Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 504
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Licha ya mateso tunayoyapata kutokana na yale yanayowapata ndugu zetu wa Gaza na madhehebu ya Mayahudi ambao wamekuwa wabaya kwa muda mrefu, dhalimu wa Uzbekistan anajitokeza dhidi yetu kwa kuwakamata mashababu wa Hizb ut Tahrir na kuwatishia kwa vitendo vya ukandamizaji ni yale yale waliyoshtakiwa kwayo na Karimov aliyekufa, na ambayo walifungwa kwa karibu miaka ishirini, mashtaka ya kubuni ambayo hayana ushahidi.
Ushiriki wa Hizb ut Tahrir/Uswidi katika amali za kampeni ya kilimwengu iliyozinduliwa na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir yenye kichwa “Enyi Umma; Kilio Wanacholia Wafungwa wa Dhamiri nchini Uzbekistan!”
Kushiriki kwa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika amali za kampeni ya kilimwengu iliyozinduliwa na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa kichwa, “Enyi Ummah; Kilio Wanacholia Wafungwa wa Dhamiri nchini Uzbekistan!”
Kalima kutoka kwa Ustadh Mahmut Kar, Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki, akiwawajibisha wahalifu waliowasha moto wa ufisadi katika mji wa Uturuki wa Kayseri baina ya wahamiaji wa Syria na wakaazi wa Uturuki ambao umeenea hadi miji mingi ya Uturuki.
Jana, Jumamosi, tarehe 6 Julai 2024, lile linaloitwa Kongamano la Kisiasa na Majeshi ya Kiraia ya Sudan lilifanyika katika mji mkuu wa Misri, Cairo; nukta muhimu katika taarifa ya mwisho zilizotolewa zilikuwa: “...wanakongamano pia walisisitiza ulazima wa kushikamana na Azimio la Jeddah na kuzingatia taratibu za utekelezaji na maendeleo yake ili kuendana na maendeleo katika vita…
Vyombo vya usalama nchini Uzbekistan vimewakamata tena wanachama 23 wa Hizb ut Tahrir na kuendelea na taratibu za kesi zao Mei 9 2024 kwa mashtaka yale yale waliyoshtakiwa wakati wa enzi ya dhalimu aliyefariki Karimov. Mashababu hao tayari walikuwa washatumia karibu miaka 20 jela na mateso tangu 1999 - 2000 M.
Vyombo vya usalama nchini Uzbekistan vimewakamata tena wanachama 23 wa Hizb ut Tahrir na kuendelea na taratibu za kesi zao Mei 9 mwaka huu kwa mashtaka yale yale waliyoshtakiwa wakati wa enzi ya dhalimu aliyefariki Karimov, ambayo kwayo walitumia karibu miaka 20 jela na mateso tangu 1999 - 2000 M.
Bajeti ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa imezua Balaa kwa Waislamu! Hukmu za Uislamu ndizo pekee zilizo na uwezo wa kuhafifisha migogoro mikubwa ya kiuchumi.