Jumatano, 15 Rajab 1446 | 2025/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ukombozi wa Konstantinopoli Tukio Muhimu Katika Maisha ya Ummah wa Kiislamu

Umuhimu wa matukio katika maisha ya Ummah wa Kiislamu hutofautiana kutoka tukio moja kwenda jingine, kama katika mapambano yake yalio muhimu zaidi kutoka kwa yale mapambano yaliyobakia. Miongoni mwa vita muhimu zaidi ni vita vya Badr, Al-Khandaq, Yarmouk, Al-Qadisiyah, Warsaw, Ain Jalut, Hittin, Konstantinopoli. Na miongoni mwa mapambano muhimu yajayo, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, kupigana na Mayahudi na kuikomboa Roma.

Vita vya Badr ni vita muhimu zaidi katika historia ya Uislamu, kwani kupitia kwake, Mwenyezi Mungu (swt) ameutukuza Uislamu na harakati yake na kuudhalilisha Ukafiri na harakati yake. Badr ilikuwa ndio siku ya upambanuzi (Furqan), Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

[يَوْمَ الْفُرْقَانِ يَوْمَ الْتَقَى الْجَمْعَانِ]

“Siku ya kipambanuo, siku yalipo kutana majeshi mawili.” [Al-Anfal:41] Ni siku ambayo bendera ya Uislamu ilisimama juu, nguvu za Waislamu ziliimarika, nguzo za Dola yao zikawa thabiti, na uwezo wao umeweza kujulikana zaidi, hivyo hofu ilivamia nyoyo za makafiri na wanafiki, kwa kuwa siku tukufu ya Idd al-Fitr katika mwaka wa pili wa Hijrah ilikuwa ndio Idd ya mwanzo katika historia ya Waislamu aliyoiweka Mwenyezi Mungu (swt), siku chache baada ya ushindi wa Waislamu katika vita vikubwa vya Badr.

Ama kuhusu Vita vya Al-Khandaq, ambapo washirikina walishindwa vibaya mno, Mwenyezi Mungu (swt) aliwapelekea upepo na askari wasiowaona; kwa hivyo, ushindi wa Waislamu katika hilo ulikuwa dalili ya kuwa Dola ya Kiislamu imekuwa ina nguvu zaidi ya maadui wote wakichanganywa.

Ama kwa Vita vya Yarmouk, ushindi wa Waislamu dhidi ya Waroma ulikuwa ni ushindi mzuri mno, na siku hiyo ilikuwa mwanzo wa kurejea nyuma kwa Himaya ya Waroma, ambayo ilikuwa ndio Dola Kuu duniani wakati huo.

Ama kwa Vita vya Al-Qadisiyah, vimeiangamiza Himaya ya Wafursi, iliyokuwa dola kuu ya pili duniani, ikishindana na Waroma katika nafasi ya kwanza.

Ama kwa Varsco, ambapo Waislamu waliwashinda watu wa Msalaba, pia Ain Jalut, ambapo Waislamu waliwashinda Watartar baada ya kuweza kuiangusha Khilafah ya Abbasiya katika Baghdad, ikiachwa Misri kuwa ni ngome ya karibu ya kuulinda Uislamu na Waislamu, na kama watu wa Msalaba au Watartar wangeweza kuwashinda Waislamu Misri, wangeichukuwa Makkah na Madina na kuangamiza Uislamu na Waislamu. Lakini Mwenyezi Mungu (swt) aliupatia na kuujaalia Ummah huu viongozi wakubwa kama Seif al-Din Qutz (Mahmoud bin Mamdud) aliyeongoza mwenyewe vita vya Ain Jalut, na kuwashinda Watartar kwa kishindo, na hivyo kuzihifadhi ardhi za Waislamu kutokana na uovu wao.

Katika Vita vya Hittin, Waislamu waliwashinda watu wa Msalaba, ushindi wa kukata ukiongozwa na Salahuddin Al-Ayyubi, aliyeikomboa Al-Quds, ambayo ilitekwa na watu wa Msalaba kwa miaka 88. Kushindwa huku kulimaliza uwepo wao Al-Sham ambapo waliweza kukaa kwa kipindi kifupi baadaye Al-Nassir bin Qalawun hatimaye aliwatoa.   

Kwa upande wa kukombolewa Konstantinopoli, ilikuwa ni siku muhimu ya mabadiliko katika historia ya Waislamu. Uislamu uliingia Ulaya kwa kishindo baada ya kufungika Andalusia, ambako Uislamu uliikomboa katika kipindi cha Khilafah ya Umayyah, kisha baada ya karne ya nane, makafiri waliwatoa Waislamu huko. Kadhalika, kukombolewa Konstantinopoli kulitanua upeo wa ukombozi katika Ulaya na ulikuwa umejifunga katika maeneo machache yaliyo kombolewa wakati wa Viongozi wa Uthmaniya kabla ya Muhammad al-Fatih. Ukombozi wa Kostantinopoli ulikuwa pia ni mshindo wa radi ulioishtua Ulaya yote, ambayo kwa wakati huo ikiathiriwa na ushindani wa utaifa na wa kidola, hivyo ukombozi wa Konstantinopoli umeiyumbisha na kuitikisa kwa nguvu, ikiungana kwa hofu ya ukubwa wa Uislamu wa kuifuta yote.

Kutokana na umuhimu wa ufunguzi wa Konstantinopli, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitoa bishara ya kukombolewa kwake. Abdullah bin Bishr Al-Khath’ami amepokea kutoka kwa baba yake kuwa alimsikia Mtume (saw) akisema:

  «لَتُفْتَحَنَّ الْقُسْطَنْطِينِيَّةُ، وَلَنِعْمَ الْأَمِيرُ أَمِيرُهَا، وَلَنِعْمَ الْجَيْشُ ذَلِكَ الْجَيْشُ»

“Hakika mtaikomboa Konstantinopoli. Amiri bora alioje Amiri huyo, na jeshi bora lilioje jeshi hilo! Akasema, hivyo Maslamah bin Abdul-Malik aliniita na kuniuliza, na nilimsimulia (hadith hii), kisha akaivamia Konstantinopli, (kutoka kwa Ahmad). Bishara hii ilifanikishwa na Muhammad II, ambaye, baada ya kuikomboa akaitwa “Al-Fatih”. Sheikh wake na mshauri wake, Aq Shams al-Din, ameingiza mapenzi ya Jihad na ukombozi, na kuwa yeye angeweza kuwa ndio mkombozi wa Konstantinopoli kuipata bishara ya Mtume na kuwa ni mmoja wa kukamilisha ahadi hii. Bila shaka, ufunguzi umekamilishwa naye. Mwenyezi Mungu (swt) amemtukuza kwa hili, na kwa ukombozi huo imeonyesha kuwa amestahiki pongezi za Mtume (saw), hivyo mkombozi alikuwa kweli kiongozi bora na Amiri bora na askari wake walikuwa kweli ni askari bora na jeshi bora. Konstantinopoli ilikuwa ni yenye umuhimu mkubwa, kwa sababu ilikuwa ni mji imara, uliokingwa kwa kuta zake ndefu zinazozuwia kupenya kwa jeshi lolote, na kama dunia yote ilikuwa ni dola moja wakati huo, Konstantinopoli ingekuwa mji wake mkuu.

Waislamu walijaribu kuikomboa tokea mwanzoni mwa Uislamu. Katika mfululizo wa (Khilafah) ya Muawiyah, jeshi la Waislamu lilikuwa ni jeshi la kwanza kuivamia Konstantinopoli kwa mategemeo ya kukamilisha bishara ya Mtume (saw).

Masiku haya yanaashiria maadhimisho ya Ukombozi wa Konstantinopoli, ambao unatukumbusha ukubwa wa Uislamu uliowatengeneza viongozi wa dola kama Muhammad al-Fatih, na hakika, ukombozi huu ni kitangulizi cha uhakikisho wa bishara nyingine, inayojumuisha kurejea kwa Khilafah

 «... ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» 

“Kisha itarejea Khilafah kwa njia ya Utume…” imepokewa na Ahmad, kupigana na Mayahudi na kuwashinda kwa namna ambayo hawatokuwepo tena baada ya hapo, na kufunguliwa Roma, ambayo itafuatiwa na kujisalimisha kwa Ulaya yote kwenye Uislamu na kuingia kwa watu wake ndani yake baada ya kuwa ni kizuizi kikubwa kilichozuwia utanuzi wa Uislamu ndani yake, na kuwa suala hili halitofanikishwa hadi baada ya kusimamishwa kwa Khilafah Rashidah ya pili kwa njia ya Utume ambayo Hizb ut Tahrir inafanya kazi usiku na mchana, hadi Mwenyezi Mungu aubarikie Ummah kwa ushindi wenye kufuatana na wenye nguvu. Siku hiyo ipo karibu, na tarehe ya ushindi ni yenye kutokea upesi, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Shayef Al-Sharady – Yemen

#ConquestofIstanbul

#Constantinople

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 10 Mei 2020 11:44

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu