Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  2 Dhu al-Hijjah 1445 Na: HTY- 1445 / 33
M.  Jumamosi, 08 Juni 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watawala wa Yemen na Wafuasi wao Wameweka Macho na Nyoyo zao Nje!
(Imetafsiriwa)

Wakati wa mkutano wake na wanachama wa Muungano wa Ulaya, Aidarous Al-Zubaidi alisisitiza haja ya uingiliaji kati kutoka kwa jumuiya za kikanda na kimataifa kwa jumla, na hasa Muungano wa Ulaya. Mnamo Mei 26, 2024, Aden Al-Ghad aliripoti kwamba Dkt. Ali Al-Masbahi, aliyesifiwa na tovuti kama mtaalam wa kiuchumi, alisema katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba uendeshaji wa Viwanda vya Kusafisha mafuta vya Aden unahitaji uwekezaji mkubwa na wa maana. Alipendekeza kuwa serikali ihusishe kampuni za kimataifa za mafuta katika ufufuaji na uendelezaji wa Kiwanda cha Kusafisha Mafuta cha Aden kwa kutoa zabuni ya kimataifa ambayo itajumuisha kampuni maalum kama BP, Shell, Mobil na Total kuingia ushirika nayo. Zaidi ya hayo, wakati wa ziara yake jijini Moscow, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Bunge la Wananchi Faika Al-Sayyid Ba'alawi alitoa wito wa wazi, ulioripotiwa na Aden Al-Ghad mnamo Jumatano, Mei 29, 2024, kwa Urusi kuwa na uwepo katika Bahari Nyekundu na Bab Al-Mandab ili kuweka usawa katika uwepo wa kimataifa, kwa mujibu wa taarifa yake. Hili lilitokea wakati wa mahojiano na Shirika la Sputnik la Urusi.

Yeyote anayesikiliza vitendo hivi hawezi kuamini! Watawala na wafuasi wao nchini Yemen wanaonyesha kutokuwa na uwezo wa ajabu wa kusimamia masuala ya nchi hii kisiasa na kiuchumi. Hayo hayo yanaweza kusemwa kwa viongozi wengine ambao wameitawala Yemen kwa miongo kadhaa mfululizo.

Yemen inamiliki sifa zinazoiwezesha kuiongoza dunia; watu wake wanabeba Aqeedah (itikadi) tukufu ya Kiislamu, na eneo lake la kipekee la kijiografia linatazamana na Bahari ya Nyekundu pamoja na Bahari ya Arabia, pamoja na rasilimali zao za baharini na bandari.

Zaidi ya hayo, ina maliasili kama vile mafuta na madini, pamoja na kilimo. Inakosa tu mtu anayeweza kuitawala kwa uwezo kamilifu kama alivyoiombea Mtume Muhammad (saw) akisema:

«اللَّهُمَّ بَارِكْ لَنَا فِي شَامِنَا ويَمَنِنَا» “Ewe Mwenyezi Mungu! Tubarakie Sham yetu maYemen yetu.”

Je, vipi na kwa nini wanasiasa hawa wanasubutu kunyoosha mkono wao waziwazi kwa mashirika ya kigeni wakati ambapo sauti zetu zimepaa kuwaonya watu wa Yemen kuhusu kushadidi mzozo wa kimataifa juu yao? Mzozo huu ni pamoja na ukoloni mkongwe wa kijeshi ulioondoka pamoja na askari wake lakini ukabaki na ushawishi wake wa kisiasa, na ukoloni mpya wenye sura mpya ya kiuchumi, kithaqafa, kijamii, na kielimu ambao umekuwa ndio mzizi wa masaibu yetu kwa zaidi ya miongo sita. Katika kipindi hiki, Yemen imeshuhudia vita vya ndani vya kuendelea na vya mara kwa mara kwa miongo kadhaa, na nchi hii ingali inakabiliwa na mgogoro mkubwa unaotishia kuiangamiza kabisa.

Kanuni msingi, enyi watawala, ni kwamba wananchi wa Yemen wamekukabidhini nyinyi na kukuteueni msimamie masuala yao ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na mambo ya nje ya nchi pamoja na majukumu mengine. Kanuni msingi ni kwamba munapaswa kuwatawala watu kwa mujibu wa Aqidah yao tukufu ya Kiislamu. Hata hivyo, mumeupa mgongo Uislamu na kuwatawala watu kwa mujibu wa mfumo wa kibepari. Sasa, mnamwalika jhata kafiri Magharibi kuwatawala wananchi.

Je, hili linawafurahisha watu wa Yemen, au wana maoni tofauti na wanayofanya wanasiasa na wanauchumi sasa? Wanajua kwamba Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

 [وَلَنْ يَجْعَلَ اللهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلاً] “wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [An-Nisa:141] Hivyo basi, watu wa imani na hekima hawana budi ila kukukataeni nyinnyi kama mtu anatupavo mbegu, na kufanya kazi pamoja na Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ili tupate kutawaliwa kwa Uislamu. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal:24].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu