwa hiyo, hamuwezi kuyatatua matatizo haya kupitia kushiriki katika njama chafu za wakoloni na kuendelea kushirikiana nao. Na ikiwa kweli munataka kupigana na ugaidi, komesheni mabomu yasilipuliwa katika miji na kulinda maisha ya raia wasio na hatia, hatua ya kufanya ni wazi. Je, inakubalika kwa nchi kubwa kama Uturuki kupambana na mashirika ambayo ni mwanakandarasi mdogo wa ugaidi, ndani ya mipaka iliyowekwa kwa ajili yake? Kwa hiyo huwezi kubakia washirika wa Uingereza na nchi nyingine za Ulaya huku mnaipiga vita PKK! Huwezi kudumisha ushirikiano wenu wa kimkakati na Amerika huku mnaipiga vita PYD/YPG! Huwezi kuwa marafiki na Putin, ambaye alitoa ruhusa kwa PYD/YPG kufungua afisi jijini Moscow!
Kupambana na ugaidi ni suala la ikhlasi. Katika mapambano haya, fahamu "gaidi wenu ni mbaya, gaidi wangu ni mzuri", kama serikali ya sasa na watawala wanafiki wanavyofanya, haiwezi kukubalika. Ambapo mapambano dhidi ya ugaidi yanaanzia kwa kutomchukulia gaidi kuwa ni halali na kutomshughulikia. Lakini munafanya kazi pamoja na Amerika, dola kubwa zaidi la kigaidi duniani, katika maeneo mengi. Na munawaita marais wa kigaidi wa Marekani marafiki zenu. Na munashirikiana na nchi za Ulaya zinazoua watu wasio na hatia kwa maslahi yao binafsi. Pia hamuoni aibu kusalimiana na mikono yenye damu ya Sisi, ambaye aliwatumia "majambazi" kuwaua watu wa Misri katika uwanja wa Rabaa. Pia munabarizi na Amir wa Imarati, ambaye mulimlaumu kwa jaribio la mapinduzi la Julai 15, kwa pesa chache. Pia muna hamu ya kukutana na Assad, mchinjaji ambaye kitendo chake cha kigaidi huko Reyhanli mnamo 2013 kiliua watu 53 na kujeruhi wengine 146. Pia munamsubiri Devlet Bahceli akufungulieni njia hilo. Kwa njia hii, hamuwezi kupigana na ugaidi, wala kuwahisabu magaidi kwa uadilifu, wala kuwalinda watu wetu wasio na hatia, wala kupata radhi za Mola wa Walimwengu, Mwenyezi Mungu Mtukufu! Wakati umewadia wa kuwawajibisha wahusika halisi wa vitendo hivi vya kigaidi vinavyotudhuru! Tutasubiri hadi lini?
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Uturuki |
Address & Website Tel: |