Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wito wa Khilafah Kutuunganisha ni wa Kiulimwengu Hivi Sasa

Ikiashiria Kurudi Kwake Kuwa Dola Kuu Inshaallah

Katika kukamilisha miaka mia ya kalenda ya Hijri ya kuvunjwa kunakoumiza kwa Khilafah, Hizb ut Tahrir imetekeleza kampeni kubwa ya kilimwengu ikitaka kurejeshwa kwake. Ndani ya Ulimwengu wa Kiislamu, ndugu wa kike na kiume wa Hizb ut Tahrir kutokea Tunisia upande wa magharibi hadi Indonesia kwa upande wa mashariki wamegawanya nyezo mitaani, pamoja na kwenye mitandao ya kijamii, huku wakitekeleza kampeni pana ya mashinani. Kwa Waislamu wanaoishi ugenini kwenye nchi za Magharibi pia, Mashababu wa Hizb ut Tahrir walinyanyua wito wa Khilafah kwa Njia ya Utume, ukionyesha kweli kwamba umefika dunia ni kote.

Kwa rehema za Mwenyezi Mungu (swt), wito ulikuwa wenye nguvu na ulipokewa vizuri, ukichochea Ummah na mjadala mpana kuhusu kutoweka kwa Khilafah.

Kwa hakika, Waislamu wamehisi hasara kubwa ya kuondokewa na Khilafah kwa ufahamu wenye nguvu. Tokea kuanguka kwa Khilafah mwaka 1342 Baada ya Hijra, inayowafikiana na 1924 Kalenda ya Miladi, Ummah Mmoja umegawika katika nchi zaidi ya hamsini, baadhi yake zina idadi ya watu chini ya idadi ya walio kwenye miji mikuu katika Ulimwengu wa Waislamu. Kwa nini tusiihisi hasara ya Uislamu ukiwa kama dola na mamlaka ya kutuunganisha sisi?

Sisi hivi leo kwa hakika tumedhoofishwa kwa mgawanyiko wa sasa, kama walivyokuwa Ansaar kabla ya kutawaliwa na Uislamu. Mtume (saw) aliwakumbusha Ansaar wakati wa Hunayn akisema,

«يَا مَعْشَرَ الْأَنْصَارِ أَلَمْ أَجِدْكُمْ ضُلَّالًا فَهَدَاكُمُ اللهُ بِي، وَكُنْتُمْ مُتَفَرِّقِينَ فَأَلَّفَكُمُ اللهُ بِي، وَعَالَةً فَأَغْنَاكُمُ اللهُ بِي؟»

“Enyi Ansaar! Sijakukuteni nyinyi mmepotea na Mwenyezi Mungu akakuongozeni kwa sababu yangu? Na mlikuwa mmegawanyika na Mwenyezi Mungu amekuunganisheni kupitia mimi? Na hamkuwa masikini na Mwenyezi Mungu akakutajirisheni kwa sababu yangu? [Bukhari]. Kila ambapo Mtume (saw) alipowauliza suali walijibu, «اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمَنُّ» “Hakika, Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wametukirimu”

Ni wakati wapiganaji wa ki-Ansar walipotoa Nussrah kusimamisha Uislamu ikawa ni dola na mamlaka, ndipo Waislamu waliweza kuunganishwa kivitendo na kuwa na nguvu dhidi ya maadui zao. Hivyo, Ummah wa Kiislamu uliounganishwa uliweza kuwashinda maadui wao walio na nguvu kwa ushindi wa wazi, huku watu wake wakiukumbatia Uislamu kwa hiyari makundi kwa makundi, bila kushurutishwa.

Bila shaka, uwepo wa kiwango kikubwa cha Ummah wa Kiislamu hivi leo, wenye lugha na asili zilizotafauti, ni ushahidi wa wazi wa ukarimu wa Uislamu.

Angalia hali yetu hivi leo, je ni kama ya Ansaar? Hatuishi katika machungu chini ya mifumo iliopotoka, ya kifalme, ya kidikteta na kidemokrasia? Hatuungui ndani ya moto wa migawanyiko, tukihitajia umoja chini ya Khalifah? Hatujafukarishwa kwa kukosa kuhukumiwa Kiislamu, hali ya kuwa utajiri wa dunia upo chini ya ardhi zetu?!

Je, hatupo katika hitajio kubwa kwa wapiganaji wetu, mamilioni ya vikosi katika majeshi ya Waislamu, kujitokeza mbele hivi sasa na kutoa Nussra yao kwa ajili ya kutawaliwa na Uislamu? Hakika ni wakati muwafaka kwa watoto wa Ansaar wa vita kutoa Nussra kwa Hizb ut Tahrir, ili hatua ya kuelekea kuueneza Uislamu iendelee baada ya kisimamo kichungu cha miaka mia moja Hijri.

أقيموا_الخلافة#
#ReturnTheKhilafah
#YenidenHilafet
خلافت_کو_قائم_کرو#

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Musab Umair – Wilayah Pakistan

  

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu