Alhamisi, 24 Jumada al-awwal 1445 | 2023/12/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  19 Muharram 1445 Na: 1445 / 01
M.  Jumapili, 06 Agosti 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kubadilisha Serikali kwa Takwimu Mpya za Uongozi si Lolote zaidi ya Kutia Viraka Mfumo!
(Imetafsiriwa)

Baada ya muda mfupi kufuatia kuchaguliwa kwa Shavkat Mirziyoyev kama rais kwa mara ya tatu, alianza mfululizo wa mageuzi, lengo kuu likiwa ni suala la wafanyikazi. Inafaa kukumbuka kuwa zaidi ya maafisa 80 kutoka ngazi mbalimbali za mahakama, masuala ya ndani na mfumo wa kodi walifutwa kazi. Leo, hali ya kisiasa na kiuchumi nchini, na pia nyanja ya elimu, iko katika hali ya kusikitisha, na ukosefu wa ajira umeenea. Uovu kama vile rushwa, ufisadi, ukabila, na uhalifu mbalimbali umekita mizizi. Zaidi ya hayo, katika wakati ambapo raia wa nchi hiyo wanaofanya kazi nje ya nchi, hasa nchini Urusi, wanakabiliwa na ubaguzi, matatizo ya kiuchumi, ukiukwaji wa haki zao, na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa visingizio mbalimbali, ikifuatiwa na kuburuzwa katika vita vya Ukraine, serikali ya Mirziyoyev haiwezi kufanya kazi kwa ujasiri kama nchi huru kuwalinda. Yote haya yanaimarisha hali ya mfadhaiko na kukosa imani nayo miongoni mwa wananchi.

Hivyo basi, mara tu baada ya uchaguzi, serikali ya Mirziyoyev ililazimika kuanzisha idadi ya mipango mipya na kuanza kuzitambua na kuzitenga "pande zenye hatia." Kwa msingi wa ukweli uliotajwa hapo juu, tunaweza kutambua kuwa kuna malengo mawili yaliyokusudiwa:

Kwanza, kufufua matumaini ya watu ambao bado hawajachoka kungojea baadhi ya mabadiliko chanya, kumaliza mfadhaiko wao, na kwa maana nyengine, kuwadanganya kwa mara nyengine tena kwa kipindi fulani na kubangaiza wakati.

Pili, kuwaonyesha maafisa hao kuwa wao ndio chanzo halisi cha ongezeko la ukosefu wa ajira nchini, matatizo ya kiuchumi na kuenea kwa uhalifu.

Je, kihakika hili ni kweli? Je, dhiki na mgogoro uliopo sasa ni matokeo ya ukweli kwamba maafisa hawatekelezi majukumu yao kwa uwajibikaji? Na je kubadilishwa kwao kutasababisha kuboresha hali hiyo? La hasha! Kwa sababu kuzorota kwa hali ya kisiasa na kiuchumi, shinikizo kwa elimu ya dini, na ukweli kwamba mamia ya wafungwa wa kidini na kisiasa bado wako gerezani, yote haya ni matokeo machungu ya mfumo wa kidemokrasia na mfumo wa kiuchumi wa kibepari ambao ulipigiwa kura ya maoni hivi karibuni. Basi, tafakarini maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ambaye anasema:

[وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكاً]

“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki” [Surat Ta-Ha:124].

Kwa hivyo, ni muhimu kusisitiza kwamba Mirziyoyev, kwa kuwafuta kazi maafisa kadhaa na kuwalaumu kakamilifu, kimsingi anajaribu kumaanisha kuwa watu hawa wanawajibika kwa kila kitu. Hivyo, anarefusha uhai wa demokrasia hii fisadi ya kibepari isiyofaa na ambayo watu wetu wanaonja uchungu wake. Kwa kufanya hivyo, analenga pia kuibakisha nchi yetu chini ya ushawishi wa dola za kikoloni kama vile Urusi, Marekani, na China kwa muda mrefu ujao.

Zaidi ya hayo, idhini kutoka kwa "kaka wakubwa" kwa kura ya maoni ya hivi majuzi na uchaguzi wa rais ilikuwa kweli ni badali ya "huduma ambazo hazijalipiwa." Kwa hiyo, hakuna matumaini ya kutarajiwa kutoka kwa "mageuzi" ya Mirziyoyev kwa manufaa ya Waislamu wetu. Njia pekee ya kweli ya wokovu ni kurudi kwenye Uislamu, ambao uliteremshwa kama rehma kwa walimwengu, na kuukubali kama mfumo kamili wa maisha unaosimamia mambo yetu yote. Endapo sisi Waislamu tutasahihisha fikra zetu na kuikumbatia dini yetu kwa namna hii, ni hakika kwamba Mwenyezi Mungu atatuepusha na matatizo ya leo na ataiboresha hali yetu, kama anavyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[وَمَن يَتَّقِ اللهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجاً * وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ]

“Na anaye mcha Mwenyezi Mungu humtengezea njia ya kutokea. Na humruzuku kwa jiha asiyo tazamia.” [Surat At-Talaq: 2-3].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu