Jumapili, 20 Jumada al-thani 1443 | 2022/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  26 Jumada I 1442 Na: HTY- 1442 / 18
M.  Jumapili, 10 Januari 2021

 Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

Hadi ni kama Al-Mashat, Wote Wametweza Majukumu Yao kwa Watu wa Yemen, na Wanapaswa Kung'olewa
(Imetafsiriwa)

Afisa wa afya katika mji wa Al-Anad-Tuban, mkoa wa Lahj, alielezea kuwa kituo cha afya jijini humo kimepokea watoto wengi wenye ugonjwa wa ngozi, ambao ulisababisha hali ya hofu na wasiwasi miongoni mwa familia. "Familia nyingi zimeleta watoto wao kwenye kitengo hiki cha afya na ugonjwa wa ngozi," Nabeel Qaba, naibu mkurugenzi wa Kituo cha Afya cha Al-Anad, Bir Nasser, akibainisha kuwa visa vitatu viligunduliwa katika kitengo hicho cha afya kwa dalili sawa za ugonjwa huu wa ngozi. (Wavuti wa Aden News wa gazeti la Al-Ayyam 10/01/2021)

Taarifa za maafisa wa afya huko Al-Anad na Bir Nasser juu ya kuibuka kwa ugonjwa wa vipele katika watoto na picha zilizowasilishwa na wavuti wa Al-Ayyam ni dalili dhahiri ya kiwango cha mateso ambayo watu wanapata kutokana na watawala hawa wajinga. Jukumu la kutibu magonjwa ya kawaida na ya dharura ambayo yanaenea kati ya watu ni ya madaktari ambao wanateuliwa na serikali katika hospitali, vituo na vitengo vya afya kote nchini na kwa maslahi anuwai ya watu, elimu, dawa, usalama ...".

Leo Abd Rabbo Hadi, ni kama wale waliomtangulia, wameachana na jukumu la utunzaji wa afya kwa wale walio chini ya uchungaji wao, na kulirudisha kwa watu, kwa hivyo watu lazima wawahesabu na hata kuwang'oa kwa sababu uhalifu wa watawala hawa dhidi ya Dini na Ummah wao umefika hadi angani, kwa hivyo ni wagonjwa wangapi kote nchini hawawezi kutoa huduma za afya kwao wenyewe na familia zao wanaougua magonjwa anuwai, sembuse kutibu magonjwa ambayo yanatishia maisha yao kwa sababu ya ukosefu wa dawa na ukosefu wa huduma za afya?!

Lini Abd Rabbo, ambaye yuko Riyadh, au Qasim Buhaibah, Waziri wa Afya katika serikali ya Ma'in Abd al-Malik, ambayo inatetemeka kwa hofu ya kukaa Aden, watachukua jukumu lao, na ni jukumu lao, kushughulikia matibabu ya visa vya ugonjwa ambavyo vimeonekana na kuenea kati ya watoto katika Al-Anad mkoa wa Lahj, ambayo iko karibu na mikono na masikio yao, kisha kuangalia sababu ya kuenea kwake na kuiondoa?! Bila kusahau kuwa wao ndio sababu ya visa hivi vya utumiaji wa silaha ambazo husababisha uharibifu wa kibinadamu na mazingira, haswa kwani eneo la Al-Anad hivi karibuni lilikuwa makao makuu ya kambi ya anga ya Amerika ambayo droni zilirushwa kuua watu wa Yemen kwa madai ya "ugaidi", na Al-Anad iko karibu na eneo la mawasiliano kati ya pande mbili za eneo hilo kwenye mzozo nchini Yemen, ambazo zitabadilishana tuhma juu ya sababu za kutokea kwa vipele kati ya watoto katika Al-Anad?!

Jana, 01/05/2021, Al-Mashat alikuwa na ndoto ya kuteua hospitali kwa kila gatuzi ya  magatuzi ya Yemen, na leo mpira uko katika uwanja wa Hadi kutibu mwelekeo wa ugonjwa katika Al-Anad. Wawili hao wametweza majukumu ya uangalizi wa afya ambayo ni wajibu juu yao kwa watu wa Yemen.

Katika Uislamu, jukumu la huduma ya afya liko kwa dola. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitunukiwa daktari, kwa hivyo akamfanya kuwa wa Waislamu, kwa hiyo hii ni dalili kuwa daktari ni maslahi kwa Waislamu, kisha angalieni historia ya Waislamu katika siku ambazo tulikuwa na khalifa na Khilafah jinsi walivyokuwa wakitafuta matibabu huko Bimaristan. Hakika Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume ndio ambayo itakayowajali watu kwa Uislamu, basi huu ndio wakati wake na umekuwa ni mrefu na alfajiri yake imekaribia. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

“Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” Imeripotiwa na Ahmad kutoka kwa Nu`man ibn Bashir, basi kuweni pamoja na wanaofanya kwa ajili ya kuisimamisha.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail:  aan1924@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu