Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
H. 11 Dhu al-Qi'dah 1441 | Na: 1441 / 15 |
M. Alhamisi, 02 Julai 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Msimamo Munaotaka Watu Wauchukue Dhidi ya Muozo wa Maadili
Ambao Mumeusababisha kwa Mikono Yenu Wenyewe uko Mbali na Ikhlasi!
(Imetafsiriwa)
Mnamo Jumatatu, Juni 29, Raisi Erdogan alitoa taarifa ambayo kwayo aliyahutubia makundi ya wapenzi wa jinsia moja, wasagaji, mashoga, makhuntha, na watu walio badili jinsia asili kwenda jinsia ya pili (LGBT), na akasema: "Mmoja wao ameshambulia vibaya maadili yetu ya kiakhlaqi na ya kidini. Lengo lao ni kutia sumu mabongo ya vijana na wale wanaounga mkono mitindo hii isiyo ya kawaida kwa mtazamo wetu ni washirika wa upotovu huu. Natoa wito kwa watu wetu walioko hapa kuchukua msimamo dhidi ya wale wanaounga mkono upotovu huu ambao Mola wetu ametuharamishia."
Unapoitazama taarifa hii, inaonekana kana kwamba Raisi wa Jamhuri Erdogan amesahau wadhifa wake wa utekelezaji na kuhamisha jukumu kwa watu! Zaidi ya hayo, historia ya kisiasa ya hivi karibuni ni ushuhuda kwa serikali hii tawala na mamlaka yake iliyo ruhusu miko, ufisadi na upotofu wote na kufungua njia kwa fikra zote potofu zinazo pelekea kuvua maadili ya kijamii, kudhoofidha mafungamano yao na kuchana umoja wake! Ni Raisi Erdogan ndiye aliye waita wale waliopotoka milangoni mwa uchaguzi kwa dhana ya "kura moja yamaanisha kura moja" na kwenda katika nchi za Kimagharibi kupata usaidizi wao, na huku akisema: "Ni lazima kuwepo na dhamana ya kisheria kwa haki za wapenzi wa jinsia moja ndani ya mipaka ya haki na uhuru wao"! Na maandamano ya kila mwaka ya kujifakhirisha yanayo andaliwa na watu wenye upotofu wa kijinsia yamefanyika tu wakati wa utawala wa Chama cha Uadilifu na Maendeleo (AKP). Na Kongamano la Istanbul, linalo tetea haki za mwelekeo wowote wa kimapenzi na kulinda mitindo yote hii, lilitiwa saini mnamo 2011 wakati wa idara ya serikali ya AKP! Na aliyemteua raisi wa kamati ya usimamizi wa mitihani ya vyuo vikuu, iliye husisha mada inayo sifu mapenzi yaliyo potoka ya jinsia moja, si mwengine ila ni raisi wa jamhuri! Ikiwa ni muhimu kuchukua msimamo dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na mashirika yao; basi ni wajib kwamba chama tawala na Erdogan wafanye hivyo, kwani wao ndio walio kileleni mwa tawi la utekelezaji ambalo kwalo upitishaji na utabikishaji wa sheria hufanyika.
Enyi Watawala: Vipi mnatarajia watu kuchukua msimamo dhidi ya upotovu huu ilhali mnauhami kisheria?! Ni ujinga gani huu, na ni mgongano gani huu? Serikali ndiyo inayo pitisha sheria ili kulinda watu wake kutokana na vitendo viovu na amali mbaya, na huwaadhibu wale wanaokiuka sheria hizi, ikihakikisha nidhamu ya kijamii, na kumaliza kila kitu kinacho dhuru mujtamaa, na kwa njia hii, huwalinda watu wake kutokana na fikra na suluki zozote potofu. Hivyo basi, ulindaji watu kutokana na amali mbaya na vitendo viovu ni kazi msingi ya dola, basi vipi watu wataelezwa: "Tafadhali jilindeni kutokana na amali mbaya" bila ya dola kufanya lolote?! Ikiwa dola imeshindwa kuwalinda watu wake, vipi watu watajilinda wenyewe kutokana na utendaji wa amali mbaya?!
Ama kwako wewe, Raisi wa Jamhuri: Ikiwa unaamini kuwa mapenzi ya jinsia moja, uhalifu na uzinzi hayaoani na maadili ya mujtamaa, basi ambaye anapaswa kuchukua msimamo wa kwanza dhidi yake ni serikali, hivyo unapaswa kuchukua hatua ya kwanza kabla hujachelewa. Mashirika yote ya mashoga ni lazima yafungwe na amali zao kusitishwa. Unapaswa kuzuia ulinganizi wa mapenzi ya jinsia moja, usifiaji, uungaji mkono, kuyapa uhuru na uhalali wake kama kiongozi wa dola, na kumhisabu kila anaye fanya yoyote katika hayo kwa adhabu kali. Ni lazima ufutilie mbali sheria zote zinazo dhamini ulinzi wa mapenzi ya jinsia moja, ya kwanza yake ikiwa ni Kongamano la Istanbul na kulivunjilia mbali. Hapo ndipo pekee tutakapo sema: "Tumefanya kila tuwezalo, na sasa ni zamu yenu!" lakini, kuwaambia watu kuchukua msimamo kabla ya hilo, lenyewe ni unafiki, na limekosa uaminifu na ikhlasi!
Katika kutamatisha, tunawaambieni, Enyi Waislamu: chimbuko la vitendo viovu na amali zote mbaya ni hii nidhamu ya kikafiri, kisekula, ya kidemokrasia na uovu utaendelea kuenea ndani ya mujtamaa mithili ya janga la maambukizi maadamu nidhamu hii ingalipo!
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Wilayah Uturuki
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Uturuki |
Address & Website Tel: |