Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
H. 2 Dhu al-Hijjah 1445 | Na: HTY- 1445 / 32 |
M. Jumamosi, 08 Juni 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Vita vya Kiuchumi vinavyoongezeka kati ya Pande Zinazopigana kwa Gharama ya Watu wa Yemen
(Imetafsiriwa)
Benki Kuu ya Yemen, inayoshirikiana na ile inayoitwa serikali halali ya Aden, ilitoa maamuzi mawili mnamo Alhamisi, Mei 30, 2024. Uamuzi wa kwanza unaamuru kusitishwa kwa shughuli na benki sita zenye makao yake makuu katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi la Houthi. Benki hizi ni: Benki ya Tadhamon, Benki ya Yemen-Kuwait, Benki ya Yemen na Bahrain ya Shamil, Benki ya Al-Amal Microfinance, Benki ya Kiislamu ya Al-Kuraimi Microfinance, na Benki ya Kimataifa ya Yemen. Benki hizo zilipewa makataa ya siku 60 kuhamisha makao yao makuu hadi Aden. Kukosa kufuata sheria hiyo kutasababisha adhabu chini ya Sheria ya Kupambana na Ulanguzi wa Pesa na Ufadhili wa Ugaidi. Uamuzi wa pili unahusu kuondoa toleo la zamani la sarafu ya Yemen inayozunguka kwa sasa katika maeneo yanayodhibitiwa na Mahouthi ndani ya miezi miwili.
Kwa upande mwingine, Benki Kuu ya Yemen jijini Sanaa, ambayo iko chini ya udhibiti wa kundi la Houthi, ilitoa uamuzi wa kupiga marufuku shughuli na benki 13. Benki hizi zilituhumiwa kwa kuendesha shughuli za kibenki bila leseni na kukiuka masharti ya Sheria ya Kupambana na Ulanguzi wa Pesa na Ufadhili wa Ugaidi. Benki Kuu jijini Sanaa pia ilizituhumu benki hizi kwa kujihusisha na taasisi zinazoshutumiwa kimataifa kwa ufisadi, ulanguzi wa fedha, na kufadhili makundi ya kigaidi, pamoja na kukabidhi data za kifedha kwa nchi na mashirika hasimu. Kutokana na hali hiyo, Benki Kuu iliamua kuzipiga marufuku taasisi za fedha za ndani na nje na zisizo za kifedha kuamiliani na benki zifuatazo: Benki ya Kiislamu Al-Qutaibi Microfinance Bank, Benki ya Al-Basiri Microfinance, Benki ya Kiislamu ya Aden Microfinance, Benki ya Kwanza ya Kiislamu ya Aden, Benki ya Kitaifa ya Yemen – Aden, Benki ya Mikopo ya Ushirika na Kilimo, Aden, Benki ya Kiislamu ya Inclusion Microfinance, Benki ya Kiislamu ya Mtaji ya Salam Microfinance, Benki ya Tamkeen Microfinance, Benki ya Development Microfinance, Benki ya Kiislamu ya Eastern Yemen Microfinance, Benki ya Hadramout Commercial na Benki ya Kiislamu ya Bin Dawl Microfinance.
Imepita miaka miwili tangu mapatano kati ya pande zinazozozana nchini Yemen, yakisimamiwa na Umoja wa Mataifa, kuanza. Hapo awali yaliwekwa kwa kipindi cha miezi miwili kukiwa na uwezekano wa kuongeza muda, mapatano hayo yalilenga kusitisha operesheni za kijeshi, kusimamisha nyadhifa za kijeshi, kuruhusu uingiaji wa mafuta kwenye bandari za Hodeidah, na kufungua tena Uwanja wa Ndege wa Sanaa kama hatua ya kwanza. Hatua zilizofuata zilipaswa kujumuisha kufungua barabara, kulipa mishahara kwa wafanyikazi, na kufikia makubaliano kuhusu masuala ya kiuchumi kati ya wahusika. Licha ya kuongezwa mara kadhaa kwa mapatano hayo, hakuna makubaliano yaliyofikiwa ili kupunguza mateso ya watu wa Yemen hadi leo.
Watu wa Yemen wamevumilia matatizo makubwa tangu vita vilipoanza zaidi ya miaka tisa iliyopita, mzozo uliochochewa na dola za kikoloni-Marekani na Uingereza-kupitia wakala wao wa ndani, Mahouthi na ile inayoitwa serikali halali na zana zake. Ushindani huu mkali kati ya wakoloni wa kudhibiti rasilimali za nchi umeleta mateso makubwa, ikiwa ni pamoja na vifo, uharibifu, taabu, njaa, umaskini, ukosefu wa ajira, kuzorota kwa huduma, na hali mbaya zaidi ya afya na maisha duniani. Hata hivyo, pande zinazopigana bado hazijali, hazionyeshi rehema wala huruma kwetu!
Vita vya kiuchumi, ambavyo vimegharimu maisha zaidi ya vita vya kijeshi, sio maendeleo ya hivi karibuni. Mapambano ya kiuchumi yalianza kwa kuhamishwa kwa Benki Kuu hadi mji mkuu wa muda, Aden, mnamo 2016. Hii ilifuatiwa na mgawanyiko wa kifedha mwishoni mwa 2019 wakati Mahouthi walipopiga marufuku sarafu iliyochapishwa na serikali iliyoitwa halali, na kusababisha mifumo miwili ya viwango vya ubadilishanaji: mfumo ulio thabiti kiasi katika maeneo ya Sanaa na mfumo tete, unaozorota katika maeneo ya Aden, na tofauti kati yao hivi karibuni ikizidi mara tatu. Sera hizi, miongoni mwa zengine, zimesababisha kuongezeka kwa viwango vya mfumko wa bei ya bidhaa na huduma, na kuongeza mzigo kwa watu wa Yemen, ambao hawana hisa katika mzozo huu.
Huku mapigano ya mstari wa mbele yakipungua, mzozo wa ndani umehamia mbele ya uchumi. Mgogoro huu sasa ni kati ya pande za kusini zinazoungwa mkono na Imarati (UAE) na Uingereza, na upande wa kaskazini unaoungwa mkono na Iran, Wasaudi (kwa siri), na Marekani. Mifumo ya fedha na benki iko mstari wa mbele katika mapambano haya ya kiuchumi. Maamuzi ya Benki Kuu yenye makao yake makuu mjini Aden yameimarisha kamba karibu na Mahouthi, ambao, kwa kujibu, pamoja na wafuasi wao, watafanya kazi kukabiliana na kuepuka vikwazo hivi.
Vita vya kiuchumi kati ya pande zinazopigana vinazidi kuongezeka, na maamuzi haya yatasababisha upotevu wa pesa za waweka amana na kuongezeka kwa bei huku kukiwa na kukosekana kwa mishahara katika maeneo yanayodhibitiwa na Mahouthi. Katika maeneo yanayoitwa ya serikali halali, mishahara haikidhi gharama za msingi, na gharama kubwa ya maisha inakandamiza maisha ya watu. Wahasiriwa wakuu ni watu wa Yemen, ambao hawana nguvu katika hali hii. Dhurufu na matukio haya ni mazito kiasi cha kuwaamsha wafu na kusikiwa na viziwi.
Tatizo kubwa liko kwenye mfumo wa kibepari uliolazimishiwa watu, ukiwemo mfumo wa kiuchumi. Suluhisho haliko katika uunganishaji upya benki kuu na sarafu au kutoa tu mishahara na marekebisho mengine ya juu juu. Suluhisho lipo katika kuung’oa mfumo huu wa dhulma na wale wanaoshikamana nao, na kuubadilisha kwa mfumo wa Kiislamu chini ya Dawlah (Dola) inayoutekeleza kikamilifu na kwa upana.
Enyi Watu wetu katika Yemen: Makundi yanayopigana yanajali tu kuwatumikia mabwana zao, bila kujali mateso yetu. Wanaishi kwa anasa, bila kuathiriwa na kushuka kwa thamani ya sarafu au gharama kubwa ya maisha, huku wakituacha sisi kubeba mzigo wa shida. Wamechukua udhibiti wa maisha yetu, wakiamuru kila nyanja. Njia yetu pekee ya kutokea ni kupitia masuluhisho ya kimsingi ya migogoro na matatizo haya kwa kutabikisha mfumo wa Kiislamu, ambao lazima usimamishwe kupitia Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Dola hii itaokoa nchi yetu na ulimwengu kutokana na mateso na kuleta baraka na ustawi. Kwa hiyo, Hizb ut Tahrir inakuombeni mufanye kazi nayo kwa ajili hii, ikitumai kwamba Mwenyezi Mungu atatoa ushindi hivi karibuni, na kuifanya iwe uhalisia unaokirimu Uislamu na watu wake. Ewe Mwenyezi Mungu, yafanye hayo kuwa mapema kuliko baadaye.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal:24].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Wilayah Yemen
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Yemen |
Address & Website Tel: |
E-Mail: yetahrir@gmail.com |