Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  6 Rabi' I 1445 Na: HTY- 1445 / 05
M.  Alhamisi, 21 Septemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Je, Ni Mapinduzi Mangapi Yemen Inayohitaji ili Kubadilisha Uhalisia Wake?!
(Imetafsiriwa)

Kwa kuzingatia sherehe za kumbukumbu ya miaka 21, 2014, gazeti la al-Thawra, ambalo huchapishwa jijini Sana'a, lilichapisha kwenye ukurasa wake wa mbele kichwa cha habari kifuatacho: "Mapinduzi Yanaonyesha Umuhimu wa Uasi wa Kiuchumi na Kimaendeleo nchini Yemen" mnamo Jumamosi, 09/16/2023.

Ripoti hii na ripoti zengine zilizomo kwenye gazeti la al-Thawra katika kipindi cha wiki hii zilirundika sifa mbaya juu ya pande zote za kisiasa na kiuchumi, nk. Kama zilizofanya zile zilizopita, katika jaribio la kutupa majivu machoni mwa watu wa Yemen juu ya jinsi nchi yao ilivyokuwa, kuanzia kuenea kwa ufisadi, kuduwaa kiuchumi, na hali mbaya ya maisha, hadi vizuizi vya kisiasa na usalama, hadi kuhisi kwao kufifia kwa hadhi yao na udhalilifu walioupata chini ya mapinduzi haya, kama ilivyokuwa hali chini ya serikali za zamani.

Ni aibu kusikia vilio vya kile kinachojulikana kama uhalali na wafuasi wake kutoka chama cha Congress ndani, nje ya nchi, na chama cha Islah kikiimba kuhusu Septemba 26. Kwa upande mwingine, tunasikia na kuona Mahouthi wakiwa na wasiwasi kuhusu Septemba 21, na Hali nchini Yemen haijabadilika. Kwa kweli, hali yake leo haitaji majadiliano, kwani dhiki imefikia pomoni mwake!

Je! Tumejikomboaje kutokana na usimamizi na utegemezi, wakati Yemen inaanguka chini ya kifungu cha 7 cha Umoja wa Mataifa, na wajumbe wake wanne wakizunguka pambizoni mwa faili ya Yemen, na mashirika ya yanayovuka mipaka yanaivuruga Yemen kwa marefu na mapana?! Kama kuhusu ibara "kuwakomboa watu wa Yemen kutokana na maagizo ya kigeni na kuregesha haki yao ya uhuru, na ubwana," ni kauli mbiu ambayo watu wanatambua ukweli wake, na hawadanganywi nayo. Mifumo na sheria za Magharibi, ambazo ni kinyume na sheria ya Mwenyezi Mungu, bado zinatutawala na kudhibiti nyanja zote za maisha yetu.

Watu wa Yemen leo wanatishiwa na hatari ya kugawanywa katika sehemu karibu nusu ya dazeni, na labda zaidi kati ya miungano ya kisiasa, kikabila na kikanda. Kama vile mlivyokuwa jana mnalaani wale waliohalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi, leo mna kwenda kwao, na kesho mtawafuata katika kuhalalisha mahusiano. Ukweli, Utukufu uwe Kwake, amesema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاءَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِين * فَتَرَى الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يُسَارِعُونَ فِيهِمْ يَقُولُونَ نَخْشَى أَن تُصِيبَنَا دَائِرَةٌ فَعَسَى اللهُ أَن يَأْتِيَ بِالْفَتْحِ أَوْ أَمْرٍ مِّنْ عِندِهِ فَيُصْبِحُوا عَلَى مَا أَسَرُّوا فِي أَنفُسِهِمْ نَادِمِينَ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu. Utawaona wale wenye maradhi nyoyoni mwao wanakimbilia kwao wakisema: Tunakhofu yasitusibu mabadiliko. Huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi au jambo jingine litokalo kwake wakawa wenye kujuta kwa waliyo yaficha katika nafsi zao.” [Al-Ma’idah 5: 51-52].

Je! Tumekombolewa vipi kiuchumi wakati mfumo wetu wa kiuchumi ni wa kirasilimali, huku Benki ya Dunia na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa zinavuruga uchumi wa Yemen?! Je! Ni vipi kwamba Mpango wa Chakula Duniani, UNESCO, FAO, na UNICEF bado hujaza maghala ya nyumba zetu kwa ngano ya kigeni na misaada, wakati mazao yetu ya ngano za kisaki (GMO) yakitegemea mbegu zinazotufikia nje ya mipaka, bila kutaja umaskini, njaa, na ukosefu wa ajira, kwa kuzingatia kupunguzwa kwa mishahara ya wafanyikazi wa serikali?!

Kana kwamba miongo sita ya udanganyifu na ahadi za uwongo haijatosha kwetu tangu Septemba 26, 1962, na malengo yake sita yaliyoandikwa kwenye karatasi, bila kufikia malengo yake kiuhalisia, ili ipate bendera ya kidaganyifu na batili kutoka kwake mnamo Septemba 21, 2014, kwa kuzirudia ahadi na kwa njia ile ile ya uchochezi ambapo miaka tisa ya mporomoko imepita tangu kuzinduliwa kwake, na malengo ya mapinduzi yote mawili, ambayo kiuhalisia yanatuweka kwenye matope ya utegemezi wa kipofu kwa Kafiri Magharibi na kutengwa kutokana na Dini yetu ya haki ya Kiislamu!

Watu wa Yemen lazima wajue kuwa mabadiliko moja yanatosha kwa Yemen kubadili mwendo wake kutoka kwa hali mbaya inayoteseka kwayo, hadi usalama, utulivu, na maisha mazuri yaregeshwe kwa watu. Hayatakomea kwa Yemen pekee, bali yatapita maeneo yote kuwatoa wanadamu wote kutoka kukandamizwa na kuelekea kwenye uadilifu chini ya Dola ya Khilafah. Waislamu lazima wajiunge katika kufanya kazi ili kurudisha maisha katika Uislamu na kuishi chini ya hukmu adilifu za Mola wao, na kujitahidi sana kuziondoa serikali hizi ambazo hazitawaliwa na sheria ya Mwenyezi Mungu, na hii inaweza kufanywa tu kupitia kufanya kazi ya kusimamisha Dola ya Khilafah Rashidah ya pili kwa njia ya Utume ambayo kwayo Hizb ut Tahrir inafanya kazi. Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

[وَعَدَ اللهُ الَّذِينَ آَمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئاً وَمَنْ كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُولَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur 24:55]. Bishara njema za Mtume Wake (saw) zimethibitisha:

«...ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

“...Kisha utakuweko utawala wa kutenza nguvu, na utakuweko katika muda apendao Mwenyezi Mungu uweko kisha atauondoa apendapo kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” (Imepokewa na Ahmed).

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu