Jumanne, 14 Shawwal 1445 | 2024/04/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki

H.  16 Rabi' II 1441 Na: 1441 / 06
M.  Ijumaa, 13 Disemba 2019

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Nani Atakayeiunga mkono Turkistan Mashariki… Nani Atakayesema Imetosha kwa Udhalimu wa Uchina?!

(Imetafsiriwa)

Siku ya Ijumaa tarehe 13 Disemba baada ya swala ya Ijumaa, Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Uturuki iliandaa jukwaa la usomaji wa taarifa kwa vyomba vya habari kwa jina "Nani atakayeiunga mkono Turkistan Mashariki... nani atakayesema imetosha kwa Udhalimu wa Uchina?!" mbele ya msikiti wa Malika Khatun mjini Ankara, Ubalozi wa Uchina ndani ya Istanbul, Msikiti wa  Ulu huko Adana, Msikiti wa Al-Sina'a huko Hattay, na msikiti wa Alu huko Mersin. Umati wa watu kutoka miongoni mwa Waislamu na ndugu na dada wahamiaji kutoka Turkistan Mashariki walishiriki katika matukio, ambayo mambo yafuatayo yalisisitizwa:

Enyi Waislamu! Ummah bora ulionyanyuliwa kutoka kwa Wanadamu! Uombolezi wa vilio vinavyo nyanyuka kutoka Turkistan Mashariki hutingisha Kiti cha Enzi cha Mwingi wa rehema, hamusikii? Kiti cha Enzi cha Mwingi wa Rehema kinatingishika kwa mashtaka yao, hamuhisi? Na ndugu zenu Waislamu wa Uyghur wanauwawa kikatili bila huruma, hamuoni? Wanakumbwa na mateso na dhuluma zinazotingisha kila mwanadamu, kwa hivyo ni nani atakayekomesha ukandamizaji wa Makafiri hawa wa Kikomunisti? Nani atasema 'imetosha' kwa malalamiko haya? Je ni Umoja wa Mataifa ambao awali waliwakabidhi Waislamu wa Bosnia kwa wachinjaji wa Serb?! Je mwasubiri msaada kutoka kwa Umoja wa Mataifa unaochukua maamuzi yake kwa kunyakua ardhi za Waislamu kwa ajili ya maslahi ya Amerika?! Naapa kwa Mwenyezi Mungu, kuikabidhi hatima ya Waislamu nchini Turkistan Mashariki kwa Umoja wa Mataifa, na kutafuta suluhisho kwa shirika hilo, si jingine bali ni kukiuka haki za Waislamu wa Uyghur, na kuwakilisha masuala ya Turkistan Mashariki kwa Umoja wa Mataifa si lolote bali ni usaliti kwa ndugu zetu Waislamu.

Enyi Watawala katika Ardhi za Waislamu! Mumekosea sana hapo zamani! Mumeiweka biashara yenu juu ya ubinadamu wenu, ufahari na heshima, na mukawapa mgongo ndugu zenu Waislamu kwa kuogopea mahusiano yenu na Uchina. Kuwahifadhi ndugu zenu Waislamu wa Uyghur na kuwaokoa wao kutokamana na mateso ya Uchina ni wajibu juu yenu, kwa hivyo musiwape mgongo ndugu zenu wahamiaji wa Uyghur kutoka Turkistan Mashariki ambao wametaka hifadhi kwenu kama ndugu zao na wametaka hifadhi kutoka Anatolia, ambayo ni maarufu kwa huruma yake

Na nyinyi, makafiri wavamizi wa Kichina: musiwache kimya cha watawala wa Kiislamu kiwadanganye, wala ukubwa wa idadi yenu usiwadanganye, na mujue kuwa madhila yenu hayataendelea hadi siku ya kufufuliwa. Hivi karibuni, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, Khilafah ya Uongofu kwa njia ya Utume itasimama, na Waislamu wataungana chini ya Bendera moja, mioyo yao itaungana, malengo yao yataungana; majeshi yao yataungana, na itawakomesha Madhalimu wote na wanyanyasaji kama nyinyi.

Enyi Ndugu zetu Waislamu wa Turkistan Mashariki! Ishikilieni dini yenu licha ya dhuluma zote munazotekelezewa, ishikilieni kisawasawa, na muendelee kuwafundisha mafundisho ya Uislamu watoto wenu. Imani hii ndio uokovu wenu na uokovu wa watoto wenu na vizazi vitakavyokuja baada yenu katika ulimwengu huu na siku ya hesabu.

Jihadharini na wale ambao hawaoni suala lenu kama njia ya Uislamu, na kuwaalika nyinyi katika ukabila na utaifa. Na musisahau kuwa suala la Turkistani Mashariki ni suala la Uislamu, na Uislamu unapokosekana, basi hakuna nyumba au nchi! Na Mwenyezi Mungu, utukufu uwe Kwake, Aliye epukika kutokamana na udhaifu wowote, Anasema:

(إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ)

“Hakika bila shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watakapo simama Mashahidi” [Ghafir: 51]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Wilayah Uturuki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu